LGE2024 Uandikishaji Wapiga Kura Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Matarajio, Uhalisia na Mapendekezo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Tuingie cost mara mbili kivipi? Hebu rudia kusoma
Kengeza lilinipitia😅😅 ila mpaka sasa si maandalizi yanakuwa yapo tayari mpaka upande wa wasimamizi.... kufanyika mwakani inamaanisha mtu aanze kwenye foleni ya mtaa ndio aende kwenye uchaguzi wa rais....

Pia uchaguzi mkuu unafanyika kwenye vituo tofauti na za mtaa, kuunganisha yote haya kkuwa za mtaa na rais huu ni mtiti mwingine, yaani itakuwa vurugu mechi
 
Nchi hii tusipochapana na kuuwana, kamwe ccm haitaondoka madarakani
 
OR TAMISEMI mnazingua, kuna watu hatuna NIDA wala kitambulisho cha kupiga kura, ni vile tumehamasika kushiriki kwenye uchaguzi huu... nimekuja kujiandikisha nikaambiwa naweza kushiriki bila kuwa na kitambulisho, mtawezaje kunizuia kushiriki kwenye kupiga kura na vitambulisho sina?

Mnasubiri mpaka mtu atilie shaka😹😹🤣 kwahiyo mtu asipotiliwa shaka mambo yanaenda bila shida.

Yaani mmeweka matobo makusudi halafu mmeangusha mzigo kwa wananchi ili mjivue lawama
 
Kama takwimu siyo siri kwanini hakuna takwimu za kata na mitaa? Kwanini takwimu hizo zipo kimkoa? Hamuoni mmeweka tobo la takwimu kupikwa?
 
Alipataje za Mkoa akashindwa kupata za kata?
Hapa sasa, kwanini wakatae kutupa takwimu za za ngazi hii ya chini halafu watupe kiujumla hivyo, kuna namna... inamaana sasa hivi mtu akitaka kupata takwimu za kidondoni pekee, au ubungo pekee, hazipo
 
Nadhani orodha ya Wapiga Kura itabandikwa vituoni kabla ya Uchaguzi 🐼
 
Zoezi la Uandikishaji Wananchi watakaoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 limekamilika ambapo kwa mujibu wa TAMISEMI, takriban Watu Milioni 32.9 (94%) wamejiandikisha

Kwako Mdau, una mtazamo gani kuhusu zoezi hilo lilivyoendeshwa ikiwa ni takriban mwezi mmoja umesalia kuelekea siku ya Kupiga Kura?

Ungana nasi leo Oktoba 31, 2024 Saa 12:00 Jioni kupitia XSpaces ya JamiiForums ambapo tutapokea maoni ya Wananchi katika Mjadala utakaoangazia Mchakato Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Mwongoza mjadala: Chief Edwin Odemba - Mwandishi wa Habari/Mtangazaji

WAZUNGUMZAJI
1. Idd Mkanza - Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF
2. Jebra Kambole - Wakili wa Kujitegemea
3. Askofu Maximillian Machumu - CHADEMA
4. Mbarala Maharagande - Katibu wa Haki za Binadamu ACT Wazalendo
5. Bob Chacha Wangwe - Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)

Kushiriki mjadala Ingia x.com

IDD MKANZA (Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF):

Mchakato wa Uandikishaji haukwenda vizuri, sisi CUF tumezungumza kuwa hakuna dhamira njema, mfano kule Newala kuna Viongozi wetu walikamatwa na kumekuwa na changamoto inayowahusu Wapigakura

Handeni, Tanga kulikuwa na kupishana kwa idadi ya Wapigakura waliojiandikisha na wale ambao majina yao yalibandikwa, ilikuwa hivyo pia hata Bagamoyo (Pwani)

Ukitazama takwimu za Wapiga Kura zilizotolewa na TAMISEMI na zile Takwimu za Sensa 2022 zinapishana, mbali na hapo kuna Mawakala ambao wamekuwa wakizuiwa kusaini licha ya kuwa Kanuni inaelekeza hivyo, kuwa wanatakiwa kusaini muda wa kufungwa kwa uandikishaji

Kuna Wasimamizi wa Uchaguzi walikuwa wanapokea majina kwenye simu wengine walikuwa wanakwenda nyumbani kuwafuata Watu, hayo yote yanaonesha zoezi la Uandikishaji liliharibika

