KOMBAJR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 5,827
- 1,271
Abiria wanaotumia ndege za shirika la ndege maarufu kama Fast Jet zenye bei nafuu kuliko ndege zote nchini, huenda wakakosa huduma hiyo kutokana na shirika hilo kuwa hatarini kufungwa kutokana na kukiuka mkataba uliokuwepo kati yake na Fly540 Aviation Ltd. Sakata hilo limekuja baada ya kampuni ya Fly540 kutangaza kuondoa leseni yake iliyotoa kwa FastJet ili kuendesha shughuli za usafirishaji ktk anga la Tanzania, Angola, Kenya na Ghana.
Kuondolewa kwa leseni hiyo kunamaanisha kuwa FastJet sasa itapaswa kisheria kusimama kutumia alama au chapa zote za Fly540 Ltd, kampuni ambayo inasemekana iliuza hisa kwa mkataba ambao FastJet wameukiuka.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga, Fadhili Manonga, amethibitisha kupokea barua toka kwa makampuni yote mawili yaliyowekeana pingamizi za kisheria, huku Fly540 ikiitaka FastJet kuacha kutumia alama na chapa zake katika shughuli zake hapa nchini.
Source Tanzania Daima la Feb.08, 2013
ile ofisi pale samora pembeni ya steers ina nuksi kila co ya ndege inayopitia pale aidumu.hahahahaha community airline,540,fastjet na kabla ya hapo kuna nyingine nyingi zilipita hapo.poleni wazee wa 32,000.vya raisi huwa havidumu