Uanaume na mazoezi ya mwili ni pacha

Uanaume na mazoezi ya mwili ni pacha

Pamoja na changamoto za maisha zinavyotupeleka kasi, hivi karibuni kumekuwa na matangazo kila kona ya kurejesha uanaume. Mshana husema urijali, Bujibuji husema nguvu za kiume, hali kwa asilimia kubwa husababishwa na mwili kutokuwa na mazoezi ya kutosha ya kuushughulisha moyo (cardio).

Jambo linalofanya kusiwe na mzunguko mzuri wa damu, sababu nyingine ni ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi mfano chips, unywaji wa soda nk. Jambo linaloongeza lehemu katika mishipa ya damu na unene, hata hivyo mtindo wa maisha wa kukaa muda mrefu katika kazi za maofisini au biashara husababisha ulegevu wa mwili na mwili kutokuwa active.

Hivyo solution mojawapo ya hayo ni kufanya mazoezi angalau mara tatu Kwa wiki mazoezi Kama kukimbia kidogo kidogo, kuruka kamba kutembea kwa kasi na mengine mengi jamani

"Uanaume na mazoezi ni pacha" kwa ustawi wa ndoa na afya ya mwili

Hakika....
 
Back
Top Bottom