Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"


Kwamba chadema hawajui politics, hizi ni kauli za wanamagamba na washabiki wao.

chadema wameondoka wangapi na chama kinazidi kusonga mbele? unamzungumzia mwenyekiti wa bawacha wakati alishaondoka makamu mwenyekiti Dr. Kabouru lakini chama kimezidi kusonga mbele.

Hizo siasa mnazotaka chadema ifanye ni za huko huko mliko, wao wana siasa zao wenyewe, mtu akishindwa kujiheshimu kwa kiwango cha utovu wa nidhamu wa waliokuwa madiwani, hakuna namna ya kuwasaidia zaidi ya kuwavua uanachama. Ili watafute mahali pengine wanapoweza kufanya siasa bila kuheshimu viongozi wao wa juu.
 


Mkuu,

kwenye true democracy hiyo unayoita nidham ya jeshi hakuna
tazama marekani leo,wapo wabunge wanapinga mpaka miswada ya obama bungeni na ni wabunge wa chama cha democdrats

Sio kila atakae pinga maamuzi ya chama ahukumiwe kuwa msaliti
nini maana ya demokrasia sasa,
si tofauti ya mawazo na misimamo?
 

Naheshimu maoni yako yote, sikubliani nayo hata chembe. Sijui msimamo wako wa kisiasa. Kilichotokea ndizo siasa za Chadema, kama wewe ni mwanachama wa CDM ebu jitahidi kutumia forum za CDM kupenyeza mawazo yako hayo.

Ila kama nitakuwepo kujadili mawazo yako hayo nitakupinga kwa nguvu zote.
 
Mzee wa Rula, sehemu kubwa ya andiko langu ni opinion tuu backed by facts na trends, hivyo sio hisia.
Maadamu umeweka kipimo ni hizo chaguzi ndogo, tusubiri na tuone, time will tell.
Nakubaliana nawe kabisa Pasco usahihi wa maamuzi hayo ni suala la muda na si malumbano tena.

Nashukuru kwa mtazamo wako mzuri lakini kwa taarifa muafaka ule uliongiwa na wale madiwani wa CDM ulikuwa na mawaa kiasi hivyo kujenga sintofahamu nyingi. Kuhusu principle of natural justice ulisoyosema, mimi nadhani walipewa, ila ni ujeuri wao walijaribu kuonyesha kuwa hakuna jambo kubwa linaloweza kuwasibu zaidi ya kupewa onyo au karipio kali.

Binafsi naamini kabisa kuwa hakuna maamuzi yasiyokuwa na gharama kabisa hivyo ni tumaini langu katika hili ni lazima kutakuwa na gharama ikizingatiwa kuwa wale jamaa wanasiri kiasi za chama hivyo ni lazima watazitoa ili kukinukisha chama.
Mwisho time will tell.
 

Mwita Maranya, kwanza asante kwa kulitambua hili la sheria kandamizi.

Nakubaliana na wewe kuwa Chadema wameikuta hiyo sheria mbovu, nilichosema, ni kwa vile Chadema wanaijua hiyo ni sheria kandamizi, na inakwenda kinyume cha katiba ya JMT, mimi niliwategemea Chadema kuwa wao ni chama cha watendahaki, hivyo sikuwategemea kuitumia sheria hiyo kandamizi kuwakandamiza wananchi wa Arusha walioipa Chadema dhamana kubwa ile.

Nilitegemea Chadema kwa vile ina jeshi dogo kuliko mahasimu wao, basi fighting strategy yake, ingekuwa 'consolidation' of whatever little it has on its hands, kumbe its the other way around, ndio maana kuna mahali nimesema, "safari bado ni ndefu".
 

