Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Mary Mallon alizaliwa mwaka 1869 huko nchini Ireland. Mama yake akiwa na mimba yake alipatwa na ugonjwa wa Typhoid. Hili likamfanya Mary awe na maambukizi ya wadudu wa Typhoid ambao waliishi katika mfuko wa nyongo. Wadudu hawa hawakumsababishia ugonjwa wa typhoid ila aliweza kuambukiza wengine. Mtu wa hivi anaitwa asymptomatic carrier, yaani ana wadudu lakini haonyeshi dalili zozote za ugonjwa.
Baadaye Mary alipokuwa akahamia Marekani na kuanza kufanya kazi kama mpishi kwenye majumba ya matajiri. Kila nyumba aliyofanya kazi wenyeji walipatwa na typhoid kali. Hata baadhi wachache walipoteza maisha. Baada ya watu kufanya uchunguzi waligundua kuwa Mary ndiye anahusika na kusambaza typhoid kwa watu. Walipomface alikuwa mkali kama pilipili. Mwishowe akachukuliwa na kuwekwa quarantine ya watu wenye magonjwa ya kuambukiza. Walipomtoa bado akagoma kuacha kazi yake ya upishi, akaishia kuambikiza watu wengine. Mamlaka zikamuweka tena quarantine ya maisha hadi kifo chake mwaka 1938
Hadi anafariki hakuamini kwamba yeye ni carrier wa typhoid, na suala la kuitwa Typhoid Mary lilimuumiza sana.
Ukiona unapata typhoid mara kwa mara chunguza kwa makini sehemu unayokula na watu wanaoandaa chakula unachokula. Kuna carriers ambao wao wenyewe hawajawahi kuugua hata siku moja.