Matukio ya ukatili wa kingono yanaendelea kuripotiwa nchini huku baadhi ya kesi zikihusisha watoto wadogo.
Leo, Septemba 2,2026, jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limetangaza kumkamata kijana mwenye miaka 21 anayeshukiwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye miaka 6 katika wilaya ya Mbarali. Kwamujibu wa Polisi, tukio hilo limetokea Agosti 28,2026.
Soma pia: Dkt. Gwajima: Vitendo vya Ubakaji na Ulawiti vimepungua kwa asilimia 6.3 na 19 mwaka 2024
Wiki zilizopita, mahakama kuu imemfungia maisha mtu aliyepatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa mwaka mmoja na miezi minne huko Pangani, Tanga.
Aidha takwimu za serikali zinaonyesha kuwa kesi zilizoripotiwa za ukatili wa kingono Tanzania zilipungua kutoka 12,749 mwaka 2024 hadi 11,625 mwaka 2025. Hata hivyo, idadi hiyo bado ni kubwa na inaonyesha kwamba tatizo halijaisha.
Je, adhabu kali pekee zinatosha kukomesha ubakaji na ulawiti, au jamii inapaswa kuongeza nguvu kwenye malezi, elimu ya watoto, ulinzi na utoaji wa taarifa?