Ubahili ni utajiri(Tuesday Thought)

Ubahili ni utajiri(Tuesday Thought)

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Nimekuwa shuhuda mzuri wa mafanikio ya watu wenye tabia za kibahili na binafsi nishawahi kujaribu kuwa mbahili kwa kifupi ubahili ni utajiri kuishi maisha ya ubahili sio kazi nyepesi inahitaji roho ngumu sana maana utakuwa ukiishi kinyume na jamii inayokuzunguka sababu utakuwa sio mwepesi wa kutoa michango mbalimbali kwenye jamii kama sherehe na hata pia misiba.

Hoja yangu ni kuwa kwa wale ambao wanahustle na still bado hawajafanikiwa wajaribu kuishi maisha ya kibahili ili kuweza kutimiza ndoto zao. Kwa mfano

1. Kama unamiliki smartphone ya 500,000 na kuendelea waweza kubadilisha na kutumia smartphone ya 100,000 ili kilichobaki uwekeze.

2. Kutotembea na kiasi ambacho ujaplan kukitumia.

3. Kukwepa kampani za watu ambao ukushawishi kutumia pesa kwenye anasa

Karibuni tupeane uzoefu na mbinu ambazo zinazoweza kutufanya kuepukana na janga la umasikini.
 
Kuna ku budget matumizi na plani zako alafu kuna ujinga unaitwa ubahili. Ubahili bila plan za kuwekeza ni ujinga.
 
Back
Top Bottom