Twin turbo zinafungukaje

Ni mahususi kwa diesel engine, petrol hutumia supercharger kama sikosei
Mzee teknolojia imebadilika. Kuna gari ya gasoline ni turbocharger, supercharger na plug-in hybrid pia. Gari hii ina 401HP, 0-60 in 5.3 seconds with top speed ya 140mph. Hii Volvo XC T8.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, turbo inatokana na turbine engine, hizi ni teknolojia za kuunda engine ndogo yenye uwezo wa kuzalisha nguvu kubwa na kuongeza ufanisi (efficiency) wa matumizi ya mafuta. Hivyo ukiona gari inatoa moshi mwingi na gari hiyo ina engine yenye turbo, inamaana turbo hiyo haifanyi kazi sawa. Moshi mweusi ni matokeo ya mafuta ambayo hayajachomwa vizuri.

Turbo inafanya kazi kwa kutumia sensors. Sensors hizo husoma kinetic energy (velocity) ya moshi utokao katika exhaust pipe. Hivyo sensor zinaendana pia na RPM ya engine. Moshi unapofika katika level flani ya RPM, husababisha sensor kuruhusu turbines kuvuta hewa safi, iliyopozwa kuingia katika combustion chambers ili kuongeza mafuta yanayoendana na kiasi cha hewa na kuyaunguza, ili kutoa energy output inayohitajika na engine. At the same time, hewa iliyokwisha unguzwa hutolewa kupitia chamber nyingine nana kutolewa nje kupitia exhaust pipe. Kwa gari zenye intercooler, hewani safi hupitia kwenye intercooler kupoozwa zaidi, ili volume kuwa kubwa na kuongeza ufanisi zaidi katika kuchomwa kwake ktk engine.

Sasa twin turbo inamaana kuna turbo ya lower end and higher end RPM. Lower end, turbo imesetiwa kwa gear namba mbili, moja na unapokuwa katika 4wd. Higher end turbo sensor yake imesetiwa kwa gear namba 4, 5, na 6 kwa gari za kisasa, zenye uwezo wa kutoa output kubwa (Higher torque).
 
Mafundi ushuzi wa chini ya mwembe wanaelewa hayo Mambo kweli? au ndo kugonga gonga na nyundo tu magari ya watu?
 

Also, you have to set a reference pressure level, which mostly is based on intake manifold pressure. Kwenye gari yangu, turbo nimeiseti ku build pressure mpaka 22psi.

Baada ya hapo pressure ina kuwa released through the waste gate (kimlango kidogo ambacho kiko kwenye exhaust side ya turbo na kinafunguliwa na "waste gate actuator"). Hii part ni muhimu ili kuhakikisha una control pressure buildup. Otherwise utafumua cylinder head gasket😄
 
Kwahiyo hapo kuna parts kama waste-gate actuator na boost controller ambazo ni umuhimu katika kucontrol ujazo wa hewa kwenye engine. Waste-gate inapokea pressure signal from boost controller, ambayo ndio inasetiwa kuiambia waste gate iistopishe turbo at a particular pressure of your choosing. Kwa mfano, mimi nimeseti turbo controller yangu to signal the waste-gate when intake manifold pressure reaches 22 psi.
 
Nyongeza, sorry kama ni nje ya maada...
Ukichange turbo ili upate power zaidi, basi jua inabidi ubadilishe mlolongo mrefu wa parts nyingine ambavyo vinatakiwa kusupport turbo kubwa. Hii inahitaji uwe na roho ngumu 😄...

Kwa mfano, Lazima ubadilishe:
Exahust system
Fuel Injectors
Fuel pump
Engine computer modification
Clutch plate and Pressure plate
Bigger intercooler
All turbo pipes
Manual/electronic boot controller

Na kadhalika...
 
upo sawa kabisa skupingi kwa sababu kazi ya turbo ni kuongeza hewa kwa wingi kwenye cylinder na turbo inafanya kazi vizuri rpm ikiwa juu ndo tunasema turbo imefungua
 
Ubadili hata kama hizo parts hazina defects zozote?
 
Bro...unajua hadi unakera asee[emoji119]safii
 
Ubadili hata kama hizo parts hazina defects zozote?
Ndio, lazima ubadili ili kufikia power unayo itaka. Kitu kikubwa ambacho engine computer inafanya ni kumechisha air na petroli ili zikiingia kwenye engine ziilipuke vizuri kikemia (correct air/fuel ratio). Sasa ili kupata the right air/fuel ratio lazima injector zimachi na turbo. Ukiweka turbo kubwa basi injector nazo lazima ziwe kubwa. Lakini injector kubwa nazo zinahitaji fuel pump kubwa. Fuel pump kubwa nayo inahitaji umeme wa kutosha kwahiyo lazima ubadilishe wiring syste ili umeme uwe wa uhakika kwenye pump kubwa.

Pump kubwa nayo inahitaji fuel regulator mpya, maana original iliyokuja na gari haito himili pressure ya pump kubwa. Kwahiyo lazima uweke fuel pressure regulator ambayo unaweza adjust mwenyewe (mimi natumia ya kampuni na Fuel-Labs).

Hapo bado hujagusa mahitaji ya kupooza engine (bigher radiator, bigger intercooler, na hata water injection). Pia transmission lazima uiimarishe ili iweze kuhimili power/torque....

.... kwahiyo mlolongo wa kubadilisha parts unakua mrefu sana🤣🤣🤣🤣
 
Nimekuelewa chief. Ila swali langu lililenga kuelewa hoja ya kubadili hizo parts zingine endapo nimeweka turbocharger mpya yenye specs zilezile kama za turbocharger iliyopata defects.
 
Nimekuelewa chief. Ila swali langu lililenga kuelewa hoja ya kubadili hizo parts zingine endapo nimeweka turbocharger mpya yenye specs zilezile kama za turbocharger iliyopata defects.
Sorry,...hapana. nipale tuu unapoongeza turbo. Nahata hivyo una badilisha pole pole, kimoja kimoja pale unapoona kifaa kimeishiwa nguvu au hakihimili nguvu mpya ya gari. Ila mwisho wasiku inakubidi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…