kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Nimejaribu kupitia maudhui ya kazi ya kijana Erick kujua kama anahusiana na timu ya wazee iliyotingisha chama juzi Kati na kubaini kuwa mtajwa Kuna viashiria kwamba alifanya kazi na chama Tena kwa uhaminifu 2015.
Labda yawezekana baada ya hapo aliamia kufanya shughuli zake binafsi na mashirika mengine na kwa kuwa ana malengo na utashi na anategemeo flani kwa kesho akaona aingie kwenye habari za kiuchunguzi ambazo tawala za kiafrika nyingi hazitaki kuzisikia.
Yawezekana pia kwa kufanya kazi nzuri anatakiwa kurejea kwenye kazi alizofanya na akina Makamba 2020 ila yupo busy na pia yawezekana yeye mchezo huu anaujua vyema.
Tatizo la waandishi wetu Ni kwamba ikifika kipindi Cha uchaguzi wanakuwa na uandishi wa kikampeni na pale kampeni zinapoisha Mambo yakabadilika wanarudia professional yao.
Waangalie pia wasanii wa muziki na filamu wanavyotumika, Ni vigumu leo wengi wao kuaminika kwa sababu wanakula na kunywa na wanasiasa wakati wa kampeni lakini ikifika wakati wa Raha ( baada ya uchaguzi) wanasiasa wanawatumia watakavyo.
Tujaribu kuwashauri vijana wenye upeo na maono ya mbali kukaa mbali na fadhila, vujeni jasho usiku na mchana kutengeneza kesho yenu bila kujiegemeza kwa wanasiasa.
Mwisho nitoe pole kwa Bw.Erick na MWENYENZI MUNGU amtangulie amalize salama changamoto anazopitia na kurejea kwenye majukumu yake.