Ubabaishaji Urambo

Ubabaishaji Urambo

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Posts
2,146
Reaction score
886
Tamisemi Wamulike ubabaishaji mkubwa unaofanywa na watendaji idara ya elimu upande wa Sekondari wilayani Urambo, Walimu wa sekondari Urambo hawapandishwi madaraja, toka walioajiriwa mwaka 2004 hadi leo 2011 wapo wengi tu hawajapandishwa madaraja, watendaji wa elimu kazi yao ni vikao, semina, na safari zisizokwisha, Afisa Elimu wa wilaya anayeitwa Mzungu huyu jamaa anadharau sana walimu, ana lugha chafu sana, amesababisha walimu walioenda kusoma kutorudi Urambo baada ya kuhitimu masomo kwa sababu ni mnyanyasaji sana, hivyo Mheshimiwa Sitta fuatilia jimbo lako hali ni mbaya sana, ama sivyo walimu wa sekondari walio masomoni hawatarudi kufanya kazi jimboni kwako, ufisadi unatisha halmashauri ya Urambo upande wa Elimu Sekondari, nawasilisha waungwana.
 
Back
Top Bottom