Ishara ya kilichotokea katika Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura ni mbaya. Nikumbushe jambo, Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Watu kujiandikisha tofauti na ilivyo Mwaka huu (2024)

Mwaka huu (2024) vituo vingi vimekuwa vikavu, hakuna Watu lakini baadaye kwenye orodha ya majina inaonekana majina ni mengi, yametoka wapi? Inamaanisha kuna Watendaji waliofanya kinyume cha taratibu kwa kuandikisha Watu ambao hawakidhi vigezo

Mazingira ya Uandikishaji yanaonesha hakukuwa na uhalisia kulikuwa na Watu wengi wasio na sifa wakiwemo wenye umri chini ya Miaka 18, mwamko pia ulikuwa upo chini

Newala Vijijini (Mtwara), nusu ya Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwepo kwenye Vituo vyao

Tulipokuwa tunaulizia Viongozi wao wa juu wakisema wengine wapo katika majukumu mengine lakini ilionekana wazi kuwa Watu hawakuwa na hamu ya kupiga kura

Rais ameleta 4R lakini utendaji wa Watendaji wake hauendani na anachokitaka Rais

Kuna sehemu nilizungumza na Mkurugenzi (siwezi kutaja sehemu) alikuwa hafurahishwi na baadhi ya mambo, nadhani hizi 4R za Rais ambazo amezihutubia akiwa na dhamira ya dhati ikiwezekana kuwe na maelezo ya nini hasa ambacho anakitaka kiongozi wa Nchi

Kuna Watu wa huku chini ndio ambao wameharibu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mfano kule Mbeya Viongozi wetu waliambiwa wato ‘copy’, hilo ni jambo dogo lakini linaonesha jinsi ambavyo vitu vingi havipo sawa

WILLIAM (Mdau):

Takwimu zilizotolewa na TAMISEMI zinaonesha kuna ongezeko la Wapigakura waliojiandikisha, ni jambo zuri lakini tunatakiwa kuwa na takwimu sahihi

Muhimu zaidi tunachotakiwa kufanyika ni kuwapa elimu Wananchi ili waweze kushiriki kwa kuwa wao ndio wanaofanya maamuzi kupitia Kura wanazopiga

Licha ya upungufu uliojitokeza kwenye mchakato wa Uandikishaji bado tunatakiwa kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza na kufanya maamuzi kupitia Kura

Askofu Maximillian Machumu (CHADEMA)

Uandikishaji ulivyoanza sisi kama Chama tulipinga ikiwemo kufanya maandamano Nchi nzima, lengo lilikuwa ni kutaka TAMISEMI wasisimamie uchaguzi huo kwa kuwa kusingekuwa na Haki

Baada ya yote yaliyotokea tukakubaliana kuwa hatuwezi kususia kushiriki kwa kuwa kwa Katiba hii na TAMISEMI hii tuliwahi kushinda katika chaguzi zilizopita

Tumeshuhudia Daftari la Kupiga Kura limekuwa na mizengwe mingi ambayo inaonesha Uchaguzi hautakuwa salama

Jambo zuri katika maandalizi haya ni kuwa wametangaza na kuweka mabango sehemu nyingi kama Kanuni zinavyoelekeza lakini wanachokiuka ni kuandikisha Watu wasio na vigezo vya kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kuna watu wamejiandikisha zaidi ya mara moja kwa kuwa Daftari lilikuwa halina nafasi ya kuonesha huwezi kujiandikisha katika zaidi ya Kituo kimoja

Kuna Kituo waliandikisha Watu zaidi ya 200 lakini majina yaliyoandikishwa yalikuwa zaidi ya 600 hadi Watu wa Mtaa husika wanajiuliza hao watu wengine wametoka wapi

Kuna sehemu walikuwa wanachukua daftari la majina ya Wanafunzi na kwenda kuhamisha kwenye Daftari la Kupiga Kura

ISIHAKA MCHINJITA (Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo - Bara)

Kuna matukio ambayo sio ya bahati mbaya kwenye Uandikishaji na hatukuona kama TAMISEMI wakionesha mwitikio, kitu ambacho kinaonesha hawana dhamira ya kweli

Kuna maeneo ambayo Msimamizi ameandikisha Mtu ambaye amefariki na Msimamizi Msaidizi akakiri, unajiuliza hilo jina liliandikishwaje?

