Ualimu umenichosha

Ualimu umenichosha

mnyongeni

Senior Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
141
Reaction score
24
Habari wana jf, labda nitoe tu historia kwa ufupi... mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu mwaka juzi (2011),na kada niliyoisomea ni ya ualimu. ( kwa sasa ni mwalimu), mnamo mwaka 2008 nilipomaliza form six, nilipo omba vyuo nilipata kuchaguliwa vyuo viwili yaani kozi ya ualimu na mass communication.na nilichaguliwa elimu kwani aliyekuwa ananielekeza kujaza form aliniambia niweke education kama first choice, sikuwa na jinsi kwani uelewa ulikuwa ni mdogo wa nini nifuate...... Malengo yangu yalikuwa natamani sana kusomea video shooting and editing (kwani nilitamani sana kuwa mtengeneza movie na music video). ila nilijikuta nakosa elimu ya maelekezo ya ni jinsi gani nitaweza kufikia ndoto yangu., Nilipo washirikisha wazazi walikataa kata kata mimi kusoma mass communication kwani waliponda sana wakisema uandishi wa habari hauna dili ( sana sana baba, kwani yeye by that time alikuwa ni afisa elimu vifaa na takwimu (SLO)) sikuwa na jinsi kwani nilipoendelea kubisha baba alitaka kunizira kuwa nilienda mass communication nikikwama nisimuhusishe kwani aliamini naweza kosa mkopo, na education mkopo ulikuwa ni wa kufikia. siyo siri nilienda chuo kishingo upande, mwaka wa kwanza karibia wote nilikuwa ni wa kulalamika tu, second year nikaaza kurecover. nikamaliza 2011, mwaka 2012, nikaajiriwa wilaya moja hapa tz, kama walimu wa o level kwenye shule moja ya kata. kiukweli nafundisha ndiyo ila moyo wangu na mapenzi hayako kwenye ualimu kabisa.... pia maslahi madogo... mshahara wenyewe full makato, na ukipata mshahara inabidi usubiri mpaka mwisho wa mwezi ndo uione hela nyingine... kiuhalisia nafikiria kuachana na ualimu naomba nisaidiwe yafuatayo

1. nikitaka kurudia ndoto zangu ni chuo gani ntaweza kusomea fani ya video shooting & editing niwe professional wa movie?

2. ni fani gani nyingine at least inalipa kwa mtu wa combination ya HKL?

ntashukuru endapo nitapata ushirikiano wa dhati.
 
Pole sana kwa frustration hizi. Jifunze kitu kimoja, kwenye maisha huwezi kupata kila unachotamani.

Sijajua utapataje hizo ndoto zako, lakini umeshajiuliza utajilipiaje hiyo shule endapo utaipata? Na je baada ya kumaliza shule, mtaji wa kujiajiri unaupataje? Ama utapata ajita ambayo nadhai itakuwa very frustrating manake kina ray wana hizo biashara na hawajasomea. Akikuajiri atakulipa tzs laki 2 labda.

Kila la kheri. Kwa issue ya kipato sidhani kama ni lazma ufundishe serikalini. Tafuta shule ya private utapata mshahara nafuu. Pia angalia jinsi ya kufanya biashara na kuongeza pato huku unaatamia ndoto zako.
 
