Tyson Fury amchapa Tom Schwarz kwa Knockout round ya 2

Muda ndio utasema kama ulivyosema kwa AJ..kama wataalamu wote walivyoshangazwa na kipigo kwa Aj ndivyo muda pia utakavyoamua kwa hao wengine.
Kuna miamba kwenye historia ya ndondi ilikaa na kukalishwa na vikaja visingizo kibao oooh sijui madawa ooh mara kanywa maji.Unaendaje na matokeo kabisa wakati unayepigana naye ana hamu ya kushinda na kuweka Historia?
 
mike tyson alidundwa na "bums" douglas buster jr, lenox lewis alidundwa na "bums" rahman hashim
 

Sikubaliani na hilo. Kama ni hivyo basi hata maradona na pele ni bora zaidi ya Messi, kwakuwa wa zamani sio?😁😁
 
Wataalamu karibu wote wa masuala ya ngumi walishangazwa na matokeo ya pambano la AJ na Ruiz, maana kabla ya pambano karibu kila mtu alikuwa anajua AJ anashinda tena mapema tu kutokana na rekodi yake, so ni wazi ushindi wa Ruiz uliwashangaza wengi.

Acha uongo, ni wewe tu ulishangazwa kushindwa kwa AJ lakini usiwajumuishe wote. Ukienda kwenye record Destroyer pia mbaya lakini ukamdharau kwa sababu kibonge eti 😁😁


Boxing record
Total fights34
Wins33
Wins by KO22
Losses1
 
Acha uongo, ni wewe tu ulishangazwa kushindwa kwa AJ lakini usiwajumuishe wote. Ukienda kwenye record Destroyer pia mbaya lakini ukamdharau kwa sababu kibonge eti [emoji16][emoji16]


Boxing record
Total fights34
Wins33
Wins by KO22
Losses1
Kwenye Ranking za BOXREC alikuwa no16 kabla hajapigana na AJ, huku AJ akiwa no1. Kama kwako wewe no16 kumpiga no1 si habari ya kushangaza inabidi tukupeleke Milembe. Halafu kwenye Boxing hawaangalii tu umeshinda marangapi, wanaangalia je umepigana na kina nani? Kabla Ruiz hajapigana na AJ pambano lake credible lilikuwa moja tu dhidi ya Joseph Parker ambapo alipoteza, wengine aliopigana nao hakuna aliuekuwa top 10. Kwa sasa amepata ratings za juu sana kwavile amempiga bingwa
 
Matokeo ya kuchaguachagua ndo unajikuta unapigwa na mtu ambaye hukumtegemea, AJ hakutegemea kama anaweza kupigwa na Ruiz, alijua ni njia tu ya kuiboresha rekodi yake
 
mike tyson alidundwa na "bums" douglas buster jr, lenox lewis alidundwa na "bums" rahman hashim
Lennox aliwadunda wote waliompiga kwenye Rematch, sijui kama AJ ataweza kufanya hivyo kwa Ruiz
 
Lennox aliwadunda wote waliopiga kwenye Rematch, sijui kama AJ ataweza kufanya hivyo kwa Ruiz
Kuna watu bado wanamjaza kichwa AJ.hiyo rematch Ruiz atamkalisha kama kawa na heshima itarudi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…