Wakuu,
Binafsi naona hizo Brand nilizotaja hapo zimefail kubadilisha majina na itachukua miaka mingi watu kuendelea kutumia old names yaani Twitter na Tigo instead of X or Yas.
Ni brand gani nyingine zimefail kubadilisha majina yake?
Yas wangeweka iwe Yas Pesa, angalau tungeweza kuwasamehe. Lakini kuweka tena mambo yao mengine mengine meusi yasiyoeleweka, hakika wameboronga si kidogo.
Hakuna hata iliyofeli, ni mazoea tu. Hata tigo zaman ilikuwa mobitel wakaipa jina la tigo ila watu waliendelea kuita mobitel, wakaanza kuzoea taratibu mpaka tigo. So, ni suala la muda mtu kuzoea brand.