Ubabe wa Tanzania: Meli kubwa mbili zilizojengwa na watanzania zazinduliwa kwenye ziwa lenye mgogoro

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890
WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI ITUNGI KYELA MKOANI MBEYA



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Mhandisi huyo alisema mbali na kukamilika kwa mradi huo pia TPA imeingia mkataba na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 300 za mizigo. Mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho kamilika utagharimu sh. bilioni 9.12.
 
I remind u frankly. Mipaka yote duniani kwenye water bodies huwa ni katikati. Acha wapige kelele under exploitative powers we will procure our rights.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nimeipenda sababu Magufuli kaamua kuijibu Malawi kwa vitendo hii ndio kati ya miradi ya kwanza kabisa kuianzisha alipoingia ikulu,

Sasa kinachofata ni oil exploration kwenye Lake Nyasa
 
Ikumbukwe ndio meli za kwanza kuingia Lake Nyasa tokea liwapo tayari wameshapokea maombi lukuki ya usafirishaji kwa viwanda na biashara mbali mbali so far.
 
TANZANIA more than yesterday's
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…