Ubalozi wa Marekani Saudi Arabia washambuliwa na ndege 2 zisizo na rubani

Ubalozi wa Marekani Saudi Arabia washambuliwa na ndege 2 zisizo na rubani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, umeshambuliwa na ndege mbili zisizo na rubani na kusababisha moto mdogo katika eneo la makazi ya kidiplomasia, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia.

Shambulio hilo lililotokea mapema Jumanne pia lilisababisha uharibifu mdogo wa mali katika eneo la ubalozi, wizara hiyo ilisema katika taarifa yake. Baadaye kulikuwa na taarifa kuwa ndege zaidi zisizo na rubani zilikuwa zikilenga eneo hilo huku Iran ikiendelea na mashambulizi ya kulipiza kisasi katika eneo la Ghuba kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel.

Rais wa Marekani, Donald Trump, aliliambia shirika la habari la NewsNation kuwa majibu ya Marekani kuhusu shambulio hilo la ubalozi pamoja na kuuawa kwa wanajeshi wanne wa Marekani yatawekwa wazi hivi karibuni. “Mtajua hivi karibuni,” alisema.

Mosho mweusi ulionekana ukifuka juu ya eneo la Diplomatic Quarter mjini Riyadh, linalohifadhi balozi mbalimbali za kigeni, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Watu watatu waliiambia Reuters kuwa mlipuko mkubwa ulisikika na moto ulionekana katika ubalozi huo, ingawa Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia na mmoja wa vyanzo hivyo walisema moto uliotokea baada ya shambulio hilo ulikuwa mdogo kwa kiwango.

Jengo la ubalozi halikuwa na watu wakati wa shambulio hilo, kwa mujibu wa watu wawili wanaofahamu tukio hilo walioliambia Reuters, na hakukuwa na taarifa za majeruhi.

Chanzo kilicho karibu na jeshi la Saudi, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kiliiambia shirika la habari la Agence France-Presse kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilidungua ndege nne zisizo na rubani zilizokuwa zikilenga eneo la kidiplomasia la Riyadh.

----------
The United States Embassy in the Saudi Arabian capital, Riyadh, was hit by two drones and a “limited fire” broke out at the diplomatic compound, the Saudi Ministry of Defence has said.

The strike on the US Embassy early on Tuesday also caused “minor material damage” to the compound, the Defence Ministry said in a statement, while there were reports later that more drones were targeting the site amid Iran’s retaliation across the Gulf to US-Israeli attacks.


US President ⁠Donald Trump ⁠told the NewsNation media outlet that the US response to the embassy attack and the killing of four American service members would soon be made clear. “You’ll find out soon,” he said.

Black smoke was ⁠seen rising over Riyadh’s Diplomatic Quarter, which houses foreign missions, after the attack, the Reuters news agency reports.

Three people told Reuters that a loud blast was heard and flames were seen at the embassy, though the Saudi Defence Ministry and one of the sources told the news agency that the fire in the aftermath of the drone attack was small in scale.

The embassy building was empty at the time of the attack, two people familiar with the matter told Reuters, and there were no reports of casualties.


riyadh.png
 
Dunia haiwezi kuwa salama kama hawa watu: Trump, Netanyahu, na Putin wataendelea kuwa viongozi wa nchi zao.
 
Dunia haiwezi kuwa salama kama hawa watu: Trump, Netanyahu, na Putin wataendelea kuwa viongozi wa nchi zao.
Ni lini dunia ilishawahi kuwa salama?
Miaka miaka nenda rudi watu wanapigana tu pakipoa huku panawaka kule
 
Back
Top Bottom