Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 5,319
- 10,416
Mtafaruku,
Mkuu yote haya yanafahamika... Lakini ukweli bado umebakia kuwa Mugabe kama rais ni lazima ajikate... Nilitegemea hizo digree zake zingweza kuona mbali zaidi ktk hili. Mugabe ni MBINAFSI na true reflection of NDIVYO TULIVYO..
Swala la Uingereza linajulikana sana na binafsi huyo Morgan sina kabisa aibu ya kusema hafai ni kibaraka kama kina Karzai, Musharaf, na mtu kama Hosni Mubarak wa Egypt ambaye yupo madarakani kabla hata Zimbabwe haijapata Uhuru...Nani kisha mnyooshea kidole huyo?... hakuna!
Lakini pamoja na yote haya Zimbabwe inastahili kupata mtu mwingine kuwakosha Uingereza kama walivyofanya China....
Ilikuwa zuga kuondoa Utawala wa Mao Tse Tung lakini libeneke bado Wachina wanaliendeleza chini ya utawala wa chama kile kile tena basi sasa hivi ndio wanashinda vita ya kiuchumi...
Mugabe anatakiwa kufikiria nje ya Box mkuu bado anaweza kuwa na nafasi yake ya juu ndani ya chama lakini aondoke mbele ya jukwaa....Anakipaka!
Mkandara at long last you are coming head on in this Mugabe saga. All along thats what we have said, Ingawa imekuchukua mda kuuoana uzandiki wa Mugabe. imperfect as it may be Mugabe aondoke..Zimbabwe pale ilipo haimuhitaji. Yes, ukibaraka ndo unatuua waafrika, lakini unposema Mogani humtaki ni kibaraka...sasa nani asiyekibaraka unayemtaka? Tell me Africa kiongozi gani si kibaraka?
Leo Sinclair anakwambia ameiona report ya madini hata sisi walipa kodi na wapiga kura hatujaambiwa chochote..but th man saw na alikuwa ameshamwelekeza mkuu wa kaya cha kufanya! Ndugu yangu tuhangaike na tunavyoviweza tutetee maisha ya waafrika wenzetu..lakini tukianza ku-finger point nani anafaa nani hafai, nani kibaraka nani si kibaraka...hatufiki popote.
Mugabe mwenyewe alikuwa kibaraka, its because the mission has gone sour, that he is turning! This is Africa. Kinachoniuma mimi..ni hawa raia wanaouliwa wakati waafrika tuko kimya tukiwasingizia wazungu..surely,, Bush has nothing to do with the death of these people!