saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Mkoa wa Manyara uliundwa mwaka 2002 baada ya kuugawa uliokuwa mkoa wa Arusha. Bahati mbaya Baada ya Magufuli kupata urais wa Tanzania alitangaza wazi kuwa mikoa ya Kaskazini itabidi isubiri wakati mikoa mingine wakipelekewa maendeleo. Mwanzoni sikuamini, lakini sahivi ndio nimeamini ile kauli ilikuwa ya kweli na thabiti.
Masikini Mkoa wa Manyara, mkoa wa Manyara una maendeleo gani mpaka usubiri mikoa mingine? Wilaya ya Mbulu ni mojawapo ya wilaya iliyoko mkoa wa Manyara. Mji wa Mbulu ulianzishwa mwaka 1905 siku moja na mji wa Nairobi. Mpaka sahivi navyoandika mji wa Mbulu haujafikiwa na barabara ya lami. Ukiacha wilaya za Babati na Hanang ambazo makao makuu yamepitiwa na barabara za lami kwa sababu tu barabara hizi zinapita kuelekea mikoa mingine ya Dodoma na Singida. Wilaya zingine zote, yaani Kiteto, simanjiro na Mbulu km nilivyotaja ni vumbi tupu kuna nyakati hata hazipitiki. Mkoa wa Manyara hauna soko la kisasa, hauna Stand ya kisasa mabasi ni vumbi na kadogo kweli utafikiri stand ya kijiji nafikiri watanzania wanaopitaga Babati wanafahamu vizuri.
Mkoa wa Njombe ulianzishwa mwaka 2012 miaka 10 baada ya kuanzishwa Mkoa wa Manyara. Leo Njombe wana stand ya mabasi ya kisasa, wana soko la kisasa, Njombe(makao makuu ya mkoa) imeunganishwa na wilaya zake zote kwa barabara za lami. makete, Wang'ing'ombe na Ludewa zimeunganishwa na lami.
Rais samia anapita njia ilelile ya Magufuli hana lolote jipya ubaguzi uleule. Kwanini viongozi wanabagua maeneo ya nchi ileile moja wanayoiongoza? Wanachobagua ni kitu gani. Makabila yanayoishi ndani mikoa athirika? au Ardhi ya mkoa husika? Manyara imewakosea nini Marais wa Nchi hii? Ubaguzi ni dhambi mbaya sana, alituasa baba wa Taifa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu!!!