Uambukizwaji, dalili na chanjo ya ugonjwa wa Polio

Uambukizwaji, dalili na chanjo ya ugonjwa wa Polio

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Ugonjwa wa Polio husababishwa na virusi vya Polio, ambavyo huenezwa kwa njia ya kula na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa.

Ugonjwa huu unaweza kuwapata watu wa rika zote lakini watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ndiyo wanaoathirika zaidi.

Hushambulia mishipa ya fahamu hatimaye husababisha kupooza kwa misuli, hasa ya miguu, mikono au yote kwa pamoja, na pengine misuli ya kiwambo (diaphragm) na kusababisha kifo.

E663C5D9-51D4-45B1-88D2-0B0B32802F11.jpeg


Njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa huu ni kupitia chanjo (OPV) ambayo hutolewa kwa watoto kwa njia ya matone ya kumeza mara nne kwa utaratibu ufuatao-
  • Chanjo ya kwanza, mara tu mtoto anapozaliwa
  • Chanjo ya pili, mtoto akifikisha umri wa wiki 6
  • Chanjo ya tatu, mtoto akifikisha umri wa wiki 10
  • Chanjo ya nne, mtoto akifikisha umri wa wiki 14
Kwa kuwa ugonjwa wa polio hauna tiba, pia husababisha ulemavu wa maisha na hata kifo, ni muhimu kuhakikisha kila mototo anapatiwa chanjo zote nne na akamilishe afikiapo umri wa wiki 14 (miezi mitatu na nusu).

Chanzo: Mpango wa Taifa wa Chanjo Tanzania
 
Je zipi ni tofauti kati ya IPV na bOPv...ili hali zote ni chanjo za kuzuia Polio.

#MaendeleoHayanaChama
 
Je zipi ni tofauti kati ya IPV na bOPv...ili hali zote ni chanjo za kuzuia Polio.

#MaendeleoHayanaChama
1. Kutengeneza kinga
IPV huwa na ufanisi mkubwa katika kutengeneza kinga kinywani, hivyo kukata kabisa nafasi ya kuambukiza ugonjwa huu kupitia kinywa. Lakini huwa na uwezo mdogo wa kutengeneza kinga imara kwenye tumbo na utumbo hivyo nafasi ya kusambaza na kuambukiza ugonjwa huu kupitia choo huwa bado ipo hata baada ya kupata chanjo.

OPV huwa na ufanisi wa kutengeneza kinga sehemu zote mbili, kinywani na tumboni/kwenye utumbo hivyo nafasi ya kusambaza/kuambukiza ugonjwa kupitia choo almost huwa haupo kabisa.

2. Gharama

IPV huwa na gharama kubwa kuliko OPV

3. Njia ya kutolewa
OPV hutolewa kwa matone, IPV kwa njia ya sindano.
 
Back
Top Bottom