Tz shilling gained strength today

nashangaa pale mlimani city kuna maduka yanauza bidhaa kwa dola! Kila nikipita kwenye lile duka karibia na shoprite huwa napandwa hasira!

kuna mama wa kichina kama sio mkorea anauza nguo pale

nilingia nikamwuliza wauza shilingi ngapi?

akanambia dola kadhaa, nikachapa mwendo
 

Mkuu,

Sikupingi kuwa pesa zipo nyingi katika mzunguko wa fedha zimechangia kuyumba kwa thamani ya shillingi but sio sababu pekee ya kuyumba kwa sarafu ya nchi. Hapa ndip napokupinga. Unapozungumzia pesa nyingi wachumi wanaweza kupunguza mzunguko huo na kudhibiti mfumuko wa bei (inflation). Kwa kutumia monetary approach na fishers principle wanaweza kupandisha interest rate on deposits, and loans kuencourage watu wasave pesa zaidi kulikoni kutumbua maisha. Vile vile kudhibiti mikopo kunasaidia makampuni kuwa na limitation ya matumizi yao ya pesa. Isitoshe serikali inaweza kuingiza vitu kama lottery kusaidia kupunguza amount ya pesa katika mzunguko.

Ila unaposema makampuni yalibadilisha pesa na hivyo kusababisha pesa ya shillingi thamani yake kushuka hilo tunaweza kusema ni jambo la muda mfupi (kwasababu ya uhaba wa mafuta) au kipindi kile cha uchaguzi tumeona sarafu ikishuka thamani. Hata hivyo huwezi kukataa policy za nchi hii pia zinachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa thamani ya sarafu nchini. Mfano kampuni za madini nchini huchukua madini na kwenda kuyauza nchi za nje. Kampuni inahodhi balance sheet in foreign currencies je huoni kwamba hizi kampuni za madini zikiwa zinasimamiwa ziwe zinaweka rekodi zake in Tshs na kuhodhi pesa katika benki zetu kutasaidia kupandisha thamani ya sarafu nchini????

Pia kampuni za real estate, shule kama St. whatever, na shule nyingi za mjini Dar wanachaji fees zao in US dollar wakati zipo tanzania. Unategemea dollar demand itashuka??? Mpaka nguo ukienda baadhi ya maduka unauziwa in US dollar utafikiri tupo USA wakati tuko Tanzania this is dangerous kwani malengo makuu ya kuwepo sarafu ni kwamba itumike kama chombo cha kubadishia thamani. Ikiwa kama hatuthamini sarafu yetu tusitegemee hata siku moja itakuja kuwa thamani nchini.

Vile vile sarafu ya Tanzania iko pegged na US dollar baada ya recommendation za World Bank na IMF zilizosababisha tukauza reserves zetu za gold in favour of US dollar. Kutokana ya hilo US dollar ikiwa haina thamani na sisi thamani ya shillingi inashuka thamani. Ikipanda thamani na shillingi yetu inaimarika. Kwa kuthibitisha hayo angalia trend ya kuanguka shillingi kuanzia January hadi May au April utatambua imeshuka kipindi dollar inashuka na kuimarika inapoimarika US dollar.

Ingelikuwa Central Bank wamezidiwa na mzunguko wa pesa wangeliweza kudhibiti ila tatizo la sarafu liko kwenye fiscal policy za nchi hii. Bila kuwapo na fiscal policy imara ni kazi bure na thamani ya shillingi itaendelea kuporomoka.
 
