Ubadilishaji wa fedha na soko la Hisa

Ubadilishaji wa fedha na soko la Hisa

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Posts
8,328
Reaction score
7,784
Hivi hii inakuwaje ubadilishaji wa fedha za kigeni na Soko la hisa?

Nimekuwa nikiona kwenye taarifa ya habari ya Star TV kuhusu ubadilishaji wa fedha za kigeni, je wana bureau au nikitaka kubadili kwao nafanyaje?

Msaada tafadhali.
 
Star tv ni chombo cha habari, hivyo wanachokifanya wao ni kuripoti tu na si kwamba wao ndio wanaofanya hizo biashara.

Ukitaka kununua fedha za kigeni popote pale ulipo tafuta sehemu imeandikwa Bureau de change.

Na ukitaka kununua hisa kuna brokers saba ambao ndio wanatambulika na serikali, hao ndio wanaweza kununulia hisa katika soko la hisa la dar. Kuna thread nyingi zimezungumzia hili, jaribu kuzitafuta.
 
Jamani bei ya madafu leo ikoje? Asanteni.
 
Hivi hii inakuwaje ubadilishaji wa fedha za kigeni na Soko la hisa?
Nimekuwa nikiona kwenye taarifa ya habari ya StarTV kuhusu ubadilishaji wa fedha za kigeni, je wana bureau au nikitaka kubadili kwao nafanyaje?

Msaada tafadhali

Kuuza na Kununua fedha za kigeni ni biashara kubwa sana kwenye masoko yaliyoendelea kama NYSE, S&P, NASDAQ, NIKKEI...
Wanachofanya wananunua currency moja toka soko moja ambapo inauzwa bei ya chini na kwenda kuuza kwenye soko jingine ambapo ipo juu...
Mfano unanunua €1=1$ unaenda kuuza €1=1.01$ soko jingine...
 
Star tv ni chombo cha habari, hivyo wanachokifanya wao ni kuripoti tu na si kwamba wao ndio wanaofanya hizo biashara.

Ukitaka kununua fedha za kigeni popote pale ulipo tafuta sehemu imeandikwa Bureau de change.

Na ukitaka kununua hisa kuna brokers saba ambao ndio wanatambulika na serikali, hao ndio wanaweza kununulia hisa katika soko la hisa la dar. Kuna thread nyingi zimezungumzia hili, jaribu kuzitafuta.

Mkuu nafahamu kuhusu Bureau D'Change, hapa nilikuwa nauliza kama na wao wana bureau yao maana rates zao zipo chini sana ukilinganisha na bureau de change nyingi
 
Kuuza na Kununua fedha za kigeni ni biashara kubwa sana kwenye masoko yaliyoendelea kama NYSE, S&P, NASDAQ, NIKKEI...
Wanachofanya wananunua currency moja toka soko moja ambapo inauzwa bei ya chini na kwenda kuuza kwenye soko jingine ambapo ipo juu...
Mfano unanunua €1=1$ unaenda kuuza €1=1.01$ soko jingine...

So na mimi mfano nikitaka kununua hizo currency lakini kama user tu sio kwa business naweza kwenda kwao hawa jamaa??
 
Mkuu nafahamu kuhusu Bureau D'Change, hapa nilikuwa nauliza kama na wao wana bureau yao maana rates zao zipo chini sana ukilinganisha na bureau de change nyingi
Sina uhakika ila nadhani wao huwa wanachukua rates za BOT kwakuwa wao ndio nchanzo rasmi kuliko kuchukua bureau fulani.
 
Back
Top Bottom