Tetesi: Ubalozi wa Misri kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje kuandaa sherehe ya kupongezana itayobeba kauli mbiu, 'Afrika tukiamua tunaweza'

Tetesi: Ubalozi wa Misri kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje kuandaa sherehe ya kupongezana itayobeba kauli mbiu, 'Afrika tukiamua tunaweza'

kamsi kilelo

Member
Joined
Mar 27, 2017
Posts
78
Reaction score
147
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mdau magogoni kwamba, Ubalozi wa Misri kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje wamendaa sherehe itakayowajumuisha wawakilishi wa nchi mbalimbali barani afrika kwa ajili ya kujipongezana juu ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa Stiglers Gorge baina yao.

Aidha mdau huyo ameeleza lengo kubwa la Sherehe hiyo ni kuhamasishana nchi zote za afrika katika kudumisha mahusiano na mashirikiano kwenye shughuli na miradi mbalimbali watakazokuwa wakizifanya ambapo kauli mbiu katika sherehe hiyo itakuwa "Afrika tukiamua tunaweza"

Aidha mdau huyo ameeeleza kwamba nchi za afrika zinatofautiana uwezo katika mambo mbalimbali na endapo zitashirikiana upo uwezekano wa miradi na shughuli mbalimbali zinazowahusu wakazimaliza wenyewe bila kulazimika kushirikisha mataifa ya nje ya Afrika.

Mdau huyo hakubainisha siku ya tukio hilo ila alisisitiza ni tukio ambalo limeanza kufanyiwa utekelezaji na ugawaji wa mialiko kwa nchi mbalimbali umeanza tangu tarehe 12/12/2018, aidha pia, ameeleza juu ya uwepo wa baadhi ya nchi za Asia na Ulaya kwa ajili ya kuongeza uhamasishaji juu ya mashiriano hayo ya nchi za afrika na pia kutoa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia katika utekelezaji wa kauli mbiu hiyo kama wadau wa maendeleo barani afrika.
 
Watashirikiana katika kulinda madaraka tu ya watawala lakini sio katika mambo yanayoweza kuifanya Afrika iondokane na umasikini.
 
Sherehe ya nini? Hiyo ela si ikajenge hospitali? We need consistency!
 
Itapendeza sana! lakini wanawaalika na hao tena? mmh sijui kama watahudhuria, na wakihudhuria itakuwa kishingo ...
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mdau magogoni kwamba, Ubalozi wa Misri kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje wamendaa sherehe itakayowajumuisha wawakilishi wa nchi mbalimbali barani afrika kwa jili ya kujipongeza juu ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa Stiglers George baina yao.
Aidha mdau huyo ameeleza lengo kubwa la Sherehe hiyo ni kuhamasishana nchi zote za afrika katika kudumisha mahusiano na mashirikiano kwenye shughuli na miradi mbalimbali watakazokuwa wakizifanya ambapo kauli mbiu katika sherehe hiyo itakuwa "Afrika tukiamua tunaweza"
Aidha mdau huyo ameeeleza kwamba nchi za afrika zinatofautiana uwezo katika mambo mbalimbali na endapo zitashirikiana upo uwezekano wa miradi na shughuli mbalimbali zinazowahusu wakazimaliza wenyewe bila kulazimika kushirikisha mataifa ya nje ya afrika.
Mdau huyo hakubainisha siku ya tukio hilo ila alisisitiza ni tukio ambalo limeanza kufanyiwa utekelezaji na ugawaji wa mialiko kwa nchi mbalimbali umeanza tangu tarehe 12/12/2018, aidha pia, ameeleza juu ya uwepo wa baadhi ya nchi za Asia na Ulaya kwa ajili ya kuongeza uhamasishaji juu ya mashiriano hayo ya nchi za afrika na pia kutoa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia katika utekelezaji wa kauli mbiu hiyo kama wadau wa maendeleo barani afrika.
Tetesi zilizopikwa ufipa.
 
Waafrika tunakwamishana sisi wenyewe kwa tamaa zetu;

Huwezi amini katika kizazi hiki Pamoja na mateso waliyotupa wazungu ;

Bado kuna vibaraka wanafurahia tukikwama.

Inasikitisha Mno
 
Umeanza vizuri kuwa ni mkutano wa Waafrika kwa Waafrika ila mwisho ukaharibu eti nchi za Ulaya nazo zinaalikwa
 
Back
Top Bottom