Twendendeni AFCON na singeli yetu.

Twendendeni AFCON na singeli yetu.

njundelekajo

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
310
Reaction score
227
Ni mwezi huu klabu ya Simba imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika,timu ya taifa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya mataifa ya Afrika na bondia mtanzania Hassan Mwakinyo amemdunda bondia Sergio Eduardo Gonzalez nchini Kenya kwa Knockout(KO) round ya tano.Mungu atupe nini kingine kwenye michezo?

Achana na mtanzania George Jonas anayefanya kazi kampuni ya ya Boeng nchini Marekani aliyepata tuzo ya muhandisi bora wa mwaka (Beya) ,tuzungumze kuhusu michezo na namna tunavyoweza kubrand vitu vyetu vya ndani kupitia mafanikio haya.

Nilimuona Simon Msuva,Mzee wa "miasist" papa John Raphael Bocco,Mngoni Erasto Nyoni na Le kaptein "mtu mbaya" Mbwana Ally Samatta wakiselebuka juu ya mirindimo ya Singeli.Ilisisimua sana kila muimbaji aliposikika anahadithia kisimu chake cha line mbili kinavyomsave,na namna vya wachezaji wa stars walivyoyarudi.

Pale muimbaji anaposema "ukiiba simu ya Hajibu na muziki utazimwa" Zinakuja picha za Manzese ya Dar,Mji Mpya ya Morogoro,Mihanzini ya Iringa,Ngamiani ya Tanga,Mwanza road ya Tabora na maeneo mengine ya nchi yetu yenye vibaka.

Ni muziki unaosisimua kwa mashairi yake,unagusa watanzania wengi tunaoshi uswahilini,unaelezea hasa vitu vinavyogusa hisia zetu."Unaringa unaringa una nini wewe?umekopa vikoba umeazima dera" Rejea haya mashairi ukiwa umefumba macho utanielewa.Ni muziki wa aina yetu wenye lugha yetu na unaotutambulisha.

Nikapata wazo na swali kwa nini tusitumie muda huu dunia inapotushangaa kwa mafanikio yetu tuliyoyapata kuipeleka Sungeli Misri na Kongo?.Ni suala la kuamua tu kwenye matukio yote ya michezo muziki wetu ni Singeli.

Fursa hazitokei tu huundwa,wakati wanashangaa soka letu sisi tunapenyeza muziki wetu.Wakati ndo huu,namkumbuka Reginald Mengi kwenye moja ya mazungumzo yake alisema "fursa zina haibu,zinakusubiri uzikimbilie".Tusiache fursa hizi za soka kutangaza mambo yetu mengine.Zitaona haibu zikimbie alafu tukajikuta hatujachukua kombe na hatujawauzia pia hata utamaduni wetu.

Tutapiga ndege wawili kwa jiwe moja,lugha na kukua kwa muziki wenyewe.Huenda tuna hofu ya kuchekwa na kukosolewa lakini ukweli ni kuna njia moja tu ya kuepuka kukosolewa,usifanye kitu,usiseme kitu na usiwe chochote .Hivyo tuchague mojawapo sidhani kama itakuwa kutofanya chochote.

Wachina wana msemo wao "muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita .Lakini muda mzuri wa pili ni sasa".Baada ya kushindwa kuwa na muziki wetu unaotutambulisha na wenye vibe la kitanzania miaka mingi nyuma,muda wa pili ni sasa kupitia Afcon na Klabu bingwa Afrika.

Twendeni Kongo( hapo tu Kigoma kwa mbele) na baadae Misri tukacheze sana Singeli tukiondoka waarabu na wakongo wamjue Man Fongo,Sholo Mwamba,Dogo Sikide na wengine.