Pasco,itakapotokea kile unachokidhania kikawa sivyo (najua hofu yako ni CDM kupoteza viti vya udiwani),utakuja tena kutupa analysis tofauti na hii? Maana unaonekana kabisa ku underestimate the thinking capacity ya wana A-Town.
 


kama wote walioondoka walienda ccm
ungekuwa na pointi but wote tunajua
kafulila na yule mwenyekiti wa bawacha wameenda wapi na wenye akili wanaona hasara ambayo chadema wamepata
 
Pasco,itakapotokea kile unachokidhania kikawa sivyo (najua hofu yako ni CDM kupoteza viti vya udiwani),utakuja tena kutupa analysis tofauti na hii? Maana unaonekana kabisa ku underestimate the thinking capacity ya wana A-Town.

wewe unazungumza nini??????
tarime ipo wapi now??????
 

Sheria hiyo kandamiziambayo hata mimi siiungi mkono inawanyima wananchi haki ya kuendelea kupata huduma ya mwakilishi wao waliyemchagua, sheria hiyo haiwaelekezi madiwani kutotii maamuzi yaliyotolewa na viongozi wao wa chama, nadhani uchore mstari kati ya hivyo viwili.

Najaribu kutaka kuelewa pendekezo lako ni lipi kwa hali kama hii iliyotokea kwa madiwani kukaidi maelekezo ya kamati kuu. Labda kwa ufupi tu,unaweza kuniambia wewe kwa mtazamo wako kamati kuu ya chadema ilipaswa kutoa uamuzi gani?
 

Ok, sijui utanisaidiaje suala la collective responsibilities, sera za chama na kama wamekiuka katiba sijui pia utanielimishaje kuhusu kutekeleza ilani ya chama chako badala ya ilani ya wananchi

kumbuka kila chama kina misingi yake na pale inapogeukwa tena bila nidhamu lazima hili lifanyike

do you want to justify kwamba as long as walichagulia basi wabaki tu hata kama hawawakilishi chama kilichowasimamia??

YOUR ARGUMENTS WOULD HOLD WATER KAMA TUNGEKUA NA WAGOMBEA BINAFSI

anyway ngoja tujifunze zaidi
 
wewe unazungumza nini??????
tarime ipo wapi now??????

Kwani wewe unazungumza nini?? Tarime iko mkoani Mara, au una taarifa za kuhamia mkoa mwingine? Tarime na arusha ni maeneo mawili tofauti, siasa za tarime na arusha huwezi kuzifananisha.

Halafu usipende kutanguliza hisia kuliko ukweli halisi. Usisahau kwamba mwera alihama kwenda cuf kutokana na hali iliyojitokeza wakati wa mchakato wa kura za maoni na hakufukuzwa na kwahiyo aliondoka na watu wake wengi plus hujuma kadhaa alizofanya baada ya kugundua kwamba nafasi yake ya ushindi ni finyu. Hawa madiwani wamekaidi maamuzi ya viongozi wa juu wa chadema na wananchi wengi hususan wanachama na wapenzi wa chadema wanaunga mkono uamuzi huo.

Mazingira ya uchaguzi wa ubunge tarime 2010 na haya ya madiwani arusha ni tofauti sana, na hata hivyo chadema wameamua ni bora kuwa na madiwani wachache wenye kuheshimu mamalaka za chama kuliko kundi kubwa la watu wasio na nidhamu wala heshima kwa viongozi wao.
 
Kwa nini povu likutoke kaka/dada? Hebu vuta subira,tusubiri uchaguzi mdogo ndio mje na analysis zenu,otherwise naona kama mnajaribu kupaka upepo rangi.

wewe unazungumza siasa za kitoto
kuna jimbo chadema walikuwa na nguvu kama tarime?
walipogawanyika tu,wakapoteza....
kuwa na heshima,umeona avatar inakupa jinsia
 
Mwita Maranya, hili la kushinda, sio utabiri wa Sheikh Yahya, bali nilibahatika kufuta Tongotongo la tasnia ya sheria. Ingekuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria wanaruhusiwa kuwa ma advocate, then, kesi ya madiwani hawa ingefunguliwa na kutetewa na advocate mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria, na kushinda right away.

