Tx Moshi william daima tutakukumbuka

Tx Moshi william daima tutakukumbuka

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Hili lilikuwa jabali haswa la muziki! Uwezo wake wa kutunga ulikuwa wa kushangaza! Binafsi namkumbuka sana kwa muda wake alioishi na jinsi alivyotuburudisha! Mimi ni mpenzi wa R&B and hiphop lakini huyu nilikuwa namsikiliza sana
 
Mbona mtoto wake yupo kwan hakuburudish naye
 
toka kifo chake msondo nayo dizain km ishakufa!
Asilimia tisini ya nyimbo za msondo ndio alikuwa mtunzi! Alafu anastaili ya pekee kuimba hasa vibwagizo kama Tanzaniaaaaa!
 
Vichwa vya Msondo Ngoma Music Band ilikuwa ni balaa kabisa; Mzee Gurumo Mwenyewe, TX Moshi William, Seleman Mbwembwe, Joseph Maina bila kumsahau Athumani Momba. Mwenyezi Mungu aziweke roho zenu mahali pema Amen.

Wale watatu wa mwanzo yaani Gurumo, Moshi na Mbwembwe ndo huwezi choka wakati unasikiliza jinsi wanavyoimba. Dah kifo hiki jamani, ndo maana Dk Remmy aliimba kifo hakina huruma.
 
Penzi letu halikuanza zamani nae mwajabu,
nawala kamwe hatufanyi vishindo ooh mama
lakini tayari watu wameanza maneno yao
ndio maana mwanzo nilisema ulisikia
kwa kuwa tunapendana mengi utasikia lakini usijali
mimi sina wasiwasi bwana nimeyazoea
nimeishakuwa mtu mzima naelewa
penye penzi hapakosi tenzi wakale walisema
hauwezi kula mua bila kukuta fundo
Hapa moshi kule mbwembwe duh wanamuziki wameondoka wamebaki wachache na waimbaji wengiiii.
 
yule mtoto wa moshi anabebwa asife njaa mjini lakini kipaji hakuna pale
 
Penzi letu halikuanza zamani nae mwajabu,
nawala kamwe hatufanyi vishindo ooh mama
lakini tayari watu wameanza maneno yao
ndio maana mwanzo nilisema ulisikia
kwa kuwa tunapendana mengi utasikia lakini usijali
mimi sina wasiwasi bwana nimeyazoea
nimeishakuwa mtu mzima naelewa
penye penzi hapakosi tenzi wakale walisema
hauwezi kula mua bila kukuta fundo
Hapa moshi kule mbwembwe duh wanamuziki wameondoka wamebaki wachache na waimbaji wengiiii.

Katikati MAALIM GURUMO
Mbele ROMARIO
 
Slim5 wacha kabisa khabari hiyo tunakumbuka zamani.
 
Back
Top Bottom