Inawezekana Waandikishaji walikuwa wanaorodhesha tu Watu, hali kama hiyo ndio iliyotufanya kuaminia TAMISEMI sio sehemu sahihi au Watu sahihi wa kusimamia zoezi hilo la Uandikishaji wa Daftari la kupiga Kura Serikali za Mtaa

Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Kisiasa, Haki za Kidemokrasia zilikuwa zinapatikana kuliko ilivyo leo, hakukuwa na vitisho kwa Watu, mambo ya Watu wasiojulikana hayakuwepo

Hivyo, kusema leo watu wanamwamko mkubwa wa kujiandikisha ni kujidanganya

TAMISEMI haina uwezo wa kusimamia uchaguzi huu kwa kuwa wanaonesha wana upande mmoja

Jambo lingine kuna upungufu wa makosa ya kudhamiria na sio ya Kibinadamu, mfano Newala kuna Watendaji wanaosimamia hawakuwepo vituoni, mwingine walimkuta Msimamizi akasema subiri narudi, baada ya hapo hakurudi tena na simu hapokei

Mahakama kuipa TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kukatisha tamaa Demokrasia

Ujio wa Tume Huru ya Uchaguzi ilimaanisha lazima kuwe na chombo huru cha kusimamia uchaguzi, hivyo kilichofanywa na Mahakama ni sawa na kupiga rungu Demokrasia na tunaingia kwenye wakati mgumu sana, tunalazimika kuongea na TAMISEMI kuhusu matatizo ambayo tuliyatabiri yatatokea

NTEGHENJWA HOSSEAH (TAMISEMI):

Tumepokea maoni na ushauri wa Wadau, huko siku za nyuma Uchaguzi ulikuwa unafanyika lakini Uandikishaji ulikuwa chini, mfano Mwaka 2014 waliijiandikisha walikuwa Milioni 11, Mwaka 2019 waliojiandikisha walikuwa wengi hadi siku zikaongezwa baada ya ile za awali kukamilika

TAMISEMI haiwezi kuwa na takwimu ambazo sio sahihi, kwa namna ambavyo ofisi hii ina majukumu makubwa haiwezi kutengeneza takwimu

Takwimu ambazo zinapatikana TAMISEMI ndio zile ambazo zinapatika katika Mamlaka nyingine za Takwimu za Serikali

Kuhusu madai kuwa kuna Watu wameandikishwa wasiokuwa na sifa, Kanuni zipo wazi kuwa kuna muda wa mapingamizi baada ya mchakato wa Uandikishwaji wa Wapiga Kura ambapo wanaweza kuwasilisha vielelezo vyao kwa ajili ya kuweka pingamizi

TAMISEMI: Kuhusu suala la TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuwa Sheria inatupa mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo

Wadau wanatoa maoni na wanaendelea kutoa mapendekezo yao, inawezekana miaka ijayo mambo yanaweza kubadilika lakini kwa sasa hatuwezi kusema tusisimamie wakati Sheria na Kanuni zinatutaka kusimamia Uchaguzi

Jukumu la kusimamia Uchaguzi sio kwamba tunajipa wenyewe bali ni miongozo iliyopo kwenye Sheria

Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa unafanywa katika levo ya chini ya Mamlaka ya Serikali za Mtaa, kwenye Mitaa na Vijiji vingi tunavyoishi tunafahamiana

Inapotokea mtu ana shaka ndipo linapokuja suala la kitambulisho ambalo linatakiwa kuendana na lile lililoandikwa

Kuhusu kufuata Waandikishaji nyumbani wahusika waliafikiana kufanya hivyo baada ya majadiliano lakini baada ya malalamiko na maoni ya Wadau hilo likafanyiwa kazi na ikaelekezwa wanaotakiwa kujiandikisha waende kwenye vituo na sio kuwafuata

Jina na utambulisho wa Mpiga Kura linapotiliwa shaka wakati wa Uandikishaji, Msimamizi anayo nafasi ya kutumia nafasi yake kuhitaji utambulisho wa Mhusika kwa maana ya vitambulisho ambavyo vinatakiwa kuendana na majina na utambulisho wake alioandika kwenye daftari

