Uaminifu

Uaminifu

Edwardo Ommy

Member
Joined
Feb 6, 2020
Posts
36
Reaction score
52
Uaminifu ni nini ?

(kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: faithfulness) ni tabia njema ya mtu inayomfanya akubalike kwa wengine hata wakampatia dhamana ya pesa au mamlaka fulani.


Katika Biblia, Hosea ni kielelezo cha uaminifu wa mume kwa mke wake. Mchoro mdogo wa mwaka 1340 hivi katika Klosterneuburger Evangelienwerk, fol. 7v.

Kwa kawaida unapatikana kwa kuishi sawasawa na maadili ya Mungu, dini au jamii; kwa mfano sheria na taratibu za asasi, kampuni au serikali.

TIKETI YA MAFANIKIO MWANADAMU NI UAMINIFU
Ninapozungumza uaminifu siyo neno geni Kwa watu kwasasa ni neno ambalo linazungunzwa mala nyingi Zaidi. Lakini kuzungumzwa Sana Na watu siyo sababu ya Mimi kushindwa kukuambia maana ya uaminifu. Unaweza kuweka maana yeyote kuhusu uaminifu lakini Mimi ninapozungumza uaminifu ninakuwa Na Maana nyingi lakini chache kati ya hizo nyingi ni

Uaminifu ni tabia ya kubaki kuwa mkweli Kwa mtu Au kitu Na kusimamia Ukweli Bila kujari mazingira uliyonayo. Au unaweza kusema Uaminifu ni tabia ya kutimiza ahadi uliyoahidi. Au unaweza kusema uaminifu ni Kufanya kitu katika Hali ya Ukweli na uwazi. Au unaweza kusema Uaminifu ni kufanya kitu katika unyoofu wote. Kuna maana nyingi Sana za uaminifu lakini yote ya yote ni kubaki kuwa mkweli Na kuwa Na msimamo thabiti juu ya kile unachoahidi Kwa maneno mengine ni kuwa Na msimamo usiobadilika badilika, kujiungamanisha, kujitoa kuhakikisha unasimamia kile ulicho ahadi Bila kujari ni mazingira gani unapitia wewe baki katika Ukweli kuhakikisha unatimiza kile ulichoahidi/ kile ulichopewa kusimamia katika misingi ya haki.

MATOKEO CHANYA YAKUWA MWAMINIFU KATIKA JAMBO LOLOTE.

Hakuna jambo jema kwa mtu kama kuwa mwaminifu yeye mwenyewe binafsi, kwa wazazi wake, watoto, kazini, kanisani/msikitini na kwenye jamii kwa ujumla. Zifuatazo ni faida za kuwa mwaminifu.

1. Kuaminika zaidi
Moja ya faida kubwa ya uaminifu ni jamii kukuamini, kazini, kwako au kwa wateja wako na kama wewe ni mfanyabiashara na ni mwaminifu kwa wateja wako, unafungua kwa wakati, unawahudumia vizuri kwa lugha mzuri na yakupendeza, bei sio za ubabaishaji, mtu akiacha pesa yake anaikuta, basi utajijengea idadi kubwa ya wateja kwa sababu ya uaminifu wako wao kwa wao watapeana taarifa zako,

2. Hujenga mahusiano imara na bora.
Ukiwa mwaminifu kwa jambo lolote lile lazima mahusiano yako na watu yatakuwa mazuri, iwe ni kazini, shuleni, kwenye nyumba za ibada, kwenye sehemu za mahitaji na sehemu nyingine nyingi hutasikia migongano na lawama kutoka kwa watu husika ambao labda unafanya nao kazi, bosi wako, walimu au wanafunzi, ndoa yako nk. Maeneo hayo yote yatakuwa bora na imara hivyo uaminifu ni jambo nyeti sana na ni vyema kulitilia mkazo na kulitimiza.

3. Huimarisha ushirikiano.

Mtu mwaminifu huwa na ushirika mzuri na watu wenzake, mfano wewe kama ni boss kuwalipa wafanyakazi wako kwa wakati, kutimiza ahadi zako au mzazi kutimiza ahadi unazoahidi kwa watoto au mke hii inatoa motisha na ushirika mzuri toka kwa wafanya kazi au kwa watoto kumfurahia baba au mama yao. Vile vile hata wafanyakazi wakitimiza kazi zao kwa uaminifu ushirika huwa ni mzuri kati yao na kiongozi wao. Na maeneo mengine ambayo sijayataja kama mifano hai kwenye maisha yetu.

