MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Mtaji wa kwanza kwenye biashara ni uaminifu. Ukiwa mwaminifu unaweza kuvumilika kwenye madhaifu mengine. Uaminifu ni bidhaa muhimu kuwa nayo kwenye biashara.
Nchi yetu bado ina uhaba mkubwa wa watu waaminifu hasa kwenye biashara na ujasiriamali. Imefikia wakati ukisema wewe ni mjasiriamali unaonekana kama mtu mjanjajanja usiye mwaminifu. Yani kama tapeli fulani la kuogopwa.
Kwa sasa wakati dunia ikishuhudia mabadiliko ya kiteknolojia yanayosababisha ufanyaji wa biashara kubadilika pia. Siku hizi biashara zinafanyika kidigitali. Mteja ataona tangazo online ataagiza bidhaa na kulipia kwa mobile money na mtumaji naye atafanya delivery kwa taxi mtandao.
Yaani mambo yamerahisishwa sana. Ila inasikitisha sana kuona huu urahisi ukitumika vibaya na watu kuishia kudhulumiana. Muuzaji anaweza lipwa na asitume mzigo au akatuma tofauti na alivyoagizwa.
Wateja nao wapo wasio waaminifu. Ukisema uwatumie mzigo walipe baada ya kupokea inakuwa ndo umepoteza jasho lako kwa maana ya hawatalipa. Kimsingi pande zote muuzaji na mnunuzi zina matatizo ya kukosa uaminifu. Kuna wafanyabiashara wadogo wengi waliaminiwa mali kauli wakaingia mitini.
Ninashauri watu tuwe waaminifu. Mungu awabariki.