Wanaolalamika kuhusu Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura Serikali za Mitaa ni wachache na wanajulikana wanatokea upande gani lakini haina maana maoni na mapendekezo yanayotolewa tunayachukulia poa, tunayazingatia na ndio maana baadhi yanafanyiwa kazi

Maoni ya kuwa Uandikishaji unatakiwa kuhamia Kidigitali tunaupokea, inawezekana Chaguzi zinazofuata tunaweza kuhamia huko kwa kuwa tunaweza kuwa katika nafasi nzuri ya Teknolojia zaidi

SHANGWE AYO (Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT):

Mchakato huu wa uchaguzi hautoi njia ya kuwa kuna uhuru na haki, kuna matikio mengi ambayo yanafanyika ndivyo sivyo, kuna baadhi ya Shule zimetumia daftari la mahudhurio kwa ajili ya kuandikisha majina

ACT tutashiriki Uchaguzi lakini kuna makandokando mengi, TAMISEMI haikuwa na uhalali wa kushiriki kusimamia Uchaguzi huu

Mimi nipo Arumeru Mashariki huku kwetu fomu zinatolewa kwa kutoa ‘copy’, kuna baadhi ya Watendaji wanatueleza kuwa kama Wapinzani wakionekana kutawala Jimbo tunaweza kukosa misaada na vitu kama hivyo

ACT Wazalendo tumejiandaa kutoa Wagombea kila Kijiji na kila eneo katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa japokuwa kuna viashiria kuwa kuna chama fulani kimeandaliwa kushinda

Safari hii hatutakuwa lelemama kama ilivyokuwa siku za nyuma

SHASHI JOHN: MDAU

Zoezi la Uandikishaji liliwa la wazi, majina yamebandikwa na kila kitu kipo wazi, kitu kizuri ni kuwa mchakato ulifanyika kwa ngazi ya Kitongoji ambacho Wananchi wanajuana

Waliokuwa na pingamizi walikuwa na nafasi ya kuweka mapingamizi, kila kitu kilikuwa kinaonekana kwa uwazi japokuwa watu wengi wanazungumza wakiegemea upande mmoja
zeozi la uandikishaji wapiga kura kwajili ya serikali za mitaa likwenda vizuri mno licha ya changamoto ndogo ndogo kadhaa ambazo ni pamoja na baadhi ya wapinzani kupuuzia zoezi hilo na baada ya watu wengi zaidi kuhamasika kujiandikisha tofauti na matarajio yao, eti wanajitokeza na kupinga idadi ya waliojiandikisha ili hali wao ni kama walipuuza na wakasusia.

Matarajio yangu kama kiongozi wa wananchi, kwanza ni kuhamasisha wale wote waliojiandikisha wajitokeze kwenye kampeni kuskiza wagombea wao na hatimae wajitokeze kwa wingi kwenye uchaguzi huo muhimu wa kihistoria humu nchini kuamua hatimae ya uongozi wa maeneo yao.

Ni wazi uchaguzi utakua wa Amani na utulivu sana. Na zaidi sana utakua uchaguzi huru, wa haki na wa wazi mno. Fujo na vurugu hususani za ambao hawajajiandikisha halafu wanadai ushindi, hazitavumiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama ili hatimae wananchi waamue hatma yao katika hali ya amani.

Hakipo cha cha maana kuzuia uchaguzi huo muhimu kufanyika tar 27 Nov 2024.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
sio lazima kuona naweza kutazama pia na ikatosha.

Infact,
vyovyote itakavyokua, uchaguzi muhimu na w kihistoria wa serikali za mitaa na vijiji nchini mpaka sasa hakuna mabadiliko yoyote. Wananchi walihamasika kwa mamilioni yao ni wazi watajitokeza kwenye kampeni na uchaguzi wenyewe kwa idadi sawa na waliojiandikisha.

uhuru na usawa wa majadliano ni haki ya mTanzania kuelekea uchaguzi huo, lakini kamwe dosari na kasoro ndogo ndogo kwenye zoezi la uandikishaji wapiga kura haliwezi kuzuia hatua nyingine za uchaguzi huo kuendelea.

kumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa ni November 27, 2024. Chagueni viongozi makini wa CCM waliojiandikisha tu 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Zoezi la Uandikishaji Wananchi watakaoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 limekamilika ambapo kwa mujibu wa TAMISEMI, takriban Watu Milioni 32.9 (94%) wamejiandikisha

Kwako Mdau, una mtazamo gani kuhusu zoezi hilo lilivyoendeshwa ikiwa ni takriban mwezi mmoja umesalia kuelekea siku ya Kupiga Kura?

