Joseph Brighton Malekela
Member
- Jun 7, 2017
- 9
- 3
Nimejaribu kujielimisha kidogo kama kuna ugumu wowote kwa wahitimu wa elimu ya juu kujiajiri. Nimejifunza kwamba, vikwazo vikubwa kwa wahitimu kuhusu kujiajiri ni mfumo wa elimu kutokuwajengea tabia ya kujiajili, pamoja na changamoto ya kupata mitaji ya kujiajiri.
Wahitimu wa elimu ya juu wanatumia zaidi ya muongo mmoja na nusu darasani, na kwa wakati wote huo, mfumo uliopo hauwaandai kujiajiri. Kwa mfano, vyuo vingi vikubwa nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma vina kozi ambazo wanafunzi wote lazima wazisome, ikiwemo Maarifa ya Mawasiliano, Fikra Yakinifu na Somo la Maendeleo.
Licha ya uhalisia kwamba, kujiajiri ni suluhisho la changamoto ya ajira nchini na duniani kote, kozi ya ujasiliamali katika vyuo hivyo na vingine vingi inafundishwa kwa wanafunzi wachache tu ama kwa wale wanaosomea masomo ya biashara au kupitia semina za kujiajiri ambazo mara nyingi haziwafikii wanafunzi wote. Linapokuja suala la kutakiwa kujiajiri, hilo halichagui ulijifunza au haukujifunza.
Kuhusu mazingira yasiyo rafiki ya kupata mitaji kwaajili ya kujiajiri, kwa sasa, mhitimu anaweza kupata mtaji ama kutoka katika Taasisi za fedha au katika mifuko ya uwezeshaji wa vijana inayoanzishwa na serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (YDF) na zile zinazotolewa kutoka kwenye 4% ya makusanyo ya Halmashauri. Fursa ya kupata mikopo ya mitaji kutoka benki ina changamoto nyingi sana ikiwemo masharti magumu ya kuwa na dhamana ya hati ya mali isiyohamishika kama vile nyumba, kiwanja au gari, vitu ambavyo mhitimu huenda asiwe navyo.
Changamoto ya kupata mikopo ya serikali hasa kupitia fedha za Halmashauri inatokana na masharti magumu ambayo hayamruhusu mtu mmoja mmoja kupata mkopo na pia, hata akitimiza matakwa ya kuwa kwenye kikundi cha kuanzia watu watano, wanatakiwa kuwa na biashara ambayo tayari wamekwisha kuanza pamoja na mpango wa biashara unaoonesha rekodi ya mapato ya awali na namna watakavyotumia fedha wanazoomba. Fursa ya pili ndio pengine ingekuwa kimbilio jepesi, lakini bado changamoto ipo katika kuifikia hiyo mikopo na huenda wahitimu wengi wa elimu ya juu hawaoni nafasi yao katika fedha hizo.
Ili kutatua kitendawili cha wahitimu na kujiajiri, tufanye yafuatayo;
Elimu ya kujiajiri/ujasiriamali itolewe kwa Wanafunzi wa Ngazi zote Nchini. Ninaamini kwamba, kujiajiri kunajengwa na tabia ya ujasiriamali, ambayo mtu anapaswa kuwa nayo, na tabia ni kitu kinachojengwa kwa muda mrefu sana. Katika suala la kujenga tabia ya ujasiliamali, tunaweza kuanzia na elimu msingi, kwa kurejelea mitaala na kurudisha au kuweka somo au vitu fulani ndani ya masomo yaliyopo ambavyo vitajenga tabia ya ujasiliamali au kujiajiri.
Katika somo hili, mwanafunzi aanze kujifunza kutokana na daraja lake la elimu nini maana ya kujiajiri au ujasiliamali. Endapo mtaala utatengenezwa vizuri, somo hili lizidi kupanua wigo wa ufahamu wa suala la ujasiliamali katika kila sekta kutoka darasa moja kwenda darasa la hatua nyingine hadi kufikia elimu ya juu. Ninaamini kwa kufanya hivi, mwanafunzi atakuwa atajifunza vitu vingi, na hata kwa wale ambao hawapati fursa ya kuendelea na elimu ya juu kutokana na ufaulu, basi na wao watakuwa wameambulia kitu cha kwenda kuanzia kujiajiri kulingana na elimu ya kujiajiri waliyoipata kuanzia darasa la kwanza hadi kufikia kiwango cha elimu wanachoishia.