Godwine na Mdondoaji nawashukuru kwa kufanya ufafanuzi mzuri tu kuhusu hali halisi ya thamani ya Tsh. Upande mwingine si vibaya kuangalia nini kifanyike ili kuzuia "fluctuation" ya shilingi dhidi ya dola.
1. Kwanza naomba niseme kuwa kushuka kwa thamani ya pesa si lazima kiwe kitu kibaya; kabla hujanishambulia katika hili, naomba nieleze kwa nini nasema vile..... Thamani ya pesa ikishuka, ni fursa kubwa kwa uchumi (nchi) husika kuongeza exports kwa maana bidhaa zake zitakuwa na bei nzuri katika zoko la dunia ukilinganisha na nchi ambazo pesa yake ina thanani kubwa. Hii ndio maana umesikia Japan juzi inaangaika na tatizo la thamani uya ya pesa yake kupanda maana exports zao zinakuwa "hazilipi" nje ya japan. Katika hili, nashuri Serikali itengeneze Mazingira yatakayowawezesha watanzania kutengeneza na kuuza vitu kwa wingi. Hivyo tatizo sio thamani ya pesa kuwa ndogo, bali tatizo ni thamani ya pesa kucheza sana kiasi kwamba utabiri (projection) kwa biashara kubwa unakuwa mgumu. Kwa ujumla la muhimu ni kuhakikisha thamani ya pesa inabaki pale pale isipande na wala isishuke.
2. Kuhusu suala la treasury bills, hili sidhani kama serikali ina uamuzi juu ya bei. Vigezo vya bei vinazingatia "demand and supply factors". Hii inaathiriwa na vigezo vya nje ya serikali ikitegemea na credit rating ya nchi. Kwa hili ninamaanisha kuwa watu wananunua treasury bills ikitegemea na wao kama wanaona zinalipa kuwa nazo kutokana na uwezekano wa uchumi wa nchi kuwa mzuri siku za usoni na hivyo kuweza kuziuza kwa bei nzuri zaidi. Ndo maana ulisikia wamarekani juzi wanatafuta kummeza mtu mzima mzima kuhusiana na sera na maamuzi yatakayoiongoza nchi miaka 10 ijayo na jinsi yatatakavyopokelewa na ulimwengu wa wafanyabiashara na wawekezaji duniani.
3.Serikali iweke mikakati itakayowawezesha watanzania kutengeneza bidhaa zinazoendana na viwango bora vya kisasa na kuuzika kwenye soko la dunia. Nimeanza kusikia kucheza kwa bei za bidhaa za TZ kama zile za kilimo kwenye soko la dunia Tangu nimezaliwa. Pamoja na hayo sijaona kama kuna mipangilio ya kudumu ya kuhakikisha kuwa kweli bidhaa zetu zinakuwa bora. Kuna mgongano wa sera na hatuna "special focus area". Ninapoongelea bidhaa hapa naomba ifahamike kuwa hata huduma (services) zinatakiwa kuzingatiwa. Mfano ulio hai, hivi karibuni tumeona makampuni ya simu yanauza (outsourcing) kazi za ufundi kwa makampuni mengine. wanaotumika humo ni watanzania na pesa zinarudi hukooooo majuu. Sina hakika kama serikali inaona opportunity ya kuhakikisha watanzania wanakamata fursa kamakuwawezesha watanzania wakamate fursa hizo ili pesa za kigeni zibaki humu humu. Mfano wa hili, Rwanda sasa hivi inajiandaa kuwa HUB ya IT services na tayari imeanza kuandaa mazingira - mkongo wa mawasiliano uifikie kila primary school. Wakati huo huo, kwa TZ ukiachulia mbali na watoto wa mkulima kuiona komputa kwenye chaki na kuambiwa "rangi ya screen ikiwa ON na OFF inafananaje" kama ilivyo kwenye Tanganzo la Haki elimu.

..... makala itaendelea ili kuwapa wasomaji kumeza mate.
 
 

Mutensa,

Kwanza Tanzania uchumi haujawa mkubwa kufikia kiwango cha kuweza kuwa determine by market instruments (demand and supply) . Uchumi wa Tanzania uko stagnant when it comes to capital market. Hadi tutakapokuwa tumeshaubadilisha mfumo wa mitaji ndio unaweza kusema haya unayozungumzia. We are still using a control capital market na ndio maana nasema tena BOT hawashindwi kuzuia mzunguko wa fedha unapokuwa mkubwa. Benki kuu wana monetary instruments kama tbills, bonds, reserve ratio ambazo wanaweza kuzitumia kupunguza kiwango cha fedha katika uchumi. Mfano kwa kutumia reserve ratio wanaweza kuongeza kiwango cha kubakia katika account za mabenki ya biashara ili kupunguza uwezo wa benki kukopesha katika soko. Vile vile wakiongeza interest benki nyingi zitavutiwa kukopesha serikali ili kupunguza kiwango cha pesa available katika masoko ya fedha.

