Godwine na Mdondoaji nawashukuru kwa kufanya ufafanuzi mzuri tu kuhusu hali halisi ya thamani ya Tsh. Upande mwingine si vibaya kuangalia nini kifanyike ili kuzuia "fluctuation" ya shilingi dhidi ya dola.
1. Kwanza naomba niseme kuwa kushuka kwa thamani ya pesa si lazima kiwe kitu kibaya; kabla hujanishambulia katika hili, naomba nieleze kwa nini nasema vile..... Thamani ya pesa ikishuka, ni fursa kubwa kwa uchumi (nchi) husika kuongeza exports kwa maana bidhaa zake zitakuwa na bei nzuri katika zoko la dunia ukilinganisha na nchi ambazo pesa yake ina thanani kubwa. Hii ndio maana umesikia Japan juzi inaangaika na tatizo la thamani uya ya pesa yake kupanda maana exports zao zinakuwa "hazilipi" nje ya japan. Katika hili, nashuri Serikali itengeneze Mazingira yatakayowawezesha watanzania kutengeneza na kuuza vitu kwa wingi. Hivyo tatizo sio thamani ya pesa kuwa ndogo, bali tatizo ni thamani ya pesa kucheza sana kiasi kwamba utabiri (projection) kwa biashara kubwa unakuwa mgumu. Kwa ujumla la muhimu ni kuhakikisha thamani ya pesa inabaki pale pale isipande na wala isishuke.
2. Kuhusu suala la treasury bills, hili sidhani kama serikali ina uamuzi juu ya bei. Vigezo vya bei vinazingatia "demand and supply factors". Hii inaathiriwa na vigezo vya nje ya serikali ikitegemea na credit rating ya nchi. Kwa hili ninamaanisha kuwa watu wananunua treasury bills ikitegemea na wao kama wanaona zinalipa kuwa nazo kutokana na uwezekano wa uchumi wa nchi kuwa mzuri siku za usoni na hivyo kuweza kuziuza kwa bei nzuri zaidi. Ndo maana ulisikia wamarekani juzi wanatafuta kummeza mtu mzima mzima kuhusiana na sera na maamuzi yatakayoiongoza nchi miaka 10 ijayo na jinsi yatatakavyopokelewa na ulimwengu wa wafanyabiashara na wawekezaji duniani.
3.Serikali iweke mikakati itakayowawezesha watanzania kutengeneza bidhaa zinazoendana na viwango bora vya kisasa na kuuzika kwenye soko la dunia. Nimeanza kusikia kucheza kwa bei za bidhaa za TZ kama zile za kilimo kwenye soko la dunia Tangu nimezaliwa. Pamoja na hayo sijaona kama kuna mipangilio ya kudumu ya kuhakikisha kuwa kweli bidhaa zetu zinakuwa bora. Kuna mgongano wa sera na hatuna "special focus area". Ninapoongelea bidhaa hapa naomba ifahamike kuwa hata huduma (services) zinatakiwa kuzingatiwa. Mfano ulio hai, hivi karibuni tumeona makampuni ya simu yanauza (outsourcing) kazi za ufundi kwa makampuni mengine. wanaotumika humo ni watanzania na pesa zinarudi hukooooo majuu. Sina hakika kama serikali inaona opportunity ya kuhakikisha watanzania wanakamata fursa kamakuwawezesha watanzania wakamate fursa hizo ili pesa za kigeni zibaki humu humu. Mfano wa hili, Rwanda sasa hivi inajiandaa kuwa HUB ya IT services na tayari imeanza kuandaa mazingira - mkongo wa mawasiliano uifikie kila primary school. Wakati huo huo, kwa TZ ukiachulia mbali na watoto wa mkulima kuiona komputa kwenye chaki na kuambiwa "rangi ya screen ikiwa ON na OFF inafananaje" kama ilivyo kwenye Tanganzo la Haki elimu.
..... makala itaendelea ili kuwapa wasomaji kumeza mate.