Habari wanajamvi,
Hapo nyuma, niliuliza swali.
Hili hapa:
View attachment 2135040
Leo asubuhi nilipata email kutoka Dudumizi, kuwa reservation zimeanza. Nilipiga simu DuHosting, wakaelezea yafuatayo:
- Sasa hivi wanafanya reservation, kama ulisharegister jina lolote lenye format ya .xx.tz (iwe .co.tz, .ac.tz etc). Reservation inafanywa between sasa na July 2022. Opoortunity ya kwanza inatolewa kwa wale ambao wana domain tayari, na majina lazima yamatch (kama ilikuwa samedi.co.tz, utaweza kuregister samedi.tz)
- Next in line ni wale wenye trademark. Kama uliregister BRELA, unaweza kuclaim .tz domain hata kama ulikuwa hujaregister awali.
- Mwisho itawekwa open kwa raia baada ya mwezi wa saba.
Kuna majina ambayo yamekuwa reserved na TCRA, kwa mfano majina ya mikoa, majina maarufu etc.
Binafsi nina furaha kuu kwa kuwa hatimaye tuna hii fursa.