Uaminifu ni silaha ya kulinda na kukuza biashara

Uaminifu ni silaha ya kulinda na kukuza biashara

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (57)✍️
Hebu fikiria, tunaagiza magari kutoka Japan na nchi nyingine, jinsi tunavyoyaona magari kwenye mitandao ndivyo ambavyo tunaletewa na kuyapokea bandarini kama tulivyoyaona. Huo ni uaminifu wa hali ya juu kwenye biashara.

Lakini unakuta gari hilo hilo lililotoka Japan, akikabidhiwa mwafrika wa Bongo aliendeshe kutoka Dar es salaam kwenda mkoani, gari litafika likiwa limebadilishwa au kupotea baadhi ya vifaa. Inasemekana hadi kwenye Show Rooms (Yard) magari yameanza kuchakachuliwa Kilomita.

✍️Kama wewe ni mfanyabiashara zingatia.......
✓Uaminifu humjengea mtu heshima.
✓ Uaminifu hukuza biashara.
✓ Uaminifu ni Tangazo kubwa la biashara.
✓ Uaminifu huleta wateja wapya na kutunza wateja wa zamani.
✓ Uaminifu hufungua milango ya mafanikio.
✓ Uaminifu unaunganisha watu wengi.
✓ Uaminifu huleta amani ya biashara.
✓ Uaminifu hutunza marafiki wema.

Right Marker
Dar es salaam
 
Hii ina-apply kwa watu tunaowaweka kwenye biashara zetu watufanyie kazi. Kiukweli wanaturudisha nyuma sana.

Unakuta umejinyima umedunduliza mtaji ufanye biashara ili mtaji ukue uachane na maisha magumu. Lakini uliemuajiri anakuibia unaanza na moja unarudi kwenye msoto.

Vijana wa kazi wanaturudisha nyuma sana.
 
Hii ina-a
pply kwa watu tunaowaweka kwenye biashara zetu watufanyie kazi. Kiukweli wanaturudisha nyuma sana.

Unakuta umejinyima umedunduliza mtaji ufanye biashara ili mtaji ukue uachane na maisha magumu. Lakini uliemuajiri anakuibia unaanza na moja unarudi kwenye msoto.

Vijana wa kazi wanaturudisha nyuma sana.

Ni kweli kabisa. Hawa vijana wa kazi ni shida sana sana. somo la uaminifu hawajawahi lielewa hata uwafundisheje. Wanarudisha nyuma maendeleo ya waajiri wao na ya wao wenyewe kwa ujinga wao! Usiache kuwawekea mitego mara kwa mara ... na ukimshuku tu mwondoe kabisa... potelea mbali
 
Kuna mmoja leo nimemkomesha, anajidai anauza vipodozi i ,nikalipia aniltee kumbe hana biashara. Nikwatafuta wazee wa kazi wakamdaka..... atajua hajui
 
Back
Top Bottom