Ipo hii moja, housegeli kaingia mjini hajawahi ona flushing toilet, mama mwenye nyumba hakumpa orientation housegeli. Mambo yakaendelea. Baada ya jua kali la siku wakiwa wametualia nyumbani, mama akaomba maji ya kunywa, akaletewa. Punde baba naye akaomba maji, akaletewa. Mara mtoto naye akaomba, housegeli akasema 'maji yenyewe yamekwisha kule kwenye chemichemi'.
Wenyenyumba: mmmmh! wakatahamaki, chemix2 ipi??.
housegeli: si ile pale kwenye kisima cheupeee
Wakabaki midomo waziiii? Nani alaumiwe???