Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi hii inakuwaje ubadilishaji wa fedha za kigeni na Soko la hisa?
Nimekuwa nikiona kwenye taarifa ya habari ya StarTV kuhusu ubadilishaji wa fedha za kigeni, je wana bureau au nikitaka kubadili kwao nafanyaje?
Msaada tafadhali
Star tv ni chombo cha habari, hivyo wanachokifanya wao ni kuripoti tu na si kwamba wao ndio wanaofanya hizo biashara.
Ukitaka kununua fedha za kigeni popote pale ulipo tafuta sehemu imeandikwa Bureau de change.
Na ukitaka kununua hisa kuna brokers saba ambao ndio wanatambulika na serikali, hao ndio wanaweza kununulia hisa katika soko la hisa la dar. Kuna thread nyingi zimezungumzia hili, jaribu kuzitafuta.
Kuuza na Kununua fedha za kigeni ni biashara kubwa sana kwenye masoko yaliyoendelea kama NYSE, S&P, NASDAQ, NIKKEI...
Wanachofanya wananunua currency moja toka soko moja ambapo inauzwa bei ya chini na kwenda kuuza kwenye soko jingine ambapo ipo juu...
Mfano unanunua 1=1$ unaenda kuuza 1=1.01$ soko jingine...
Sina uhakika ila nadhani wao huwa wanachukua rates za BOT kwakuwa wao ndio nchanzo rasmi kuliko kuchukua bureau fulani.Mkuu nafahamu kuhusu Bureau D'Change, hapa nilikuwa nauliza kama na wao wana bureau yao maana rates zao zipo chini sana ukilinganisha na bureau de change nyingi
So na mimi mfano nikitaka kununua hizo currency lakini kama user tu sio kwa business naweza kwenda kwao hawa jamaa??