Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.
Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?
unaweza ukaambiwa na usichape lapa vile vile, jamaa wakazidi kukucheka ujinga. Jibu la uambiwe au usiambiwe litategemea kama unapenda "love iz blind" au unapenda "love is passtime".bora kuambiwa uchape lapa mapema shost,
kuliko utembee kifua mbele huku wenzako
wanakucheka ujinga, lol! inakera kweli.
Lakuvunda litanuka tu,mimi sipendi kuhusika na mambo ya watu,ukweli utadhihirika.
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...
Bora uambiwe ujue namna ya kutatua tatizo mapema
swali linakuja je una roho ya kupokea hayo unayoambiwa
au ndio inakuwa chonzo cha ugomzi wa mleta habari na mwenye habari
Tatizo kubwa la kuambiwa hata na watu wa karibu ni uhakika wa maneno..kuna vitu kama chuki, wivu au tabia ya mtu kugombanisha watu kwa maneno ya hapa na pale. Labda awe mzazi au siblings wako hapo unaweza kuamini!..sijui marafiki au nani wengineo, hapo pagumu!!..
Watu wengine hawapendi kuingilia mambo ya wapenzi hivyo wanakaa kimya hata kama wan uhakika na kitu, mana wapenzi wanaweza kugombana na kurudiana wao wakaonekana wabaya hata kama walikuwa na nia njema..
Upande mwingine hamna kitu kinaumiza kama kuchoreka pale utakapopata ukweli wakati ni too late...
Tatizo la kuambiwa ni hili cku mnapatana jamaa atakubembeleza hadi umuambie aliyekuambia wewe utajikoki nakumueleza alisanua, baada ya hapo kuna mawili either jamaa agombane nae au amtongoze sasa hapo ndio shida yenyewe.
Akili za kuambiwa changanya na za kwakoUkiambiwa kuwa anagonoka na rafiki yako utafanyaje?