Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,051
- 12,954
Mimi niko kwenye mitandao ya kijamii kadhaa kkiwemo Twitter kwa muda mrefu kidogo.
Hivyo kwa muda nilikua nikifurahia michango ya watanzania wenzangu ya kisomi kabisa Twitter na JF ila sasa Twitter imekua ya hovyo sijawahi kuona.
Twitter ya sasa imevamiwa na makundi ya wavuta bangi wanajiita wapwa, mabloo, yaani hakuna cha maana wanachokiandika zaidi ya kuomba wainuane, wainuane na wakishainuana mtu akawa na wafuasi kuanzia elfu 10 basi anabadili status anajiita motivation speaker.
Hii imechangiwa pakubwa kwa ujio wa bonanza za Tanzanians on Twitter. Hii bonaza ukiacha nia njema ya waanzilishi wake imeruhusu magenge ya wahuni na wavuta bangi kujipenyeza sasa wameharibu kabisa ladha ya Twitter. Zamani tulizoea parodies(wanaume kufungua account kwa majina ya kike na kuweka picha za kike) yalikua yamejazana facebook ila sasa yamehamia twitter, yamejiungana na mabloo na wapwa kuinuana imekua shida tupu.
Ni bora Instagram kuliko Twitter kwa sasa.