Bongo fleva imetupeleka sehemu lakini isitupe sana kazi ya kuupiga ukuta tukitumai utabadilika kuwa mlango.Hatuna namna tunavyoweza kuufanya muziki wa bongo fleva ni wetu.Kuna miziki ikipigwq tu unajua hawa ni wakongo,hawa wasouth Afrika hawa ni watu wa Afrika Magharibi hiki kitu kimekosekana kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Twendeni tukapate mafanikio mengind kupitia Singeli.Tusiogope kwa sababu mafanikio ni kupita kutoka aina moja ya kushindwa hadi nyingine bila kukata tamaa.Tuna kibeku tayari cha Afcon na Klabu Bingwa tuipakie Singeli humo tusafiri nayo.Watu werevu wakitaka kufanya kitu hutafuta njia lakini wajinga hutafuta visingizio.Kama tuaacha kutumia njia tuliyoipata kuutangaza muziki wa Singeli basi nina hakika tumeshajiandaa kutoa visingizio kwa nani hatuna muziki unaotutambulisha.

Twendeni na Singeli yetu Ni bora kushindwa kwenye kitu halisi kuliko kufanikiwa kwenye kitu cha kuiga.Kujaribu kuitangaza Singeli na tukashindwa ni bora kuliko kujivunia miziki ya kigeni.

24/3/2019

Nguzo Noel ,R.
 
Wazo murua kabisa, nashauri fowadi kwenye email ya TFF na Hajj Manara kwa Upande wa Simba
 
Singeli sio utamaduni wa Mtanzania bana, Watanzania 90% hawapendi Singeli

Singeli inapendwa na vijana wa uswahilini ukanda wa Pwani, wachache sana, sasa utamaduni wa watu wa Pwani, sio utamaduni wa Tanzania
Tena Watanzania wengi wanadharau sana utamaduni wa Pwani,

Chuoni kuna mtu alikuwa katokea Morogoro ila ukimwambia bi mtu wa Pwani anakataa mnaweza mpigane

Maana wanawaona ni watu ambao hawajaenda shule, wana uhuni mwingi, umbea, umalaya, uvivu, umasikini, watu wa kujiachia na kuridhika na vichache, wasiofikiria kesho n.k.

Ukimuuliza Mtanzania sifa za watu wa Uswahilini Pwani (ambao ndio wapenzi wa Singeli) watakuambia waba sifa hizo hapo juu
So hawakubali kuwa ndio waende ku represent picha ya Watu wa Tz walivyo
 
wimbo unaitwa KISIMU CHANGU LAINI MBILI umeimbwa na mzee wa Bwax a.k.a Mtoto wa nje ya ndoa
 
Singeli sio utamaduni wa Mtanzania bana, Watanzania 90% hawapendi Singeli

Singeli inapendwa na vijana wa uswahilini ukanda wa Pwani, wachache sana, sasa utamaduni wa watu wa Pwani, sio utamaduni wa Tanzania
Tena Watanzania wengi wanadharau sana utamaduni wa Pwani,

Chuoni kuna mtu alikuwa katokea Morogoro ila ukimwambia bi mtu wa Pwani anakataa mnaweza mpigane

Maana wanawaona ni watu ambao hawajaenda shule, wana uhuni mwingi, umbea, umalaya, uvivu, umasikini, watu wa kujiachia na kuridhika na vichache, wasiofikiria kesho n.k.

Ukimuuliza Mtanzania sifa za watu wa Uswahilini Pwani (ambao ndio wapenzi wa Singeli) watakuambia waba sifa hizo hapo juu
So hawakubali kuwa ndio waende ku represent picha ya Watu wa Tz walivyo
Acha hizo wewe nani aliyekwambia asilimia 90 ya watanzania hawapendi singeli?Alaf unasema watanzania wengi wanadharau utamaduni wa pwani wakati pwani ndiyo chanzo cha ustaarabu,Mnakuja kuja mjini mkiota mapembe mnaongea saana.
 
Utamaduni gani wa Pwani ambao ni Ustaarabu? Uislam? Vigodoro? kushinda vibarazani?

Watu wa Pwani wana kitu gani bora cha kuwafunza watu wa bara?
 
Back
Top Bottom