tumia www.autorec.co.jp ni wa ukweli, customercare safi kabisa wewe tu.
Tradecareview sio Kampuni ya kuuza magari bali ni mtandao unatumiwa na makampuni kutangaza magari yanayouzwa. Mimi na Jamaa zangu wa karibu wawili tumeagiza na tumetumepata magari yetu. Hakikisha kuwa hautumi pesa kwenye Kampuni moja kwa moja, tumia PAY TRADE, gari utalipata. Kama utatuma pesa moja kwa moja kuna uwezekano wa kuingia kwenye mikono ya matapeli.
Nashukuru sana, mkuu! I wanted to hear ushuhuda kama huo, especially hiyo part ua Pay trade!
Mimi nimeagiza mara 3 na hawa jamaa tena bila hiyo pay trade! cha muhimu ni kuwasiliana na kampuni husika na uliza hao tradecarview watakupa list ya makampuni waliyoyafungia kwa utapeli.
Na mimi nina swali,
Je hizo document za kupokelea gari wanakutumia kwa njia gani? je naweza kulipia huku nilipo na nikatumiwa document huku nilipo? mimi niko nchi jirani huku, ila nataka gari nilisajilie TZ ili mke wangu atumie?
Ukisha chagua gari watakupatia maelekezo yote, watakutumia profoma invoice, pesa utatuma kwa Telegraphic Transfer (T/T) via you bank, watakutmia confirmation mara watakapopokea pesa, gari likiondoka kwa Meli wanakutumia documents na zinakufikia within one week, ukipata document unalipia TIN unakabidhi kwa Clearing Agent wako, then unasubiri kuletewa gari nyumbani.