Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Ikumbukwe kuwa Rayvany alishajiondoa WCB lebo mama iliyomkuza tangu alipoondoka kwa Madee akiwa msanii mchanga.
Dhumuni la Rayvany kuondoka WCB pengine ni yeye kupata mafanikio makubwa kuliko yale aliyokuwa akipata pale WCB.
Ukweli unaouma ni kwamba Rayvany amekurupuka na atapata anguko kubwa lisiloelezeka.
Kumbuka kuwa WCB wanatoa 40% kwa wasanii wao huku wao wakibaki na 60%.
Asilimia hizi anazopewa msanii kazi yake ni savings, kula, kuhudumia afya yake, mazoezi, malazi, mavazi,chakula, usafiri n.k, ikiwa na maana kwamba msanii unatunzwa kama mfalme huku akimiliki mali za kifahari,
Asilimia za lebo kazi yake ni kumtengenezea msanii mazingira mazuri ya kazi, kulinda usalama wake, kulipia vibali vya serikali, kulipa wasimamizi wa lebo mishahara yao, kugharamikia promotion, kulipa hasara zote msanii anazotengeneza, nk
Majukumu haya ya Lebo ya WCB ni magumu sana ndio maana wasanii wengine au lebo nyingine zinashindwa kufika mbali na hata wakati mwingine kufa kwasababu ya kushindwa kumudu gharama za kusimama katika tasnia ya muziki.
Wale wanaomtetea Rayvany na kushutumu WCB hawana tofauti na mtu anayethamini mkungu wa ndizi huku akilaani mgomba pasipokujua asingeona ndizi bila mgomba.
Diamond Platnumz amekuwa akifanya mema mengi yasiyohesabika lakini adui zake ni wote wanaompiga vita hawana sababu nyingine zaidi ya wivu wa maendeleo yake.
Kwanini nasema kuwa kitendo cha Rayvany kuondoka WCB kitakuwa anguko katika maisha yake?
Sababu ni kuwa walipo ondoka wasanii wenzake waliomtangulia, Diamond Platnumz alipata maumivu makali na akachukua hatua ikiwemo kuwa makini kusaini wasanii n.k
Hakuna mtu ambaye atakuwa tayari kuumizwa kila siku lazima afike mahali akatae kuumizwa.
Wasanii waliopita waliondoka kwa shari na dharau kumbuka kuwa katika maisha unapomsaidia mtu alafu badae akakudharau ni maumivu kiasi gani utapata!
Hivyobasi hutakuwa tayari kuumizwa tena hata machozi ya maumivu yanaweza kumlaani aliyekusaliti na akakosa Mafanikio.