Hata hivyo huweza kutumia hizi monetary instrument bila kuwapo kwa strong fiscal policy ya nchi. Mfano kwanini hadi sasa hatukusanyi dhahabu wakati bei ya dhahabu hadi jana katika masoko ya vito (commodities market) ilikuwa $1877 per uzito. Serikali bado inawauzia wachimbaji dhahabu $400 per uzito kitu kinachohuzunisha. Tunawauzia dhahabu kwa bei ya ubwete wao wanaenda kuiuza dhahabu kwa bei ya juu na kupata faida maradufu. Watasema wawekezaji wanatumia gharama kubwa ila wasisahau dhahabu inachimba kwenye ardhi ya tanzania na dhahabu ikondoka haurudi yanabakia mashimo je is it worth the sacrifice? Kama ndio tushaingia mikataba hiyo tunaweza kujaribu kutumia njia nyengine kurudisha tofauti ya $1877 na $400 for example tukiweka superprofit tax (kama Australia na nchi za south america wanavyofanya) tax hii inaweza kufidia tofauti ya bei ya soko na bei ya kununulia. Kama hawataki waondoke na itakuwa nafuu kwetu, we may have another investor who will be willing to comply with the tax. Kuongezeka kwa mapato kutanyanyua thamani ya sarafu ya nchi.

Vile vile kukusanya dhahabu ya reserve ya nchi pia kunaweza kuisaidia nchi kuiuza kwa nchi za nje kwa bei ya soko na hivyo kusaidia kukuza thamani ya sarafu. Sasa hivi tuna $1.7 Billion kama reserves ambazo kuna hatari ya thamani ya US dollar kuwa devalued in the future na kupelekea tukapoteza mamilioni ya shillingi. Serikali ianze kukusanya dhahabu kuokoa Tshs isianguke it is a shame we are a third country in Africa in gold production following Ghana and South Africa lakini sarafu yetu iko mbali na wenzetu mabadiliko ni muhimu kuipeleka nchi mbele venginevyo tutakuja kujutia. Kuwepo na mikakati ya kukusanya dhahabu kwa wachimbaji wa kati na wadogo wadogo kuweza kuwanyanyua wachimbaji hawa na kuinyanyua thamani ya dhahabu.

Pia fiscal policy iangalie utaratibu wa dollarisation na matumizi yake nchini. Nimeenda nchi kama China inabidi ununue Renimbi ili uweze kufanya biashara. Nimekwenda Singapore hali ndio hiyo. Nimekwenda Australia the same hizi nchi zote inabidi ubadilishe hela yako kuweza kufanya transactions. Na angalia thamani ya sarafu ya nchi hizi Renimbi is devalue intentionally by China ili kuboost exports nchini mwao but it is worth more than the current value. Singapore Dollar is almost at par with USD. Australian Dollar is also at par with the dollar. Nchi zote hizi ukienda kuna maduka maalum unaweza kufanya biashara kwa kutumia US dollar but the rest inabidi uwe na local currencies. Tanzania unaweza kwenda into a local duka kununua shati tu ukaambiwa bei yake in US dollar this is an absurd!!!! The government needs to tackle dollarisation otherwise thamani ya shillingi itaporomoka tu.

Pia serikali iweke policy kwa makampuni ya kigeni kufanya transactions zao in Tshs and not US dollar au fedha nyengine yeyote ya kigeni. Hilo linaweza kusaidia kuongeza thamani ya sarafu nchini.

Unachokipendekeza ni long term solution kunyanyua sekta ya kilimo na viwanda. Hilo ni kwasababu sekta hizi zinategemeana na kwa hali iliyopo sasa kama ukame unaosababishwa na kupotea kwa mvua, kukosekana kwa umeme wa uhakika. Vikiwa vimetengamaa na tukaweza kuirekebisha na kuisimamia infrastructure nchini unaweza kupendekeza vitu hivyo ila kwasasa short term and emergency measures are needed kuikoa sarafu otherwise bila ya kuwa na short term solutions hata long term solutions hazitakuwa na maana.
 


Hili la viwanda nimeshalisema siku nyingi katika baadhi ya post na nikasema bila ya viwanda hatuwezi kuendelea kwasababu Viwanda vinatengeneza ajira, vinalipa kodi na vinasaidia kuongeza pato la nchi. Kwa sasa nafagilia Kilimo kwani sasa hivi kinalipa hasa kwa vile nchi yetu ina bahati ya rutuba binafsi na ulimwenguni sasa hivi kuna uhaba mkubwa wa chakula na maeneo ya kuzalisha chakula hivyo ninaungana na mtazamo wa serikali kukaribisha wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi kutusaidia kufanya large scale agriculture. Hilo litaweza kunyanyua pato la nchi . Kikwazo cha hilo ni upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini yaani umeme kwani bila ya hilo si Viwanda wala kilimo cha large scale vinaweza kufanikiwa. Binafsi naona Waziri Ngeleja should be sacked kwani ameshindwa na sidhani mpango wake utaweza kusaidia kutatua tatizo la nishati. But who knows time will tell!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…