Uanzishwe Mfuko wa Kuwawezesha Wahitimu Kiuchumi (Graduates Economic Empowerment Fund - GEEF). Pendekezo hili lina lenga kuhakikisha kwamba, wahitimu angalau wa ngazi ya shahada wanapata mikopo ya mitaji mara tu baada ya kumaliza masomo yao, ili kwa kutumia elimu waliyoipata ya kujiajiri/ujasiliamali tangu waanze masomo yao na kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha ambacho mfuko huo utawawezesha, basi wakawe na sehemu ya kuanzia katika kujitegemea na kujiajiri huko mtaani. Kwa maoni yangu, nadhani, kiasi kisichopungua Tsh. 1,000,000/= kinaweza kusaidia kumuwezesha mhitimu kuanza kujiajiri.
Zipo namna nyingi zinaweza kuuwezesha mfuko wa GEEF kupata fedha za kuwakopesha mitaji ya kujiajiri wahitimu wa elimu ya juu. Hii ni pamoja na;
Kupitia fedha za wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu - HESLB. Serikali inaweza kukata shilingi 1,500 kutoka kwenye shilingi 8,500 anazopewa mwanafunzi kwaajili ya kula na malazi, na fedha hiyo ikawekwa kwenye mfuko wa GEEF. Au, ikionekana kupunguza kutamuumiza mwanafunzi, serikali inaweza kuongeza shilingi 1,500/= katika fedha anayopewa hivi sasa mwanafunzi kwa siku (iongezeke kutoka 8,500/= hadi 10,000/=) na kiasi kilichozidi (1,500/=) kikawekwa kwenye mfuko wa GEEF. Vyevyote itakavyokuwa, iwe ni kwa kupunguza kiasi cha fedha anachopokea sasa au kwa kuongeza kiasi kilichopendekezwa, namna hii ni rahisi zaidi na yenye uhakika wa kusaidia wahitimu wengi kwa mara moja kupata mitaji ya kuanzia.
Kwa mfano, mfumo huu ungeanza kutumika kwa wanufaika wa mwaka wa kwanza 65,00 waliopata mikopo ya HESLB mwaka wa masomo 2021/2022, baada ya miaka mitatu, kungekuwa na kundi kubwa la wahitimu ambao wangekuwa na uhakika wa kupata mtaji wa kuanzia usiopungua Shilingi 1,080,000/=. Muhimu kuzingatia, pendekezo hili linatekelezeka endapo tu litaanza kwa wanufaika wapya tangu wanapoanza mwaka wa kwanza. Jambo hili si geni na ni sawa tu na kinachofanyika kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSSF kwa kukata sehemu ya mapato ya mishahara ya watumishi.
Kupitia 1% ya Mapato ya Halmashauri: Kwa lengo la kuwawezesha wahitimu kujikwamua na tatizo la pili la kujiajiri ambalo ni mitaji, basi ikiwezekana, asilimia 1% tu kati ya 4% za mapato ya halmashauri ambazo hutengwa kwaajili ya vijana, zipelekwe kwenye mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji wahitimu kiuchumi GEEF. Hii itasaidia kuongeza uwezo wa mfuko huo kuwawezesha wahitimu wengi zaidi kiuchumi mara tu baada ya kuhitimu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ya Robo mwaka ya makusanyo ya halmashauri nchini kwa mwaka 2021, jumla ya makadirio ya mapato ambayo halmashauri zote nchini zilijiwekea ni Shilingi Bilioni 863.9.
Hii inamaanisha kuwa, kwa pendekezo langu katika eneo hili, asilimia 1% ya mapato yote ya halmashauri iende kwenye mfuko wa kuwezesha wahitimu kiuchumi. Hii ni sawa na Shilingi Bilioni 8.6 (kwa kutumia akisi ya makusanyo tajwa). Fedha hiyo pekeyake, inaweza kuwawezesha wahitimu 8,600 kwa mgawanyo wa shilingi 1,000,000/= kwa kila mhitimu, na sio kwa kikundi.
Mwisho, Kabla ya kuwalaumu wahitimu wa elimu ya juu kwanini hawajiajiri, tuwawezeshe kutatua kitendawili cha kujiajiri kwa kuwapa elimu ya kujiajiri na kuondoa vikwazo vya kupata mitaji ya kujiajiri.

Upvote
10