4. Utapewa nafasi zaidi.
Hii hutokea kwenye jamii, makazini na hata nyumbani. Unapokuwa mwaminifu ndipo nafasi ya kupewa nafasi zaidi iwe ni kazini, nyumbani kwa wazazi basi nafasi hizo huwa ni kubwa na hata maeneo mengine mengi.

5. Utakula vya sirini.
Mtoto mtii na mwaminifu kwa wazazi wake hula vya uvunguni kwa sababu huyu mtoto hutekeleza majukumu yake kama mtoto vyema bila kusukumwa wala kubembelezwa na anajua wajibu wake. Ndivyo hivyo hata kwenye familia, jamii kwenye biashara, kazini ni rahisi kushirikishwa mambo makubwa ya kiofsi kwa sababu wanajua wewe ni mwaminifu katika kutimiza, kutekeleza na kutunza siri za kampuni vyema hivyo ni rahisi kupata taarifa mapema.

6. Ni rahisi kusaidika.
Mtu mwaminifu huwa anatengeneza mazingira mazuri ya kupata msaada kwa haraka either wa kifedha, kimawazo au msaada wowote ule sababu kubwa ni ule uaminifu aliojijengea kwenye mazingira yake ya maisha, iwe kwenye biashara, benki, nyumbani, kazini na maeneo mengine mengi ambayo yanamhusu.

7. Ni njia bora ya kuimarisha ndoa na mahusiano

Hakuna kitu kizuri kwenye mahusiano au ndoa kama uaminifu. Uaminifu ni ufunguo wa furaha ndani ya ndoa, ni ufunguo wa mafanikio na Uhuru wa nafsi, ufunguo wa kuyaona mahusiano au ndoa yako ni ya maana kuliko zingine na kuongeza thamani ya penzi lenu ambalo litastawi na kuchanua vyema. Hivyo uaminifu kwenye mahusiano na ndoa ni msingi imara.

8. Utatetewa wakati wa Magumu au mapito.


Changamoto kubwa kwa watu ni kutokuimarisha mahusiano yao na watu wengine kwa njia ya amani, waonevu, wadhurumaji, kufanya mambo bila kujua kuna kesho ambayo inaweza kuwa na uhitaji wa wale watu unaowatendea ndivyo sivyo. Mtu mwaminifu hujiongezea nafasi ya kutimiza malengo yake kwa sababu ukifanya kwa uaminifu kwa watu basi watu hao hao kuna wakati watakuwa daraja lako la kufikia jambo Fulani maishani mwako, katika uonevu utapata watetezi wengi.

9. Mtu huishi kwa amani na furaha.
Mtu mwaminifu huishi kwa furaha, amani lakini pia huwa na upendo, hapendi kuiona nafsi yake ikisononeka, ikiumia kwa kuidhurumu kwa kukosa uaminifu, hupenda kutenda jambo kwa wakati na uaminifu kwa wengine. Kutokana na kufanya mambo hayo kwa uaminifu basi moyo na akili yake hubaki huru bila deni maana amefanya kila jambo kwa wakati na uaminifu.

10. Uaminifu ni dawa
Huondoa msongo wa mawazo, humfanya mtu kuwa huru asiye na hatia, kumbuka mtu asiye mwaminifu huishi kwa uongo, muda wote anatengeneza mazingira ya kuutetea uongo wake na kuuhalalisha bila kujua kuwa anajiumiza binafsi, anatumia nguvu nyingi kupanga namna ya kudanganya wakati kama angeamua tu kuwa mwaminifu nguvu ile ile angetumia kwa ajili ya kufanya jambo lenye maana maishaini

Kwa hiyo ni vyema kutengeneza mazingira ya kuaminika na wazazi, watoto, mke, mume, jamii, na katika maeneo yote unayokuwa.

Kwa sababu uaminifu hutengeneza mahusiano mazuri na kuaminika na watu, na kama basi ikitokea kuna fursa inatokea watu watakufikiria na kukupa nafasi.
 
Haya maelezo yako niya kweli ila ili mafanikio Yakamilike/ Yafanikiwe kwa Amani na Furaha..
unamuhitaji Yesu akufunike na Neema Yake yani Nguvu za Mungu, bila hivo kunawahuni watumia majini na watumishi wa shetani wakikukuta upo mweupe bila Nguvu yoyote lazima wakuchake na kukuharibia kabisa ikiwapendeza wanakukula na nyama kabisa.
 
Back
Top Bottom