Mtandao wowote wa kijamii ukishaanza kutumiwa na watu wengi, tegemea kukutana na kila aina ya watu kwenye huo mtandao. Iwe watu wema, wabaya, matapeli, wajinga, wastaarabu n.k
Uzuri mitandao ya kijamii inakupa flexibility ya nani unataka umfollow/ uwe friend nae na nani uamue usiwe una-interact nae. Ukiona mtu huendani nae au msumbufu kuna option za kublock au mute.
Ukiwa na mtazamo kuwa mtandao fulani eti ina watu wastaarabu au inatumika na watu smart tu, basi you are setting yourself up for disappointment.
Mimi niko twitter since 2010, it has always been like that. Haijawahi badilika.Vurugu zipo, mizaha ilikuwepo, watu kutangaziana issue zao kupo, watu kutukanana au kuibiana wapenzi pia kupo n.k
Kabla ya hii watu kujiidentify as mabloo au wapwa, kulikuwa na side A na side Z. So huwa nashangaa mtu anapohisi kuwa twitter inatumika na watu wastaarabu au watu smart tu.
Tukija kwenye social media site ya Tz kama jamiiforums na yenyewe hivyo hivyo. Watu wanahisi kuwa zamani watu walikuwa wanashusha nondo tu muda wote, kutukanana pia kulikuwepo, kuzinguana, mizaha mizaha pia n.k