Ulikuwa na div ngapi F6?ila ucwakatishe tamaa wazee wa BAED mkuu
 
Habari wana jf, labda nitoe tu historia kwa ufupi... mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu mwaka juzi (2011),na kada niliyoisomea ni ya ualimu. ( kwa sasa ni mwalimu), mnamo mwaka 2008 nilipomaliza form six, nilipo omba vyuo nilipata kuchaguliwa vyuo viwili yaani kozi ya ualimu na mass communication.na nilichaguliwa elimu kwani aliyekuwa ananielekeza kujaza form aliniambia niweke education kama first choice, sikuwa na jinsi kwani uelewa ulikuwa ni mdogo wa nini nifuate...... Malengo yangu yalikuwa natamani sana kusomea video shooting and editing (kwani nilitamani sana kuwa mtengeneza movie na music video). ila nilijikuta nakosa elimu ya maelekezo ya ni jinsi gani nitaweza kufikia ndoto yangu., Nilipo washirikisha wazazi walikataa kata kata mimi kusoma mass communication kwani waliponda sana wakisema uandishi wa habari hauna dili ( sana sana baba, kwani yeye by that time alikuwa ni afisa elimu vifaa na takwimu (SLO)) sikuwa na jinsi kwani nilipoendelea kubisha baba alitaka kunizira kuwa nilienda mass communication nikikwama nisimuhusishe kwani aliamini naweza kosa mkopo, na education mkopo ulikuwa ni wa kufikia. siyo siri nilienda chuo kishingo upande, mwaka wa kwanza karibia wote nilikuwa ni wa kulalamika tu, second year nikaaza kurecover. nikamaliza 2011, mwaka 2012, nikaajiriwa wilaya moja hapa tz, kama walimu wa o level kwenye shule moja ya kata. kiukweli nafundisha ndiyo ila moyo wangu na mapenzi hayako kwenye ualimu kabisa.... pia maslahi madogo... mshahara wenyewe full makato, na ukipata mshahara inabidi usubiri mpaka mwisho wa mwezi ndo uione hela nyingine... kiuhalisia nafikiria kuachana na ualimu naomba nisaidiwe yafuatayo

1. nikitaka kurudia ndoto zangu ni chuo gani ntaweza kusomea fani ya video shooting & editing niwe professional wa movie?

2. ni fani gani nyingine at least inalipa kwa mtu wa combination ya HKL?

ntashukuru endapo nitapata ushirikiano wa dhati.
Mkuu mimi nakushauri ungejiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi pengine vitakufaa make kazi za kutumia akili naona huziwezi.
 
Ualimu usikuchose
Wenzio wamefundisha kijijini haswa, tena kulala saa 12 jion, umeme hamna, maji chumvi tupu. Mashine ya kusaga km 6. Leo hii ni walimu vyuo vikuu. USIOGOPE MAISHA WALA KUKATA TAMAA
 
Pole, kwani hauwezi kufundisha tuition mara moja moja ujipatie pesa katikati?

Pia kufuata ndoto yako basi anza kusoma unachootaka ukiwa bado unafundisha kuna masomo ya kusoma bila kuhudhuria darasa etc.

Ila duh hao watoto unawamwangia mambo yote wajue au? Usiwanyime jamani kwa mawazo uliyonayo.

Utakuwa sawa tu uwe unamuomba mzee msaada katikati ya mwezi ili ajue unasumbukaje.
 
Hata mie nilikuwa na ndoto km zk lakn kwa sasa nafkria kutengeneza fursa kwny mysha ya ualimu naamin Mungu ndio mpangaji na mpaji.
 
Na wewe ni mwalimu!?? "km, zk,kwny,mysha"...!!??
 
mkuu i urge you to follow your dream because its worth something...hata kama huto pata kama ulivyopanga huko kwenye mass communication but atleast unajuaa kwamba at one point in life ulifuata ndoto yako
 
Acha kazi ili uone ilivyo kazi kupata kazi !!
Ulichonacho mkononi ni bora kuliko unachokitarajia !!
 
Ndg uwalm cku hz umekua mgum kwasabab mnanyanyasana wenyewe kwa wenyewe,mwalm mwenzako anapopewa uafsa katka ktengo flan tatzo wanasahau wametokea wap....!nando hao mnapowapelekea shida zenu wanawanyanyasa..pole sana ila ifanye kama njia2 yakufika kule unapotaka mana serikal ndoinavyotaka nandomanakamwe ajira upande wa elm haijkutoshereza
 
Tatizo ni 'mind set' yako unadhani utaendelea kwa mshahara,hata wafanyakazi wa Benki kuu wana vyanzo vingine vya mapato
 
Kuna jamaa yangu mmoja ameacha hiyo kazi yenu yupo mjini anatafuta kazi sijui hiki kizazi kinakwenda wapi kama mwalimu ndio huyo huyo mwanafunzi atakuaje?
 
Back
Top Bottom