Kwa kumbukumbu zangu za darasa la sheria, siku ya kwanza, somo la kwanza, ukurusa wa kwanza ni What is law, ikifuatiwa na principles of natural, principle kuu ya kwanza ni
  1. No man shall be condemned unheard.
ya Hivyo kitendo tuu cha jamaa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikizwa, kunatosha kuifanya mahakama kutengua uamuzi wa CC ya Chadema.
 

bOSS,

YOU PICKED A VERY WRONG EXAMPLE... RAILA NI JAMBAZI, NA KWA MTIZAMO WA CCM, YULE JAMAA KAMA NI BONGO WANGESHAMUUA TENA KABLA HAJAFIKISHA HATA MIAKA 45

GIVE US ANOTHER EXAMPLE
 
wewe unazungumza siasa za kitoto
kuna jimbo chadema walikuwa na nguvu kama tarime?
walipogawanyika tu,wakapoteza....
kuwa na heshima,umeona avatar inakupa jinsia

Kwa hiyo Tarime ni Arusha siku hizi? Si mleta maada kasema wazi kuwa siasa za kaskazini ni tofauti kabisa na maeneo mengine? Iweje wewe ulete mfano wa Tarime kwa siasa za Arusha?
 
kama wote walioondoka walienda ccm
ungekuwa na pointi
but wote tunajua
kafulila.na yule mwenyekiti wa bawacha wameenda wapi
na wenye akili wanaona hasara ambayo chadema wamepata

Hivi wewe unaongea vitu gani hivi vya kuchekesha.

Suala si kwamba walienda magamba ama wapi, suala ni kwamba waliondoka na chadema haikutetereka.

Yani chadema kutoka kuwa na wabunge wa kuchaguliwa watano hadi 23 ndio wewe unaona ni hasara?? basi kama nyongeza ya wabunge ni 18 ni hasara basi mwalimu wangu wa hisabati kibeyo p/s alikuwa hajui kitu!!

Nadhani kimsingi wengi mnaopingana na chadema kwa uamuzi huu hamkuzoea maamuzi kama haya, mmezoea kupeana siku tisini kisha mkaongezeana siku baadae mnapotezea. Sasa chadema imefanya uamuzi ambao unawasuta sana wanamagamba na hii ni turufu kubwa sana ya chadema kisiasa dhidi ya magamba.
 

Hapo nilipobold,kwa hiyo Mahakama itaiamuru CC iwarudishie uanachama? Na kwa nini mpaka waende mahakamani kupinga wakati umesema siasa za kaskazini watu wanachagua mtu na si chama? Kwa nini wasihamie tu chama kingine na kugombea kupitia huko?
 
Sikushangai mkuu najua huu msimamo wa cdm ni mgeni kwako, but kumbuka kila jumuiya au taasisi lazima ziwepo taratibu za kufuatwa, huwezi kwenda nje ya utaratibu halafu ukasema kuwa bado ni mwanajumuiya hata baada ya kushauriwa kubadilika. So Utazoea tu!
 

Pasco kama unasomea sheria na uko ndani ya nchi hii hii lakini hujafanya jitihada za kujua ni kwa kiasi gani hao jamaa walipewa nafasi namuda wa kusikilizwa, basi nina shaka kwamba unaweza kuhitimu na kupata cheti cha sheria lakini isikusaidie sana wewe binafsi na taifa kwa ujumla wake.

Kamati ya marando ilikwenda arusha na ikawasikiliza madiwani wote wa arusha, na bado jana kabla ya kufikiwa uamuzi huumadiwani wakaidi waliitwa dodoma na kupewa nafasi nyingine tena ya kusikilizwa.

Sasa unaposema hiyo principle of natural justice haikuzingatiwa basi hapo ndo napata mashaka na uelewa wako wa hiyo principle of natural justice.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…