Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
FURSA MBALIMBALI ZA UFADHILI WA MASOMO NA TAFITI ZILIZOPO NCHINI JAPAN
(SCHOLARSHIPS FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN JAPAN)
Ubalozi unapenda kutoa taarifa kuhusu uwepo wa fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo na tafiti nchini Japan, zinazotolewa na Serikali ya Japan na wadau wengine wa maendeleo waliopo Japan, kama ifuatavyo:
i) Serikali ya Japan kupitia Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (MEXT Scholarship);
ii) Programu za Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) — programu za JICA hutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa watumishi wa umma, wataalamu, wanasayansi na viongozi wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania;
iii) Mashirika binafsi ya Kijapani yanayotoa ufadhili wa kujitegemea kwa wanafunzi wa kimataifa; na
iv) Vyuo vikuu vinavyotoa ufadhili moja kwa moja (University-Specific Scholarships) kwa wanafunzi wa kimataifa.
Sehemu kubwa ya ufadhili huu unalenga masomo kwa ngazi ya Umahiri (Master’s) na Uzamivu (PhD). Aidha, Wizara ya Elimu ya Japan hutoa ufadhili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza (Undergraduate) na masomo ya Ufundi (Specialized Training).
Kwa taarifa zaidi kuhusu fursa hizo zikiwemo sifa za waombaji na taratibu za maombi, tafadhali tembelea tovuti:
a) UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN:
🔗 TAARIFA YA FURSA MBALIMBALI ZA UFADHILI WA MASOMO NA TAFITI ZILIZOPO NCHINI JAPAN (SCHOLARSHIPS FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN JAPAN) | Embassy of Tanzania in Tokyo, Japan