Uandaaji wa uji wa ulezi

Uandaaji wa uji wa ulezi

Abra One

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
917
Reaction score
376
Wapendwa ndugu zangu naomba mnijuze ni vitu gani vya muhimu katika kuandaa uji wa ulezi na hatua zake ikibidi
 
wapendwa ndug zangu naomba mnijuze ni vitu gan vya muhimu katika kuandaa uji wa ulezi na hatua zake ikibidi


JIFUNZE KUPIKA UJI WA ULEZI KWA KUONGEZA LADHA YA VIUNGO





MWANAO ANASUMBUA AU HAPENDI KUNYWA UJI WA ULEZI? BASI JITAIDI KUUFANYA UJI HUU UVUTIE KWA KUONGEZA LADHA YA VIUNGO NA MWANAO ATAUPENDA SANA SANA. HATA WALE WENYE MATATIZO YA DIABETES WANAWEZA KUNYWA SAFI KABISA.


MAHITAJI


120 gram unga wa ulezi

240 gram ya maziwa ya maji
480 gram maji masafi
1/4 kijiko kidogo cha chai cardamom powder ( Unga wa hiriki)
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI

Jinsi ya kutengeneza uji wa chumvi – badala ya kuweka maziwa weka siagi yenye maziwa ( buttermilk ) kisha badala ya kuweka sukari unaweka chumvi. Kwa mtindo huu basi hutatakiwa kuweka cardamom powder. Mtindo huu wa kupika ni maalumu kwajili ya watu wanaoumwa Diabetes.






Chukua unga wa ulezi kisha weka katika kikaango kikavu kabisa weka katika jiko na uanze kukaanga mpaka upate harufu nzuri aka aroma kwa dakika 3 au 5 inatosha hakikisha haiungui. Lengo hasa ni kutoa harufu ya ubichi wa nafaka katika unga kisha weka pembeni.


watu wengi wakiwa wanapika uji huu huwa wanapika mpaka uunghulie kwa chini ndio wanajua umeiva lakini kwa kutumia njia hii ya kukaanga unga inaokoa muda na hutakiwi tena kupika mpaka sufuria iungue maana ule ubichi na harufu ya nafaka unakua umeshaiunguza.







Chukua sufuria kisha weka maji chemsha mpaka yawe ya vugu vugu kisha weka unga na uanze kukoroga maji yakiwa ya vugu vugu yanasaidia unga wako usishikamane na kuweka mabonge mabonge.





Endelea kukoroga mpaka unga uchanganyike vizuri kisha ongezea unga wa hiriki ndani yake.







Acha iendelee kuchemka.








Kisha ongezea maziwa. Unaweza kuongeza zaidi maziwa au ukapunguza kulingana na ladha unayopenda wewe.






Kabla ya kutoa katika jiko weka sukari ili iyeyuke haraka kisha mpatie mlaji uji ukiwa wa moto. A hearty and very nutritious breakfast and that which keeps me full until lunch. (Uji huu unavirutubisho safi sana vya kutosha kwa afya ya mlaji iwe mtu mzima au mtoto )








HATA KWA WATU WAZIMA UKINYWA UJI WA ULEZI KILA SIKU KWA LADHA ILE ILE UTAUCHOKA TU LAKINI UKIUBADILISHA KWA KUONGEZA LADHA YA VIUONGO UTAUFURAHIA SANA SANA NA HAUTAUCHOKA
 
wapendwa ndug zangu naomba mnijuze ni vitu gan vya muhimu katika kuandaa uji wa ulezi na hatua zake ikibidi

kupika uji wa ulezi........procedures si zile zile au swali lako ulikuwa wataka nini hasa
 
Back
Top Bottom