Ungana nasi leo Oktoba 31, 2024 Saa 12:00 Jioni kupitia XSpaces ya JamiiForums ambapo tutapokea maoni ya Wananchi katika Mjadala utakaoangazia Mchakato Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Mwongoza mjadala: Chief Edwin Odemba - Mwandishi wa Habari/Mtangazaji

WAZUNGUMZAJI
1. Idd Mkanza - Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF
2. Jebra Kambole - Wakili wa Kujitegemea
3. Askofu Maximillian Machumu - CHADEMA
4. Mbarala Maharagande - Katibu wa Haki za Binadamu ACT Wazalendo
5. Bob Chacha Wangwe - Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)

Kushiriki mjadala Ingia x.com

IDD MKANZA (Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF):

Mchakato wa Uandikishaji haukwenda vizuri, sisi CUF tumezungumza kuwa hakuna dhamira njema, mfano kule Newala kuna Viongozi wetu walikamatwa na kumekuwa na changamoto inayowahusu Wapigakura

Handeni, Tanga kulikuwa na kupishana kwa idadi ya Wapigakura waliojiandikisha na wale ambao majina yao yalibandikwa, ilikuwa hivyo pia hata Bagamoyo (Pwani)

Ukitazama takwimu za Wapiga Kura zilizotolewa na TAMISEMI na zile Takwimu za Sensa 2022 zinapishana, mbali na hapo kuna Mawakala ambao wamekuwa wakizuiwa kusaini licha ya kuwa Kanuni inaelekeza hivyo, kuwa wanatakiwa kusaini muda wa kufungwa kwa uandikishaji

Kuna Wasimamizi wa Uchaguzi walikuwa wanapokea majina kwenye simu wengine walikuwa wanakwenda nyumbani kuwafuata Watu, hayo yote yanaonesha zoezi la Uandikishaji liliharibika

Ishara ya kilichotokea katika Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura ni mbaya. Nikumbushe jambo, Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Watu kujiandikisha tofauti na ilivyo Mwaka huu (2024)

Mwaka huu (2024) vituo vingi vimekuwa vikavu, hakuna Watu lakini baadaye kwenye orodha ya majina inaonekana majina ni mengi, yametoka wapi? Inamaanisha kuna Watendaji waliofanya kinyume cha taratibu kwa kuandikisha Watu ambao hawakidhi vigezo

Mazingira ya Uandikishaji yanaonesha hakukuwa na uhalisia kulikuwa na Watu wengi wasio na sifa wakiwemo wenye umri chini ya Miaka 18, mwamko pia ulikuwa upo chini

Newala Vijijini (Mtwara), nusu ya Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwepo kwenye Vituo vyao

Tulipokuwa tunaulizia Viongozi wao wa juu wakisema wengine wapo katika majukumu mengine lakini ilionekana wazi kuwa Watu hawakuwa na hamu ya kupiga kura

Rais ameleta 4R lakini utendaji wa Watendaji wake hauendani na anachokitaka Rais

Kuna sehemu nilizungumza na Mkurugenzi (siwezi kutaja sehemu) alikuwa hafurahishwi na baadhi ya mambo, nadhani hizi 4R za Rais ambazo amezihutubia akiwa na dhamira ya dhati ikiwezekana kuwe na maelezo ya nini hasa ambacho anakitaka kiongozi wa Nchi

Kuna Watu wa huku chini ndio ambao wameharibu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mfano kule Mbeya Viongozi wetu waliambiwa wato ‘copy’, hilo ni jambo dogo lakini linaonesha jinsi ambavyo vitu vingi havipo sawa

WILLIAM (Mdau):

Takwimu zilizotolewa na TAMISEMI zinaonesha kuna ongezeko la Wapigakura waliojiandikisha, ni jambo zuri lakini tunatakiwa kuwa na takwimu sahihi

