Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Kulingana na Takwimu za ubakaji kwa kila Nchi 2021(Rape statistics by country 2021). Takwimu zinaonesha kuwa inakadiriwa asilimia thelathini na tano 35% ya Wanawake Duniani wamepitia ubakwaji, jaribio la ubakwaji, au usumbufu wa kingono katika maisha yao.
Katika Nchi nyingi zinaweka taarifa za ubakaji zinaonesha kuwa ni Wanawake wachache sana( chino ya asilimia arobaini 40% ya Wanawake wote Duniani wanaotafuta msaada wa kisheria baada ya kubakwa na chini ya asilimia kumi 10% ndiyo wanaotafuta msaada a kisheria.
Lakini pamoja na watu kusikia kila mara uhusiano na ubakaji kwa wanawake, wanaume pia wamekuwa wakipitia changamoto ya ubakwaji kila siku.
Wanawake wenye umri kati ya miaka 16 mpaka 19 ndiyo wahanga wakubwa wa matukio ya kubakwa Duniani, Wasichana waliofikia umri wa kuingia vyuoni yaani miaka 18 mpaka 21 hawa huwa hatarini mara tatu zaidi.
Marekani asilimia sabini (70%) ya matukio ya ubakaji hufanywa na watu wanaofahamika kwa wahanga. Takwimu zinaonesha kiwango cha ubakaji Marekani kuwa 27.3 lakini matukio ya ubakaji yamekuwa yakiwekewa usiri mkubwa kutokana na wahanga kuhofu, kuogopa kukaripiwa, kuogopa wanafamilia kufahamu, kesi kutokutiliwa uzito katika utekelezaji wa sheria. Inakadiriwa kuwa asilimia tisa 9% ya wabakaji walihukumiwa adhabu ya kifo, asilimia tatu 3% kuingia kifungoni huku asilimia ofisini na saba 97% ya wabakaji wakiwa huru mitaani.
Afrika ya kusini ndilo eneo linaloongiza kwa ubakaji Duniani kwani inakadiriwa uwa na matukio 132.4 ya ubakaji kwa kila idadi ya watu laki moja 100,000 ( 132.4 incidents per 100,000 people).
Utafiti uliofanywa na " South African Medical Research Council ulionesha inakadiriwa kuwa kwa kila mwanaume mmoja kati ya wanne walioshiriki katika kutoa taarifa za utafiti kufikiri kufanya tendo la ubakaji. Licha ya Bunge la Afrika ya kusini kupitisha na kuboresha sheria zinazohusiana na mahusiano ya kingono mwaka 2007 bado kiwango cha ubakaji kimeendelea kuongezeka.
Tanzania takwimu zinaonesha kiwango cha kesi 12.6 kwa watu 100, 000 kuripotiwa mwaka 2011 ,mwaka 2015 kiwango kilipungua na kuwa kesi 10.9 kwa watu 100,000. Mwaka 2016 Mamlaka ya Takwimu " National Bureau of Satatistics ilionesha kesi 7645 za ubakaji ambazo 7180 zilikuwa za Tanzania Bara na kesi 465 zikiwa za Zanzibar.
Hali hii inaonesha kupungua kwa kesi hakumaanishi kupungua kwa ubakaji ila kutokana na kasumba ya usiri na utekelezaji mbovu wa sheria katika Nchi mbalimbali ubakaji umeendelea kuwa mwiba na tatizo la kidunia.