Ubalozi wa Japan unatangaza ufadhili wa masomo na tafiti nchini Japan

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039

FURSA MBALIMBALI ZA UFADHILI WA MASOMO NA TAFITI ZILIZOPO NCHINI JAPAN​


(SCHOLARSHIPS FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN JAPAN)

Ubalozi unapenda kutoa taarifa kuhusu uwepo wa fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo na tafiti nchini Japan, zinazotolewa na Serikali ya Japan na wadau wengine wa maendeleo waliopo Japan, kama ifuatavyo:

i) Serikali ya Japan kupitia Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (MEXT Scholarship);


ii) Programu za Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) — programu za JICA hutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa watumishi wa umma, wataalamu, wanasayansi na viongozi wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania;


iii) Mashirika binafsi ya Kijapani yanayotoa ufadhili wa kujitegemea kwa wanafunzi wa kimataifa; na


iv) Vyuo vikuu vinavyotoa ufadhili moja kwa moja (University-Specific Scholarships) kwa wanafunzi wa kimataifa.




Sehemu kubwa ya ufadhili huu unalenga masomo kwa ngazi ya Umahiri (Master’s) na Uzamivu (PhD). Aidha, Wizara ya Elimu ya Japan hutoa ufadhili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza (Undergraduate) na masomo ya Ufundi (Specialized Training).

Kwa taarifa zaidi kuhusu fursa hizo zikiwemo sifa za waombaji na taratibu za maombi, tafadhali tembelea tovuti:

a) UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN:
🔗 TAARIFA YA FURSA MBALIMBALI ZA UFADHILI WA MASOMO NA TAFITI ZILIZOPO NCHINI JAPAN (SCHOLARSHIPS FOR INTERNATIONAL STUDENTS IN JAPAN) | Embassy of Tanzania in Tokyo, Japan

 
Fursa hii hapa! Ngoja nichangamkie mapema.
 
Za nchini ufaransa,Italy,uk, uholanzi, Sweden, Austria, Switzerland zile nchi nzuri nzuri hizo balozi huwa hawatumi kabisa kwa watanzania Bali wanapeana wenyewe wenyewe.
Mfano Ile nafasi ambayo binti wa Omar mahita aliyo nayo kule USA ivi ilitangazwaga wapi na watanzania wangapi waliomba. Yaani adi damu imwagike kiasi gani ili watawala waweze kujifunza kutoa haki kwa wote sawa sawa na badala kukaa kuimba amani amani , toeni haki kwa wote. Nionyesheni ni wapi dereva anayetakiwa huko Italy ubalozini tangazo lilipo hata mfanya usafi ama sekretari jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…