Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Siyo kweli mkuu, wazungu ni wanajiona kuwa wao ni watu Bora kuliko wengine hasa linapokuja swala la Afya, hawana Imani na tiba zozote za Kiafrica, kuna rafiki yangu naye kwenda huko leo anasku ya tano akiwa karantin na bado atakuwa hivyo siku Tisa zijazo, Kwa tarifa za Jana usiku marekani anaambukizi ya watu 70,000 utasemaje hakuna maambukizi?
Huu ni uthibitisho tosha kuwa corona Marekani haipo, au uenda kuendelea kubaki Tanzania ni hatari zaidi ya kuwa na ugonjwa huu ukiwa united state of american
 
akili zingine za kijinga sana. Marekani haisemi kwamba kwao hakuna Corona. Wanachosema watu wao warudi kwao ambako itakuwa rahisi kuwahudumia.

wanaogopa mipaka ikifungwa na hali ikawa mbaya kwao wakiwa Tanzania itakuwa mgumu kuwasaidia.

wakati wa majanga unataka familia yako irudi nyumbani kwako ambako unaweza kuwasaidia.

Hivyo ndivyo nchi zinazojali watu wake hufanya.

Uko sahihi sana
 
Yaani WHO, dunia inatangaza kila siku halafu anatokea mtu mmoja kutoka Tanzania anakubali Corona haipo Marekani, acheni kusujudia watu kila saa kwenye kila kitu mzee, tuliza akili.

Au taarifa zinazotolewa na Trump mwenyewe kuhusu hali ya Corona nchini mwake huwa hauzisikii, basi tufanye ile siyo Corona bali ni homa ya Dengue
Watu wamekuwa wapumbavu kupindukia. mtu kama huyo anaweza sema pia wamarekani hawafi au hakuna kifo marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamesisitiza Kabisa kuwa Must return to US now. Na hii wameitangaza leo ila walishaanza kuwalazimisha raia wake waondoke Tanzania. Huu ugonjwa ni hatari halafu imagine uupate ukiwa Tanzania where our medical system is very poor. Hata kama ni mimi nina option ya kuondoka I will surely do so.

Something is not right somewhere.... Only great thinkers can understand.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Wapi wameandika ''must return now''???!!

It is NOT a 'must' return. They are 'encouraged' to return.

-Kaveli-
 
Wagonjwa wa Coronavirus Marekani ni 85,612 wakati wagonjwa wa coronavirus TZ ni 13. Wamarekani Walio bongo watachagua wenyewe, kusuka au kunyoa.
 
Cha kufanya Kwa selikari zetu za Kiafrica, ni kujilinda Sana na hao wazungu pindi watakapoanza kurudi, endapo janga hili halitaziathiri Sana nchi zetu hizi za Kiafrica basi kunauwezekano wa gonjwa hili kuwa ndio fimbo ya kuzichapia nchi zetu

Kwanza mpaka sasa gonjwa hili hatuamini kama si la kutengenezwa na hao ambao leo wanaitana kurudi makwao, na Kwa nini waitane ili hali hata kwao wameathirika?

Sasa basi kama ni kweli kwamba ngozi zetu nyeusi hizi virusi hawa wanashindwa kufanya kazi Yao sawasawa, tutawaaminije hawa watu pindi wanarejea, hatuwezi jua wanaenda kufanya Mbinu gani mpya? Je kuongezea makali ya virusi hawa ili na Sisi Africa tuje tuonje joto ya jiwe?

Kama hawatuamini na iwe hivyohivyo nasi pindi wanarudi tena? Wote tusiaminiane

Hawa mabingwa wa kutengenezwa magonjwa si wa kuwaamini hata kidogo
 
Wazo langu: Kuna gonjwa lingine soon litatimba Tanzania na tutasaga meno hii statement iko very clear kuna kitu kinakuja. So guys be prepared hawa watu sio wazuri kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa wito kwa raia wake kurejea Marekani, kufuatia uwepo wa maambukizi ya virusi vya #COVID19

Ubalozi umewataka raia wake wote wanaotaka kuondoka kufanya hivyo mapema kutokana na mashirika mengi ya ndege kusitisha safari. Umesema, hadi kufikia Machi 29, 2020 Shirika la Ndege pekee litakalokuwa na ndege za kutoka nje ya Tanzania ni Shirika la Ethiopia

Ubalozi huo umesema kwa sasa haushughuliki na kuwatoa raia hao nje ya Tanzania kuwarudisha Marekani, ila kama hatua hiyo itafikiwa umewataka wale wote watakaotaka kutafutwa na Ubalozi huo kutuma taarifa zao muhimu za utambulisho

Hadi sasa Marekani ambayo ndio nchi yenye maambukizi mengi zaidi, ina jumla ya maambukizi 85,594 yaliyorekodiwa na vifo 1,300

Marekani inataka uwazi na ichukuliwe hatua sahihi za kupambana na maambukizi, kama mnadharau na kuhamasishana kujazana kwenye nyumba za ibada, na kutegemea imani kutokomeza ugonjwa baada ya njia za kisayansi. Uhuru wa kupata taarifa na kutoa pia wanadhamini. Kukosekana hayo bora raia wao waende kwenye nchi yenye maambukizi mengi na taarifa zapatikana zao kutosha,.mie nawapongeza!
 
Sasa mbona hao wamarekani hawachukui "HATUA SAHIHI ZA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI "?.
Unataka kuzima moto kwa mwenzio wakati kwako kuna teketea?
Marekani inataka uwazi na ichukuliwe hatua sahihi za kupambana na maambukizi, kama mnadharau na kuhamasishana kujazana kwenye nyumba za ibada, na kutegemea imani kutokomeza ugonjwa baada ya njia za kisayansi. Uhuru wa kupata taarifa na kutoa pia wanadhamini. Kukosekana hayo bora raia wao waende kwenye nchi yenye maambukizi mengi na taarifa zapatikana zao kutosha,.mie nawapongeza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom