Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"

 
By definition a mistake is made knowingly. Kwako wewe CDM wamefanya maamuzi mabaya kwa kujua na kufahamu.
sio kila mistake is made knowingly. Kuna mistake zinafanywa bila kujua, huku mfanyaji mistake hizo, akiamini kuwa that is the right way but at the end of the day, time will prove them wrong.
 
Pasco,

Kwangu mie kama ikithibishwa kuwa fulani ni mhujumu uchumi na Chadema wakamyonga, mie sina matatizo na hilo.

Sasa hebu angalia kesi za EPA, Meremeta, UDA, Tanesco nk na ushahidi upo waziwazi wa wizi uliotokea. Unataka watu waendelee kupozwa kwa kubadilishiwa kazi maana ukichukua maamuzi magumu, PASCO atakuja juu na kusema kuna high price to pay.

Yes, siku zote kuna high price to pay bila kujali unafanya nini. Ukikata mkono wenye kansa, unapoteza mkono na usipoukata, kansa inakumaliza mwili mzima. Sasa ufanyeje? Wale madiwani walikuwa kansa kwenye mkono ndugu yangu na lazima kitu fulani kifanywe.

Kumbuka kuna wale 5 waliomba msamaha na hadi sasa hakuna anayewaongelea. Ila hawa wao waligoma waziwazi na kuchimba mkwara mzito sana kwenye TV kuwa hawatishwi.

Swala la kuwa ukiwafukuza chama basi wanapoteza ubunge, naona hilo waulize CCM. Tangu mwaka jana lilijadiliwa na ikatolewa uamuzi kuwa Bunge ikae na ilibadilishe hilo ili kuwe na wagombea huru. Kwa kesi kama hiyo, hawa jamaa wangeliendelea kuwa Madiwani wasio na chama au hata kujiunga na chama kingine bila matatizo. Sasa basi kama hilo nalo unawalaani Chadema, mhhh.....

Mie napenda sana nchi iwe na viongozi wa kuchaguliwa bila ya ulazima wa kutegemea chama. Kuna riport fulani nilikuwa nasoma nchi moja huko Europe kuwa Marais wa Mikoa ambao hawakufungana na chama chochote, mikoa yao inafanya vizuri sana. Nina wasiwasi kuwa mikoa mingi itakuwa inawachagua hawa watu wa namna hii. Kwa vyeo kama vya Madiwani, ningelifurahi sana kuwe na madiwani wasiofungamana na chama chochote kwani hapo inakuwa ni mtu na wananchi wake waliomchagua. Hakuna haja ya kusimama upande wa chama hata kama hukubaliani nao. Haya mambo yanarudisha sana maendeleo ya wananchi na pesa nyingi huibiwa na kupelekwa kwenye chama husika.

Labda muda umefika sasa watu tuanze kudai walau madiwani wasiwe na ulazima wa kufungamana na chama cha Siasa.

Kwangu mie naupongeza sana uongozi wa Chadema kwa kuwatimua hawa jamaa. Hata kama walitukanwa na Lema, kwanza wangeliachia hayo madaraka na mwisho wakaja kumshitaki Lema kwa kuwasingizia kuwa wamepokea Hongo. Sasa wao kubishana na CC wakati siyo CC nzima ya CDM ilisema hayo maneno, wanakuwa wapuuzi. Au kweli wametumwa kufanya fujo au hawajui wagombane na nani ila lengo lao wanataka tu wazushe ugomvi kwenye Chama. Nasikitika tu kuwa wamechelewa sana kuwatimua.

Hiki kitendo kitatoa ONYO kwa wale wote wanaofikiri kuwa waende Chadema ili kupata MLO.
 
.....labda wewe unaona hivyo Mkuu lakini mimi sioni kama kuna udikteta kwenye maamuzi haya mazito hasa ukitilia maanani Madiwani hao walifahamishwa kuhusu makosa yao na walikuwa na muda wa kutosha kabisa kuyarekebisha lakini hawakuona umuhimu wa kufanya hivyo.

 
Sikonge, kwanza asante, wewe ndie mchagiaji wa kwanza kwenye hoja hii ambaye uko objective. Nakubaliana na hoja zote ulizojibu, ila nalia na moja tuu, "principles of natural justice". Wale madiwani walihukumiwa bila kuujitetea na hatimaye wamevuliwa uanachama nadhani ni bila kujitetea, japo taarifa rasmi imesema walipewa fursa ya kujieleza wakakaidi.

Hiki walichokifanya Chadema, sasa ni kichochea cha kutenganisha wateuliwa wa chama na wachaguliwa wa wananchi. Tulipinga sana ile dhana ya 'party supremacy', lakini hiki ndicho kilichofanyika. Walioadhibiwa sio hao madiwani, bali ni wale wananchi mamia kwa maelfu waliowachagua.
 

hoja namba 4 ni upotoshaji wa hali ya juu. don generalize things Posco. ni kweli kwamba Bwana Ndesa akikaa kando leo ukaitishwa uchaguzi wanamoshi watachagua chama tofauti na chadema?

basi if that is the case, hao madiwani wahamie 'upande wa pili' wagombee na tupime mapenzi ya wana-arusha kwa hawa jamaa waliotimuliwa.
 
Ng'wanangwa, siasa za Kaskazini ni kitu ingine, wanachagua watu na sio vyama. Kama madiwani waliofukuzwa, watapeleka kilio chao kwa wananchi, sio tuu wananchi watakuwa nyuma yao, bali the consequences kwa Chadema ni mbaya.

Hawatajiunga CCM kamwe, kwanza watapinga kufukuzwa, pili wataiburuza Chadema mahakamani na watashinda!, Chadema Arusha, itajikata kama pande na ku side na NCCR au hata TLP, come 2015, Chadema italitoa sadakalawe jimbo la Arusha na kurejeshwa CCM kiulaini kama walivyolitoa sadaka Tarime. Wapinzani watasplit votes na CCM ni kunguru atakae jiokotea hilo jimbo katika vita vya panzi!.

Moshi Ndesa amechaguliwa na wote mpaka wana CCM, na Mrema vivyo hivyo.
 
Hii ni comment ya mwana jf fulani kuhusu how they argue na ku tackle some issues.
 
Nilikuwa najua chadema watafanya hiviwana hamu kubwa mno ya kuionesha jamii kwamba wao sio waoga wa kufanya maamuzi
hata kama yatawa cost ,hii inanikumbusha uchaguzi uliopita walivyopoteza jimbo la Tarime.

CHADEMA sio wanasiasa kabisa, mwanasiasa lazima ujue ku commpromise kwa maslahi yenu na chama. Obama aliposhinda urais na chama chake kuwa na nguvu kubwa, alikuwa na option ya kumuondoa joe lieberman kwenye kamati za congres lakini ali compromise na kumuacha tu,licha ya Joe Lieberman kuungana na Republicans kumponda Obama wakati wa uchaguzi.....

CHADEMA ni kama mtoto mdogo anaejaribu ku prove kuwa yeye ni mtu mzima mwisho hufanya madudu tu mengi..... ukiwa mtu mzima huitaji ku prove anything..... itwacost mno hiiiii, mark my words
 


Niliwasikia ile siku wakikaidi, kuwa Mhe. Godbless Lema aliwatuhumu kushikishwa chochote kitu, Chadema makao makuu wakaunda tume ya kuchunguza, tume ile haikuwahoji chochote, bali ilituma ripoti yake kuwa ni kweli, walipokea chochote kitu.

Makao Makuu hawakuwauliza chochote, bali kuwaamuru kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya muafaka ule. Ndipo wakajibizana na CC yao kwamba kwanini wahukumiwe bila hata kuulizwa?. Hata mkosaji, anastahili kutendewa haki, jee hao madiwani wametendewa haki?.
 
kuna vingi mno wamekosea so far
na hawajakaa chini kutafakari

ubishi na ugomvi usio wa lazima na cuf na nccr umesababisha
wakose kamati za bunge.....hawajifunzi kutoka kwa zito? iweje zito akubalike na cuf na nccr na udp lakini wengine wakataliwe??????/

huwezi kuwa a succesfull politician bila ku compromise
 
The Boss, the boss is always right, and he does no mistakes. Humu jf, kuna watu wanaamini baadhi ya vyama ni malaika!

Binafsi nitampenda zaidi adui anayenikosoa ili kama nimejidhania nimesimama, niangalie nisianguke kuliko rafiki atakayeishia kunisifia kwa nyimbo na mapambio, huku ndio ninaangamia ki kweli kweli. Wewe ni miongoni mwa marafiki wa kweli wa Chadema.
 
Pasco naamini hizo ni hisia zako, mimi naona ule uamuzi ni sahihi. Kama wao walikuwa na lengo la kumaliza mgogoro huo basi wangeshirikisha uongozi wa ngazi za juu na siyo kujichukulia maamuzi mkononi.

Pia kitendo cha kuitunishia misuli CC ni utovu wa nidhamu usiovumiliwa kwa chama chochote makini na siyo CDM pekee. Tatu kitendo cha kukataa kuhojiwa kila mmoja peke yake ni ishara tosha kabisa kuwa kuliwa na agenda ya siri pale.

Kauli kama CDM haijatendea haki wananchi itaamuliwa na wananchi wenyewe katika chaguzi ndogo zitazofanyika hivi karibuni kwa kukosoa au kukubali maamuzi hayo Pasco.
 
Hivi kwa nini viongozi wa chadema wasingeenda wenyewe arusha
na kuzungumza na hao nadiwani kisiasa zaidi kuliko kuendesha mambo
kisheria mno, utasema ni chama cha mahakimu?
 
Hili nililisemea sana siku ile kususia matokeo na kumsusia aliyetangazwa mshindi. Kwa maoni yangu, kuna baadhi ya maamuzi hufanywa kwa papara. Kuna situation ambazo zinahitaji busara kutatua matatizo kuliko going by the books by sticking kwenye kanuni.

Kuna baadhi ya matatizo, they just need time to heal, nimewalaumu for wrong timing. Kipindi hiki nilidhani ni cha kujipanga kwenda kuitwaa Igunga with a bang!, hilo la madiwani lingewekwa kiporo. Kuna mada yangu moja nilisema Chadema hawajajipanga, nilishambuliwa sana. Kwa maoni yangu, miongoni mwa madhaifu makubwa ya Chadema, ni lack of the right strategies.

Miongoni mwa wafuasi wake humu JF, ni ma strategist wazuri tuu judging by their writings, lakini sijui kwa nini hawakisaidii chama chao kwa the right strategies?!.
 
Mzee wa Rula, sehemu kubwa ya andiko langu ni opinion tuu backed by facts na trends, hivyo sio hisia.
Maadamu umeweka kipimo ni hizo chaguzi ndogo, tusubiri na tuone, time will tell.
 
hivi kwa nini viongozi wa chadema wasingeenda wenyewe arusha
na kuzungumza na hao nadiwani kisiasa zaidi kuliko kuendesha mambo
kisheria mno,utasema ni chama cha mahakimu?????
The Boss, kuna baadhi ya maamuzi huhitaji busara zaidi, lakini hata hizo busara, ni lazima kwanza ziwepo, ndipo zitumike!
 

mkuu
chadema hawajui kabisa politics behind the door
wanahitaji kujifunza hilo somo
unamuona raila odinga,amefikaje hapo????
wangejifunza hawa watu....

wakati wa reagan,marekani waliwauzia silaha iran, unaweza shangaa hapo inakuwaje,wakati iran ndio adu wao mkubwa? ni politics behind the door,na kuwa na strategy za mtazamo wa mbali

hivi tmesahau pia jinsi chadema walivyompoteza mwenyekiti wa bawacha, hawajifunzi kabisa....
 
Hakika sirtawasifia chadema kwa maamuzi haya ya kufukuzana eti kwa utovu wa nidhamu; naona wachangiaji wengi wanayafananisha na ufisadi, hapana si hivyo!

Haya aliyafanya sana Mzee Mrema akishia kuiuwa NCCR, amekwenda kuyaendeleza TLP matokeo yake wote tunayaona. Nilisema pale awali kwamba haya maamuzi yamekaa kiserikali zaidi na sio ya kisiasa; tunayakumbuka enzi za Mwalimu wakati wa udikteta wa chama kimoja.
 

Pasco naamini unatambua kwamba uamuzi wa kuwavua uanachama ulifikiwa na kamati kuu ambayo ina watu wa kutosha, makini kabisa na wasomi wazuri sana vile vile.

Haya mambo unayojaribu kuyaorodhesha hata wao waliyaona, wakayajadili na kupima consequences za uamuzi wao, and they knew that there should be a price to pay.

Suala la wananchi kunyimwa haki ya watu waliowachagua huwezi hata siku moja kuinyooshea kidole chadema, hiyo ndiyo sheria tuliyonayo na wengi tunakubaliana kwamba ni mbaya.

Sasa njia bora ya kubadilisha sheria mbaya ni kuwaona wahusika na najua unawafahamu. Hapa unachojaribu kufanya ni kulalalmikia matokeo ya sheria mbaya ambayo chadema wameikuta.

Na kwa kuzingatia kwamba hao madiwani walikuwa wanafahamu kwamba walidhaminiwa na chadema ili kuwania udiwani walipaswa kuzingatia maelekezo ya kamati kuu kwa kujua kwamba hao ndio wenye dhamana ya mwisho juu ya uendeshaji wa chama. Sasa kama walikaidi kwa bahati mbaya ama makusudi pamoja na kupewa muda wa kujirudi lakini wakakaidi, na walisikilizwa ingawa unajaribu kupindisha kwamba principle of natural justice haikufuatwa, kulikuwa hakuna uamuzi mwingine chama kingechukua zaidi ya huo uliochukuliwa.

Muhimu hapa ni aheri kuwa na jeshi dogo lenye nidhamu kuliko kuwa na lundo la wanajeshi wasiokuwa na nidhamu, hamuwezi kushinda vita yoyote.

Mwisho, nimeshangazwa na utabiri wako kwamba watakwenda mahakamani na watashinda, bila shaka unaelekea kuchukua mikoba ya marehemu sheikh yahya!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…