Muhimu zaidi tunachotakiwa kufanyika ni kuwapa elimu Wananchi ili waweze kushiriki kwa kuwa wao ndio wanaofanya maamuzi kupitia Kura wanazopiga

Licha ya upungufu uliojitokeza kwenye mchakato wa Uandikishaji bado tunatakiwa kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza na kufanya maamuzi kupitia Kura

Askofu Maximillian Machumu (CHADEMA)

Uandikishaji ulivyoanza sisi kama Chama tulipinga ikiwemo kufanya maandamano Nchi nzima, lengo lilikuwa ni kutaka TAMISEMI wasisimamie uchaguzi huo kwa kuwa kusingekuwa na Haki

Baada ya yote yaliyotokea tukakubaliana kuwa hatuwezi kususia kushiriki kwa kuwa kwa Katiba hii na TAMISEMI hii tuliwahi kushinda katika chaguzi zilizopita

Tumeshuhudia Daftari la Kupiga Kura limekuwa na mizengwe mingi ambayo inaonesha Uchaguzi hautakuwa salama

Jambo zuri katika maandalizi haya ni kuwa wametangaza na kuweka mabango sehemu nyingi kama Kanuni zinavyoelekeza lakini wanachokiuka ni kuandikisha Watu wasio na vigezo vya kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kuna watu wamejiandikisha zaidi ya mara moja kwa kuwa Daftari lilikuwa halina nafasi ya kuonesha huwezi kujiandikisha katika zaidi ya Kituo kimoja

Kuna Kituo waliandikisha Watu zaidi ya 200 lakini majina yaliyoandikishwa yalikuwa zaidi ya 600 hadi Watu wa Mtaa husika wanajiuliza hao watu wengine wametoka wapi

Kuna sehemu walikuwa wanachukua daftari la majina ya Wanafunzi na kwenda kuhamisha kwenye Daftari la Kupiga Kura

ISIHAKA MCHINJITA (Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo - Bara)

Kuna matukio ambayo sio ya bahati mbaya kwenye Uandikishaji na hatukuona kama TAMISEMI wakionesha mwitikio, kitu ambacho kinaonesha hawana dhamira ya kweli

Kuna maeneo ambayo Msimamizi ameandikisha Mtu ambaye amefariki na Msimamizi Msaidizi akakiri, unajiuliza hilo jina liliandikishwaje?

Inawezekana Waandikishaji walikuwa wanaorodhesha tu Watu, hali kama hiyo ndio iliyotufanya kuaminia TAMISEMI sio sehemu sahihi au Watu sahihi wa kusimamia zoezi hilo la Uandikishaji wa Daftari la kupiga Kura Serikali za Mtaa

Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Kisiasa, Haki za Kidemokrasia zilikuwa zinapatikana kuliko ilivyo leo, hakukuwa na vitisho kwa Watu, mambo ya Watu wasiojulikana hayakuwepo

Hivyo, kusema leo watu wanamwamko mkubwa wa kujiandikisha ni kujidanganya

TAMISEMI haina uwezo wa kusimamia uchaguzi huu kwa kuwa wanaonesha wana upande mmoja

Jambo lingine kuna upungufu wa makosa ya kudhamiria na sio ya Kibinadamu, mfano Newala kuna Watendaji wanaosimamia hawakuwepo vituoni, mwingine walimkuta Msimamizi akasema subiri narudi, baada ya hapo hakurudi tena na simu hapokei

Mahakama kuipa TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kukatisha tamaa Demokrasia

Ujio wa Tume Huru ya Uchaguzi ilimaanisha lazima kuwe na chombo huru cha kusimamia uchaguzi, hivyo kilichofanywa na Mahakama ni sawa na kupiga rungu Demokrasia na tunaingia kwenye wakati mgumu sana, tunalazimika kuongea na TAMISEMI kuhusu matatizo ambayo tuliyatabiri yatatokea

NTEGHENJWA HOSSEAH (TAMISEMI):

Tumepokea maoni na ushauri wa Wadau, huko siku za nyuma Uchaguzi ulikuwa unafanyika lakini Uandikishaji ulikuwa chini, mfano Mwaka 2014 waliijiandikisha walikuwa Milioni 11, Mwaka 2019 waliojiandikisha walikuwa wengi hadi siku zikaongezwa baada ya ile za awali kukamilika

