Nilipata matatizo makubwa tu. Kuanzia pale airport Athena na hapa Julius nyerere international airport..
Waliniweka pembeni kwamba passport fake..na nimetoroka inchini.
Uzuri nilikuwa na risiti,,nikawaambiya mpigieni Simu balozi wa Tanzania Italy,
Wakasema sio kazi yao.nisiwafundishe kazi.
Baadae wakanipa kesi ya kutoroka nchini.
Halafu mbaya zaidi jina langu limewekwa la baba na la baba ndy limeanza kama ndy jina langu..
Walinisumbuwa sana,,tangu alfajiri hadi saa saba mchana,ndy natoka ,,tena baada ya kuwatajia lost passport number yangu,,na siku niliyotoka hapo airport ,kuelekea Turky..
Walipoona najitambuwa,,wakaanza kuombaomba vitu vya kwenye bag langu mfano perfumes,, PESA nk.
Jamaa waliniudhi sana hapo airport,,
Mbaya zaidi walinikosesha mtoto mrembo sukari,,baada ya usumbufu huo wa passport.
Nikiwa Cairo , nilipata mrembo mmoja wa chuo ,,tulikutana hapo hapo Cairo wakati wa kubadilisha ndege,,
Mtoto mrembo mno,,
Alikuwa mwanachuo fulani Russia,, nilikuta anapiga Simu huku analia,, kilichonifanya nimsogelee ni baada ya kumsikia anaongea kiswahili,
Kumbe alikuwa amefiwa na baba yake huko bukoba,
Ikabidi tukawa friends kwa muda ule, tukakubaliana tukifika afikie kwngu kwanza next day aelekee bukoba.
Kufika dar nikawekwa pembeni,,
nikamwambiya mrembo nisubiri,,,
Nilipotoka nje sikumwona tena yule mrembo.
sikuweza kuwasiliana nae tena.,nadhani alinisubiri hadi akachoka.
Mrembo hakuwa na namba ya Simu wala mm sikuwa na namba ya Simu ,sote tulikuwa tunatoka ughaibuni,2011.
Walinikosesha mrembo Hawa jamaa kwa uzembe wao kule embassy ya Tanzania Italy na usumbufu wa hapo airport dar.
Hivi mtu akiwa na passport ya dharura hapa Tanzania pia ni kesi?