Vodacom Tanzania
Official Account
- Aug 12, 2013
- 324
- 126
Wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 25 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vodacom Tanzania na Klabu ya Baiskeli ya ‘Twende Butiama’ tunaendelea na msafara wa waendesha Baiskeli kuanzia Septemba 28 na tutafika kikomo Oktoba 14 huko Butiama. Lengo ni kuadhimisha urithi wa Baba wa Taifa kupitia uendeshaji baiskeli, shughuli za kijamii na hisani.
Msafara huu wa Twende Butiama ulianzishwa mwaka 2019 na kikundi cha waendesha baiskeli, ili kuadhimisha upendo wa Mwalimu Nyerere wa kuendesha baiskeli na maono yake kimaendeleo katika maeneo matatu muhimu ambayo ni elimu, afya na utunzaji wa mazingira ambayo yanaweza kuwasaidia Watanzania kupiga hatua kijamii na kiuchumi.

Pia soma: Vodacom Twende Butiama 2024: Zaidi ya Waendesha baiskeli 100 waanza Safari ya Dar - Butiama
Kwa mwaka wa pili mfululizo Vodacom Tanzania tumekuwa Mdhamini Mkuu wa msafara huu ambapo kwa mwaka jana, tulifanikiwa kupanda miti zaidi ya 6,000, na kutoa huduma za afya kwa watu zaidi ya 3,200 katika Wilaya tatu ndani ya mikoa ya Mwanza na Mara. Pia, tukio hilo liliambatana na utoaji wa jumla ya madawati 610 katika shule 13 za msingi. Juhudi hizi zinaendana na malengo ya Vodacom Tanzania ya kuwawezesha watu na kulinda ustawi wa sayari yetu.
Mwaka huu, tunajivunia kuendelea kuwa sehemu ya jambo hili linalochangia kuleta mabadiliko Chanya kwenye jamii. Msafara wa mwaka 2024 umepanua wigo, kujumuisha mafunzo ya ujuzi wa kidijitali na kambi za matibabu zitakazohusisha uchunguzi na elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwenye mikoa 12 nchini.

Pia soma: Jumamosi ya kesho asubuhi safari ya baiskeli ya Dar kwenda Butiama itaanza
Katika suala la Afya, Vodacom Tanzania imeandaa kempu za afya ambazo zitatoa huduma mbalimbali zikiwemo Upimaji, uchunguzi wa awali na pia rufaa zinatakuwa katika mikoa 7 huku katika kila mkoa Wataalamu wakitarajiwa kukaa kwa siku 3 hadi 6 kutokana na uhitaji wa watu. Usisahau huduma katika Kempu hizi ni BURE KABISA
Kwa siku zilizobaki Kempu hizi zitakuwa katika maeneo yafuatayo.
Kwa siku zilizobaki Kempu hizi zitakuwa katika maeneo yafuatayo.
| Mkoa | Eneo la Kempu | Siku |
| Singida | Singida Mjini, Viwanja vya Bombadia | Octoba 7 – Octoba 12 |
| Kagera | Biharamulo, Viwanja vya Bihalamuro stendi ya Basi | Octoba 13 – Octoba 15 |
| Geita | Chato, Hospitali ya Chato | Octoba 15 – Oktoba 17 |
Wananchi wote wanakaribisha kujankupatiwa huduma za Afya kwenyeb kempu hizi ambapo pamoja na vipimo watapatiwa mwongozo mzuri wa afya ili kufikisha malengo ya kujenga jamii yenye afya.
Ungana nazi kwenye huduma hizi kupitia Twende Butiama inayokusudia kupambana na maadui watatu wa maendeleo ya jamii: ujinga, umaskini, na maradhi.
Ungana nazi kwenye huduma hizi kupitia Twende Butiama inayokusudia kupambana na maadui watatu wa maendeleo ya jamii: ujinga, umaskini, na maradhi.
Pia soma: Vodacom Tanzania wamkaribisha Nwankwo Kanu kwenye ziara ya Twende Butiama
Mwaka huu, Waendeshaji baiskeli wanatarajiwa kutembea Kilometa 1,846 kutoka Dar es Salaam hadi Butiama. Wakati msafara huu ukipita katika maeneo mbalimbali nchini, utakuwa ukigawa madawati na kupanda miti ambapo jumla ya madawati 1,100 yatagawiwa kwa shule mbalimbali na jumla ya miti 50,000 itapandwa.
Msafara wa Waendesha Baiskeli uliotokea Dar Es Salaam ukiwa umefika Butiama
Msafara wa Waendesha Baiskeli uliotokea Dar Es Salaam ukiwa umefika Butiama