TAMISEMI haiwezi kuwa na takwimu ambazo sio sahihi, kwa namna ambavyo ofisi hii ina majukumu makubwa haiwezi kutengeneza takwimu

Takwimu ambazo zinapatikana TAMISEMI ndio zile ambazo zinapatika katika Mamlaka nyingine za Takwimu za Serikali

Kuhusu madai kuwa kuna Watu wameandikishwa wasiokuwa na sifa, Kanuni zipo wazi kuwa kuna muda wa mapingamizi baada ya mchakato wa Uandikishwaji wa Wapiga Kura ambapo wanaweza kuwasilisha vielelezo vyao kwa ajili ya kuweka pingamizi

TAMISEMI: Kuhusu suala la TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuwa Sheria inatupa mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo

Wadau wanatoa maoni na wanaendelea kutoa mapendekezo yao, inawezekana miaka ijayo mambo yanaweza kubadilika lakini kwa sasa hatuwezi kusema tusisimamie wakati Sheria na Kanuni zinatutaka kusimamia Uchaguzi

Jukumu la kusimamia Uchaguzi sio kwamba tunajipa wenyewe bali ni miongozo iliyopo kwenye Sheria

Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa unafanywa katika levo ya chini ya Mamlaka ya Serikali za Mtaa, kwenye Mitaa na Vijiji vingi tunavyoishi tunafahamiana

Inapotokea mtu ana shaka ndipo linapokuja suala la kitambulisho ambalo linatakiwa kuendana na lile lililoandikwa

Kuhusu kufuata Waandikishaji nyumbani wahusika waliafikiana kufanya hivyo baada ya majadiliano lakini baada ya malalamiko na maoni ya Wadau hilo likafanyiwa kazi na ikaelekezwa wanaotakiwa kujiandikisha waende kwenye vituo na sio kuwafuata

Jina na utambulisho wa Mpiga Kura linapotiliwa shaka wakati wa Uandikishaji, Msimamizi anayo nafasi ya kutumia nafasi yake kuhitaji utambulisho wa Mhusika kwa maana ya vitambulisho ambavyo vinatakiwa kuendana na majina na utambulisho wake alioandika kwenye daftari

Wanaolalamika kuhusu Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura Serikali za Mitaa ni wachache na wanajulikana wanatokea upande gani lakini haina maana maoni na mapendekezo yanayotolewa tunayachukulia poa, tunayazingatia na ndio maana baadhi yanafanyiwa kazi

Maoni ya kuwa Uandikishaji unatakiwa kuhamia Kidigitali tunaupokea, inawezekana Chaguzi zinazofuata tunaweza kuhamia huko kwa kuwa tunaweza kuwa katika nafasi nzuri ya Teknolojia zaidi

SHANGWE AYO (Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT):

Mchakato huu wa uchaguzi hautoi njia ya kuwa kuna uhuru na haki, kuna matikio mengi ambayo yanafanyika ndivyo sivyo, kuna baadhi ya Shule zimetumia daftari la mahudhurio kwa ajili ya kuandikisha majina

ACT tutashiriki Uchaguzi lakini kuna makandokando mengi, TAMISEMI haikuwa na uhalali wa kushiriki kusimamia Uchaguzi huu

Mimi nipo Arumeru Mashariki huku kwetu fomu zinatolewa kwa kutoa ‘copy’, kuna baadhi ya Watendaji wanatueleza kuwa kama Wapinzani wakionekana kutawala Jimbo tunaweza kukosa misaada na vitu kama hivyo

ACT Wazalendo tumejiandaa kutoa Wagombea kila Kijiji na kila eneo katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa japokuwa kuna viashiria kuwa kuna chama fulani kimeandaliwa kushinda

Safari hii hatutakuwa lelemama kama ilivyokuwa siku za nyuma

SHASHI JOHN: MDAU

Zoezi la Uandikishaji liliwa la wazi, majina yamebandikwa na kila kitu kipo wazi, kitu kizuri ni kuwa mchakato ulifanyika kwa ngazi ya Kitongoji ambacho Wananchi wanajuana

Waliokuwa na pingamizi walikuwa na nafasi ya kuweka mapingamizi, kila kitu kilikuwa kinaonekana kwa uwazi japokuwa watu wengi wanazungumza wakiegemea upande mmoja
 
Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom