TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya

kufundisha mawe si kazi rahisi
 
Hao Twaweza wamethibitisha utafiti wao na Mtwakimu Mkuu wa Serikali? Tuanzie hapo.
 
Ila sijaona chama Cha kumbukumbu Kama ccm mchakato wa katiba waliuanzisha wao wakausimamia wao walipoona ohooo hii katiba itatuchinja wenyewe wakalitelekeza jangwani.
Hivi mwenyekiti wa bunge lile la katiba alikuwa ni nani mkuu?Nataka nimuandikie waraka.
 
Kilichofuata mkurugenzi wa TWAWEZA sio raia wa Tanzania! 😀😀😀

 
Watuonyeshe maswali walio uliza kwenye utafiti huo wa kisomi. Watu wengine hatuelewi Katiba Mpya ni nini na itatuletea maendeleo yapi? Kaziendelee inaeleweka - madarasa yatajengwa, barabara bora vijijini, huduma za afya bora vijijini, miradi mikubwa itamalizwa, maji safi kwa watanzania wengi na kadhalika. Faida za katiba mpya............mimi naona hasara tu za mchakato wa katiba mpya, mabillioni ya pesa yatatumika kuendeleza mchakato wa katiba mpya.
 
Kiufupi unahitaji elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya!Hujachelewa,uwe unafuatilia yanayojadiliwa kwenye makongamano ya katiba mpya!Au unaweza kurudi nyuma na kutafuta rasimu ya Warioba kabla haijachakachuliwa utapata ufahamu!
 
Weka hapa ripoti yao tuidadavue...sample population yao pengine ni mkutano wa viongozi wa Chadema
 
 
Akili kama hizi ndizo zinazoirudisha nyuma Taifa. Hizo mentioned zako zilikuwepo zinafanyika kabla ya UHURU.

Laiti ungezijua sababu za kudai UHURU usingepinga swala la katiba mpya.

Leo hii viongozi wamekuwa kama wakoloni wao ndio wanaamua na kupanga kila kitu pasipo kujiuliza wala kuwajali wananchi. Mfano wa Tozo wameamua na kuipitisha pasipokusikiliza maoni ya wananchi.

Sio kila jambo linajadiliwa kwa engo ya kichama au ushabiki, sometimes you have to face reality
 
Asipokuelewa hapa basi ameshindikana
 
Low minds ndivyo wanavyofikiria. Ukimwuliza low mind nikupe nini, nikulipue ada ya chuo, ukasome au nikupe magunia ya udaga, atachagua udaga.

Hayo uliyoaandika ni uthibitisho kuwa uwezo wako wa tumbo umefifisha uwezo wa kichwa.
 
Weka hapa ripoti yao tuidadavue...sample population yao pengine ni mkutano wa viongozi wa Chadema
Umezaliwa lini?

Ile report ya Jaji Warioba, iliyotokana na wajumbe kuzunguka nchi nzima, wakikutana na makundi yote ya jamii za Watanzania, ilionesha kuwa watanzania wengi wanataka katiba mpya. Hata wale ambao hawakusema moja kwa moja kuwa wanataka katiba mpya, mambo waliyoyataka yawekwe kwenye katiba, tafsiri yake ilikuwa ni lazima utengeneze katiba mpya.

Kwa hiyo, hii report ya TWAWEZA, ni uthibitisho wa yale tunayoyajua kupitia Tume ya katiba mpya ya Jaji Warioba.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Ccm na viongozi wake wanafikiri katiba mbaya iliyopo sasa itawaumiza wengine. Ipo siku watajuta kwamba hawakuandaa katiba nzuri kwa ajili yao na watoto wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…