Ubaguzi wa rangi: Tangazo la nywele lasababisha maandamano

Ubaguzi wa rangi: Tangazo la nywele lasababisha maandamano

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waandamanaji nchini Afrika Kusini wamewalazimisha wenye maduka ya dawa na vipodozi kufunga maduka yao, baada ya kurushwa kwa tangazo la nywele ambalo wanadhani kuwa la ubaguzi wa rangi.

Tangazo hilo linaonesha picha za nywele za kiafrika zikiwa kavu na hazina muonekano mzuri wakati nywele za mtu mweupe zikionyeshwa kuwa nzuri na zinazovutia.
Chama cha upinzani cha 'Economic Freedom Fighters (EFF)' kimeliita tangazo hilo kuwa la kibaguzi na lisilojali utu.

Kiongozi wa chama hicho bwana Julius Malema ametaka maduka yanayouza bidhaa hiyo ya Clicks kufungwa.
Kampuni imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya chama hicho cha kisiasa lakini bwana Malema amewataka wafuasi wake kuwa tayari kwa mapambano na kusema EFF haiwezi kuogopa vitisho vyao.

"Tangazo hili linamtambulisha mtu mweusi kuwa yuko chini ya mtu mweupe.Haya ni madai yanayotoa sifa za uzuri wa mtu mweupe kuwa ya kiwango cha juu na kuelezea jinsi rangi nyeusi inavyowakilisha ubovu, ubaya au jambo kutokuwa sawa," taarifa ya EFF ilieleza.

Wanachama wa chama hicho , ambao huwa wanavalia mavazi ya rangi nyekundu ili kuonesha mshikamano na wafanyakazi, walifanya maandamano kama hayo mwaka 2018 dhidi ya nguo zinazotengenezwa na kampuni ya H&M baada ya kampuni kuchapisha jarida ambalo lilimuonesha kijana mweusi akiwa amevalia sweta lililoandikwa 'nyani mzuri zaidi msituni'.
 
Je vip kwa mfano ingekuwa vice versa, yaani za mwafrika ndio ziwe nzuri ?
nawaza tu lakini
 
Ila wanawake wengi wa kiafrika nao vichwa maji sana.

Kutwa kucha mnapishana saluni kwenye kushona miwig ili nywele zenu zifanane na za wazungu au races nyingine. Je hamuoni mna justify kwamba nywele zenu ni dhaifu ?
 
Wa

Wananunua hadi original blonde hair kwa bei mbaya kutoka Brazil, Mexico, Colombia na Ulaya ili waonekana kama wazungu. Urembo una uwanja mpana.😆 😆
 
Inferiority complex, unakuta wanaoandamana wakezao na dada zao wanaandamana wakiwa wamevaa mawig ya nywele bandia wameweka Brazilian Hair.
 
Ila wanawake wengi wa kiafrika nao vichwa maji sana.

Kutwa kucha mnapishana saluni kwenye kushona miwig ili nywele zenu zifanane na za wazungu au races nyingine. Je hamuoni mna justify kwamba nywele zenu ni dhaifu ?
Tatizo wanao penda wakiona anamwonekano huo humwongezea sifa
 
Naturally nywele za mwafrika chini ya jangwa la Sahara ni kavu na fupi,sasa whats wrong with ilo Tangazo??.
Ukiwa inferior kila kitu utaona ni ubaguzi tu..
 
Back
Top Bottom