Tyson Fury amchapa Tom Schwarz kwa Knockout round ya 2

Tyson Fury amchapa Tom Schwarz kwa Knockout round ya 2

Acha mihemko ndugu, ulikuwa wapi kumnadi hivi Ruiz kabla ya pambano la AJ? Pengine hata ulikuwa humjui[emoji3][emoji3], nimeanzisha thread kibao za Ngumi kabla ya mapambano sijakuona hata moja, baada ya matokeo ndo unaonekana halafu unajifanya unawajua sana[emoji2][emoji2][emoji2]. Wataalamu karibu wote wa masuala ya ngumi walishangazwa na matokeo ya pambano la AJ na Ruiz, maana kabla ya pambano karibu kila mtu alikuwa anajua AJ anashinda tena mapema tu kutokana na rekodi yake, so ni wazi ushindi wa Ruiz uliwashangaza wengi na kuwekwa kati ya one of the biggest upset of all time kwenye boxing, sasa cha ajabu mwenzangu na mimi unajifanya eti hukushangazwa na Ruiz kushinda, nyie ndo wachambuzi wa bongo mnaochambua baada ya matokeo[emoji1787][emoji1787]. Kuhusu Ruiz kumpiga Wilder or Fury kwa mtazamo wangu naona ni ngumu sana, kwa Wilder ili umpige inabidi uwe mtaalamu sana wa kukwepa ngumi (head movement ya ajabu), maana ile right hand ikikupata ni goodnight, je Ruiz ana uwezo wa kukwepa ngumi kama FURY?Jibu ni hapana. Na kwa upande wa Fury huyu ni mgumu zaidi kumpiga kutokana na style yake, anamove sana so Ruiz hatakuwa na nafasi sana ya kupiga ngumi kama alivyofanya kwa AJ, na hata akifanikiwa kumpiga ngumi chache hazitaweza kummaliza, kama Fury aliweza kuamka baada ya kudondoshwa na Bronzebomber 2 times je Ruiz ana kipi cha ziada?
Muda ndio utasema kama ulivyosema kwa AJ..kama wataalamu wote walivyoshangazwa na kipigo kwa Aj ndivyo muda pia utakavyoamua kwa hao wengine.
Kuna miamba kwenye historia ya ndondi ilikaa na kukalishwa na vikaja visingizo kibao oooh sijui madawa ooh mara kanywa maji.Unaendaje na matokeo kabisa wakati unayepigana naye ana hamu ya kushinda na kuweka Historia?
 
Tofauti kubwa nnayoona wa sasa wako kimaslahi sana na kuogopa kupoteza mikanda yao wanayoshikilia. Wanachagua chagua wapigane na "bums" "bums" kulinda heshima. Wakati mashabiki kuna mechi wangependa sana kuziona. Ila eventually watapigana tu pamoja na dana dana zao
mike tyson alidundwa na "bums" douglas buster jr, lenox lewis alidundwa na "bums" rahman hashim
 
Sikubaliani na hilo. Kama ni hivyo basi hata maradona na pele ni bora zaidi ya Messi, kwakuwa wa zamani sio?😁😁
 
Wataalamu karibu wote wa masuala ya ngumi walishangazwa na matokeo ya pambano la AJ na Ruiz, maana kabla ya pambano karibu kila mtu alikuwa anajua AJ anashinda tena mapema tu kutokana na rekodi yake, so ni wazi ushindi wa Ruiz uliwashangaza wengi.

Acha uongo, ni wewe tu ulishangazwa kushindwa kwa AJ lakini usiwajumuishe wote. Ukienda kwenye record Destroyer pia mbaya lakini ukamdharau kwa sababu kibonge eti 😁😁

Boxing record
Total fights34
Wins33
Wins by KO22
Losses1
 
Acha uongo, ni wewe tu ulishangazwa kushindwa kwa AJ lakini usiwajumuishe wote. Ukienda kwenye record Destroyer pia mbaya lakini ukamdharau kwa sababu kibonge eti [emoji16][emoji16]

Boxing record
Total fights34
Wins33
Wins by KO22
Losses1
Kwenye Ranking za BOXREC alikuwa no16 kabla hajapigana na AJ, huku AJ akiwa no1. Kama kwako wewe no16 kumpiga no1 si habari ya kushangaza inabidi tukupeleke Milembe. Halafu kwenye Boxing hawaangalii tu umeshinda marangapi, wanaangalia je umepigana na kina nani? Kabla Ruiz hajapigana na AJ pambano lake credible lilikuwa moja tu dhidi ya Joseph Parker ambapo alipoteza, wengine aliopigana nao hakuna aliuekuwa top 10. Kwa sasa amepata ratings za juu sana kwavile amempiga bingwa
 
Tofauti kubwa nnayoona wa sasa wako kimaslahi sana na kuogopa kupoteza mikanda yao wanayoshikilia. Wanachagua chagua wapigane na "bums" "bums" kulinda heshima. Wakati mashabiki kuna mechi wangependa sana kuziona. Ila eventually watapigana tu pamoja na dana dana zao
Matokeo ya kuchaguachagua ndo unajikuta unapigwa na mtu ambaye hukumtegemea, AJ hakutegemea kama anaweza kupigwa na Ruiz, alijua ni njia tu ya kuiboresha rekodi yake
 
mike tyson alidundwa na "bums" douglas buster jr, lenox lewis alidundwa na "bums" rahman hashim
Lennox aliwadunda wote waliompiga kwenye Rematch, sijui kama AJ ataweza kufanya hivyo kwa Ruiz
 
Back
Top Bottom