Twiga Stars wamecheza vizuri sana. Viwango ni vizuri...style yao ya mashambulizi ya kushtukiza ni tamu mno. Kama refa asingewakatisha tamaa na mafilimbi yake ya offside...sasa hivi tungekuwa tunaimba akanana, na kucheza kiduku.
Tatizo kubwa nililoliona katika dakika kumi za mwisho ni kupoteza muda kana kwamba wanatafuta droo hivi. Hii ilipelekea mashambulizi mengi langoni mwao.
Twiga wanatakiwa wajue kwamba, Tanzania kwa kufika pale hatuna cha kupoteza. Wacheze mpira wao, na nina uhakika wanaweza wakafanya vizuri katika mechi zijazo.
Hongera dada zetu.