Sokaattorneys
New Member
- Jul 13, 2022
- 1
- 0
Ualbino sio ulemavu bali ni kundi lenye mahitaji maalumu.
Maana ya ualbino. Ni hali ya upungufu wa chembe chembe za rangi ya ngozi, nywele, na hata macho. Upungufu huo husababisha mtu au mnyama kuwa na ngozi nyeupe au macho yasiyo kuwa na rangi.
Ulemavu. Ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo za kawaidaa katika maisha ya jamii bila ya kuwa na msaada wa chombo au mtu katika utekelezaji wa shughuli hizo. Zipo aina nyingi za ulemavu baadhi ni kama zinavotajwa hapa chini
(a) Ulemavu wa kimwili
(b) Ulemavu wa akili
(c) Ulemavu wa milango ya fahamu.
mchanganuo huo hapo juu unajieleza wazi kwa kuzingatia maana ya ulemavu na ualbino hakuna ulinganifu wowote wakuthibitisha ya kwamba ualbino ni ulemavu na hii inatupeleka kwenye mada kuu kama ilivyo wasilishwa na mwandishi kuwa ualbino sio ulemavu bali ni kundi la watu wenye mahitaji maalumu.
Ili mada kuu iweze kueleweka mwandishi amaeona ni vyema kuelezea hoja hii ndogo ya kundi la watu wenye mahitaji maalumu kwa kina
Kundi la watu wenye mahitaji maalumu. Hili ni kundi ambalo huwa na mahitaji binafsi ukiachana na mahitaji ya muhimu ambayo binadamu hupaswa kuyapata, mfano binadamu anapaswa kupata mahitaji maalumu kama chakula, malazi, mavazi na afya bora. Linapotokea hitaji kama vile mtu fulani anatatizo lakuona mbali analzimika kuvaa miwani au mtu fulani anapotembea katika jua kali ngozI yake huaribika hivi inampasa kuwa na hitaji la kuvaa nguo zinazozuia jua au kupaka mafuta maalumu ya kupunguza ukali wajua ili usiharibu ngozi yake hilo ni hitaji maalumu na si ulemavu. Yafuatyo ni baadhi ya makundi yenye mahitaji maalumu na sio ulemavu
(a) Ualbino
(b) Wazee
(c) Watoto walio zaliwa njiti
(d) Wanawake
(c) Watoto kwa ujumla
Baada ya kuangazia kwa undani kuhusu kundi la watu wenye mahitaji maalumu sass mwandishi anjikita kwenye hoja kuu ya kwamba ualbino sio ulemavu bali ni kundi la watu wenye mahitaji maalumu kwa hoja zifuatazo.
(1) Hakuna ushahidi wa kisayansi unao thibitisha kuwa ualbino ni ulemavu. Sayansi ya mwili wabinadamu na wanasayansi wabobezi wa ulemavu kwa viumbe hai na visivyo hai hawajathibitisha kuwa ualbino ni ulemavu bali wanasayansi wengi waliofanya uchunguzi kuhusu ualbino wanalandana katika hoja zao kwamba ualbino ni hali ya upungufu wa chembe chembe za rangi ya ngozi, nywele na hata macho, hawaelezi kwamba ualbino ni ulemavu bali hoja zao zinajikita katika kuzungumzia upungufu wa rangi ya ngozi kwa binadamu na wanyama pia.
(2) Imani potofu. Imani isiyo thabiti ndio inaongoza katika vugu vugu la kulazimisha ualbino kuonekana kama ni ulemavu kuna baadhi ya makabila hapa nchini tanzania yanaamini kwamba mtoto anapozaliwa na upungufu huo wa rangi ya ngozi ni ulemavu na ni nuksi kwenye familia hivo hapaswi kuishi, kama binadamu wengine kwa imani kuwa ni mlemavu, Imani hizi ni za kupigwa vita kwa kuwa sio imani sahihi na zinakwenda kinyume na haki za binadamu pia katiba ya nchi ambayo inapinga ubaguzi wa aina yeyote.
(3) Tatizo la elimu. Tatizo la elimu kwa jamii kuhusu ualbino hili ndilo janga kubwa ambalo limepelekea mwandishi kuandika kuhusu mada kuu, elimu huweza kumpatia mtu maarifa pia msimamo wa kifikra jamii ya wasio na elimu kuhusu ualbino bado wanaamini kuwa ualbino ni ulemavu wa ngozi, na sio upungufu wa chembe chembe za rangi ya ngozi, nywele au macho. Kundi hilo bado lina amini ualbino ni ulemavu wangozi hoja hii haina mashiko kisayansi hata haina ushahidi kwenye kuthibitisha imani ambayo mwandishi anaiweka katika kundi la imani potofu.
(4) Hoja ya ualbino ni ulemavu ipo katika baadhi ya nchi za Afrika na sio ulimwengu mzima. Ukitembelea mataifa ambayo yanapatikana nje ya bara la Afrika na baadhi ya nchi chache za kiafrika hawatambui ualbino kama ulemavu bali kama kundi lenye mahitaji maalumu.
Mwandishi kwa Kutumia hoja chache na kwa ufupi ameweza kuelezea hoja kuu ya kwamba ualbino sio ulemavu bali ni kundi la watu wenye mahitaji maalumu.
Mwandishi pia anatoa ushauri nini kifanyike kubadilisha taswira ya wengi wanao amini kuwa ualbino ni ulemavu na kuwabagua baadhi ya watu wenye ualbino na kuwanyima fursa mbali mbali inayopelekea kuathiri saikolojiaya kundi la watu wenye ualbino, uchumi wa mtu na taifa kiujumla , mwandishi anashauri haya yafanyike.
(1) Elimu kwa jamii kuhusu ualbino ikifanywa na serekali kupitia ngazi mbali mbali za kielimu hapa nchini, pia semina mbali mbali zifanyike kea umma ilu kubadili taswira ambayo mwandishi anaitaja kama imani potofu
(2) Kutoa ajira na fursa sawa kwa watu wenye aulbino. Ajira zisibague huyu ni albino basi hawezi kuajiriwa kama dereva, au huyu ni albino hawezi kuwa mkurugenzi. Hili linapaswa kutekelezwa na watu binafsi, taasisi na serekali kwa ujumla
Mwandishi anawasilisha na anaruhusu ukosolewaji wakujenga na si kubomoa, chuki au audui