Ningependa kuchangia uzoefu wangu…
Twin turbo ina tumika kwa sababu ya Kupunguza turbo lag. Turbo lag ni kule kuchelewa kufunguka kwa turbo wakati gari ina panda kasi. Ukitaka gari iwe na nguvu unaweka turbo. Ukiweka turbo kubwa basi na power inaongezeka zaidi. Tatizo ni kwamba turbo kubwa ina chelewa kufunguka. Inachelewa kwasababu inahitaji kujenga pressure kubwa ya exhaust ili izungushwe kwa haraka.
Ingini ya gari ujenga pressure zaidi katika RPM ya juu. Na gari hua inachukua mda kufika RPM ya juu. Kuchelewa huku ndiko kuna sababisha kuchelewa kwa turbo kufunguka ili ianze kuiongezea power ingini. Ingini ikifika RPM ya kuifungua turbo, basi power inakuja kwa ghafla..booom. Power inaingia kwa nguvu na kwa ghafla, unaona kama vile "you suddenly being pulled on the chair", yaani kama vile tumbo linakatika hivi 🙂
Sasa tatizo ni kwamba, wateja wengi wa sports car hua hawapendi hiyo feeling ya “kukatika tumbo”. Kwahiyo basi, watengeneza magari wanaweka turbo ya pili ambayo ni ndogo na inafunguka mapema katika RPM ya chini. Kwasababu turbo ndogo haina power kama kubwa, basi mfunguko wake sio wa ghafla sana. Hii turbo ndogo ikifunguka mapema itaendelea kufunguka mpaka pale RPM ya ingini imepanda kiasi cha kutosha kufungua turbo ya pili ambayo ni kubwa. Turbo kubwa inafunguka na kumpokea mwenzake na kuendelea kujenga power zaidi. Matokeo yake ni kwamba dereva ana sikia "mfunguko nyororo" (smooth spooling).
Kwa ufupi basi, turbo mbili zinawekwa ili kuunda a "turbo system" ambayo inafanya mfunguko wa turbo usiwe wa ghafla. Tena basi, ni lazima zichaguliwe turbo ambazo zina endana ili kufanya mfunguko wa kushirikiana ulio nyororo yaani smooth. Moja kuwa moja ndogo.
Katika hobby hii, mimi nimeshabadili turbo kama nne katika gari yangu. Kwa wale mnao zijua turbo, mimi nilianza na T25, nika weka 16G, B16G, mpaka 20G. Nina spare ya FP20GRED ambayo nitaiweka pale nitakapoichoka 20G niliyonayo hivi sasa. Natumaini nimeweka mchango mzuri.
Asanteni na msisahau kutambika au angalao kuwashukuru mababu na mabibi zetu.